Kupaka mafuta ya nazi kuna tatizo?

Mweusi Mweupe

JF-Expert Member
Mar 21, 2017
332
322
Mie ni kijana wa 35+, nina mke na watoto wawili.

Lakini kwa ushauri wa mke wangu, kutokana na ngozi yangu kuwa ngumu na isiyovutia machoni mwake ndo akaniletea mafuta ya Nazi nianze kuyatumia. Na wakati mwingine yeye ndo hunipaka.

Sasa tatizo limeanza kujitokeza kwa maana kila nikipita mtaani nimekua mjadala kwa wanawake, wazee wenzangu na hata watoto.

Msaada wenu wana JF kwani kupaka mafuta ya nazi ni dhambi?
 
Mafuta ya nazi ni mazuri,. Mwambie awe anakutengenezea mwenyewe na kuchanganya na baadhi ya vitu. Ili kutoa harufu ya nazi. Mimi huwa natumia. Ni mazuri sana
 
Mie ni kijana wa 35+, nina mke na watoto wawili.

Lakini kwa ushauri wa mke wangu, kutokana na ngozi yangu kuwa ngumu
sasa mkuu kijana inakuwaje unakuwa na ngozi ngumu ina maana wewe umekuwa kenge...


Dawa nzuri ya kupaka ni MAFUTA YA UBUYU
 
huyo mke wako safi sana, mpe salamu zangu kuliko angekuteta una ngozi ngumu kakuletea na solushen kbs
 
kama katengeneza mwenyew maweeeee iyo harufu yake mhmh
kanunue ya dinamarios nasikia hayana harufu na ni mazuri
Yakutengeneza mwenyew ni mazuri zaid anaweza akayaweka asmin au vilua karafuu vyovyote upendavyo
 
napenda sana harufu ya mafuta ya nazi yale ninayo yatengeneza mwenyewe! najipakaa mwili mzima km mtoto mchanga najisikia rahaaaaaa
 
Kama unayapaka usiku ukiamka asubuhi unaoga unapaka lotion nafikiri hakuna tatizo,hivyo basi jichunguze upya kwa nini umekua gumzo mtaani
 
Sasa tatizo liko wapi apo mkuu??tatizo ukipaka ayo mafuta yanatoa haruf??au tatizo ni kua unang'ara sana ukitoka nje kutokana na kupakwa ayo mafuta au tatizo ni lipi
 
Mafuta ya nazi ni mazuri,. Mwambie awe anakutengenezea mwenyewe na kuchanganya na baadhi ya vitu. Ili kutoa harufu ya nazi. Mimi huwa natumia. Ni mazuri sana

Vitu gani hivyo?
Nauliza sababu mi na familia ni watumiaji wa hayo mafuta.
Ninatengeneza mwenyewe na ninataka nipunguze harufu.
 
Back
Top Bottom