Kupandikiza Uume Hospitali ya Benjamin Mkapa ni Tsh. Milioni 6 hadi 10

Wanawake wengi wañateseka sana sana!
Nyingine zimekuwa sugu hata uchane wembé damu haitoki!; wanaovaa pampass usihesabu, zamani unashika kitasa unanyonga ndio ufungue mlango!; siku hizi ukilenga kidole kwenye mlango tayari mlango umesha funguka.....
Aisee
 
Eleza vizuri kupandikiza kivipi, kurekebisha uliopo, au kutoa kuweka mwingine, au hata kwa mwanamke wanapandikiza anakuwa mwanauume.
 
Eleza vizuri kupandikiza kivipi, kurekebisha uliopo, au kutoa kuweka mwingine, au hata kwa mwanamke wanapandikiza anakuwa mwanauume.
Unawekwa wa mtu mwingine ambaye amejitolea au alifariki bila mtu kujitokeza viungo vinatolewa ipo sana nje
 
Hospitali ya Benjamin Mkapa imetaja gharama za kupandikizwa uume kuwa ni kati ya Sh6 milioni hadi Sh10 milioni.

Hayo yamesema leo Jumanne Agosti Mosi mwaka 2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Dk Alphonce Chandika wakati akielezea vipaumbele vya bajeti kwa mwaka wa fedha 2023/24.

Dk Chandika amesema huduma hiyo imeanzishwa baada ya kubaini kuwa kuna changamoto kubwa ambayo imewafanya waganga wa kienyeji kupita mitaani na dawa zinazodaiwa kutibu tatizo hilo.

“Sisi kama taasisi ya umma tukaona kwanini tusije na mkakati wa kuwasaidia hawa watu wenye changamoto kwenye nguvu za kiume. Kwa maana hiyo tulianza kutoa hii huduma kwa kutoa huduma kwa wanaume wawili,” amesema.

Amesema habari njema kutoka kwa wanaume hao, mambo yamekuwa mazuri na kwamba waliwapa masharti kuwa waanze kufanya tendo la ndoa wiki sita baada ya kufanyiwa upasuaji.

“Hizo ni taarifa kutoka kwao wenyewe kwasababu tuliendelea kuwafuatilia, wametuambia matukio ni mazuri sana na wamefurahi sana kwa sababu yamerejeshewa uwezo wao. Imerejesha heshima katika familia zao,”amesema.

Amesema hivi sasa wako katika mkakati wa kupanua wigo wa huduma ili kuifanya ipatikane kwa kila anayehitaji.

Amesema taasisi inayozalisha vipandikizi hivyo imesogeza huduma zake Dar es Salaam na hivi sasa inafanya usajili ili viweze kupatikana kwa urahisi.

Dk Chandika amesema baada ya wao kuanza kutoa huduma hizo ni matumaini yao kuwa na hospitali nyingine zitaanza kutoa huduma hiyo kwasababu mahitaji ni makubwa.

Amesema gharama za matibabu hayo sio kubwa ukikilinganisha na tabu anayoipata mtu.

Amesema gharama ni kati ya Sh6 milioni hadi Sh10 milioni tofauti na nje ya nchi ambazo zinatoza hadi Sh50 milioni.

Aidha, Dk Chandika amesema katika mwaka wa fedha wametengewa Sh64.52 bilioni na kwamba Sh18.62 bilioni zitakwenda katika miradi ya maendeleo ili kuendelea kuwapunguzia wananchi adha ya kusafiri mbali kupata matibabu.

Ameitaja miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa jengo la saratani, jengo la matibabu ya moyo na kifua kwa watoto na watu wazima, kituo cha upandikizi wa figo.

MWANANCHIView attachment 2705187
Wangefanya such surgeries kwenye mbongo za viongozi wetu ziweze kufanya kazi vizuri na kuwawezesha kufikiri productively ili kuharakisha maendeleo na kusaidia kuiepusha nchi na mikataba aina ya DP World
 
Back
Top Bottom