Kuongeza Mwili: Muongozo wa Mazoezi na lishe (Gym workout & Diet)

Asante
 
Hakuna mazoezi kwa sisi wanawake wembamba angalau kutiatia nyama!😊
Wewe piga msosi mwili utakuja, pili punguza stress. Ukiwa na stress huwezi ongezeka.

Mwaka 2017 nilienda stationary moja nikakutana na mdada kavaa kitenge kimemchora balaa alikuwa na kashape kama nyigu. Kumbe nae alitamani mguu wangu.

Wakati natoka akanambia dada una nguu mzuri akasema 'nikiwa na mguu kama wako ntavaa vimini wakome.' Nikamwambia hata wewe hiyo shape sio ya nchezo tukacheka.

Akanambia yeye anafanya mazoezi ya squats nikamuuliza ndo yapi? Akanielekeza.

Siku nyingine nikaenda nae kwangu majirani wadada nao wakamuona alipotoka wakamsifia ana shape matata.
Si akaanza kunifundisha hizo squats weeee niliumia miguu mpaka nikahisi nguu wangu utaisha.
Nikaendelea kufanya ila nikawa na mashaka hiki kishape chake utadhani kaongea na mungu mbona sielewi?
Tumikono kwake na miguu twembambaaa sana ila kishape kile nikajisemea moyon hapana kuna kitu.
Nikazidisha ushoga.mara siku moja akapoteza funguo nikamwambia njoo ulale kwangu.

Nikamwambia leo tupige zoezi ndo tukaanza up down up down mm hap nimevaa ki tait tu tuko wawili. Hapo kavaa mgauni wake wa kanisani kavalia tait ndefu nikamwambia si uvue mgauni tupige zoezi kakataa.mmmh??

Tukamaliza zoezi nikaoga nikamwambia na wewe oga yesuuuu kristo dada kaenda na nguo zote alizokuwa kavaa nikampa kitenge cha kuogea. Akaoga akamaliza akavaa ile gauni yake tena huko huko bafuni mmmmmh!

Nikamuuliza na hilo jasho si uvae hiyo nguo nilizokuwekea hapo? Kagoma.
Kuuuuuuuumbe ana kigodogoooooo anaogopa kuvua nikamuona.
Tukalala asubuhi akaenda kuoga tena kamalizia kila kitu bafuni .aiiiiiiiiiiiiiiiiiiikumbe mm kuangaika kote napambana na mtu aloweka kigodogo? Ishiiiiiiiii niliacha mazoezi ya nini kujitesa ishiiii.

Nikajisemea moyoni lazima nimkomeshee aache kuvaa kigodoro.
Nikamuunganisha kwa kaka mmoja hivi ambae hapendi madude ya kujiongezea ,kweli kadada ni kazuri si akakapenda ahaaaaa😂

Nikamstukiza akiwa kazini nikampeleka amuone mchumba.kaka kadata na shape. Moyoni nikajisemea nyooooo majibu utanipa mwenyewe.
Siku ya siku ameshamtoa out za kutosha sasa ikaja muda wa malipo aiiiiiiiiiiiiiii kumbe kigodoro? Mkaka nikamsanifu ' we fala nimekupa demu mkali chura kama yote!😂😂😂😂 si ndo karopoka kigodoro aiiiiiiiiiii
Nanina zake.
 
Wanawake wengi hawataki kupunguza mwili unakuta anataka atowe tumbo tu.na wengi wa hivi hawawezagi mazoezi je mkanda unaweza punguza tumbo ili siku nikipata kitambi nijifungie zangu mkanda
Sasa unapunguzaje kitambi bila kufanya mazoezi ya kubalance mwili mzima?!

Ila sipendi mwanamke anaejiachia kama kitimoto huwa nachukia.... Halafu ukute unamuelekeza taratibu kuwa hiyo hali aliyonayo sio sahihi yeye anakuletea upuuzi wa kutetea unene wake kuwa ndivyo alivyo...... Msyuuuuuu
 
mada nzuri sana,nimejifunza kitu hapa ,kwa wale wanao taka kuongeza body mass au kujenga mwili,kitu cha kwanza kabisa ni kuweka mpangilio wa chakula hasa calories kama ilivyo tajwa hapo juu. baadhi ya wengi wetu hatuna uwezo wa kupangilia budget ya chakula au kupenda kula kwa wakati ,hii inafanya mwili kudhoofika kwasababu baadhi ya watu wana high metabolism yaani namaanisha mfumo wa mwili unakuwa una reaction kubwa sana kumenge'nya chakula,unakuta mtu akila chakula anawahi sikia njaa haraka,kwaiyo basi watu kama hawa ina bidi kula vyakula vya caloriries yaani mafuta kwa wingi ili kuweka surplus ya calories mwilini ili itumike kujenga na kukuza mwili kwa haraka na baadae mazaoezi ya kukata mwili hufanywa.

hivi ni baadhi ya vyakula vinanyojenga na kukuza mwili kwa haraka kwa wale slim au wembamba.
calories food
1.Korosho

2.Karanga

3.Siagi ya karanga (peanut butter)

4.parachichi

5.maziwa

na baadhi ya vyakula vya protini
6.nyama ya ngom'be
7.nyama ya nguruwe
8.nyama ya kuku.
9.mayai
 
Unene wa asili huu

mwanamke kuwa na is not romantic hata kodogo I can't imagine mkeswangu atakula doso
 
Mchawi muda mzebaba we piga hesabu hapa nna wiki yapili sasa sjapumzika hata siku moja leo ndo nimemaliza kazi kibaha now narudi home kesho mapema eidha boti ya saa moja au saa tatu navuka maji zanzibar kuna kazi ya wiki mbili sasa kwa mfumo huu wa maisha siunaona kama kipengele?
 
Tafuta Koni Na Tafuta mazoezi yake. Unaweza kufanya mazoezi yake hata sebuleni.

Mazoezi ya Koni Ni mazoezi konki Sana hata baunsa anaweza kukimbia Sio mchezo.

Hata wachezaji wa mpira kwenye mazoezi ikifika session ya mazoezi ya Koni huwa wanachapa lapa.

Kwahiyo ni wewe tu tumia huo muda wako vizuri. Andaa nusu saa ya mazoezi ya Koni
 
Unless kama mtu anatumia supplements lakini akifanya kila kilichoandikwa pale kila siku bila kukosa kwa sets zinazotakiwa hatajaza mwili ila ataukata na misuli itadumaa kwakua haipati muda wa kupumzika. Kama uko bulked it's fine ila mwembamba hapana.
Chief

Suppliments hazina madhara kiafya?
 
Chief

Suppliments hazina madhara kiafya?
Nilishaandika uzi kwa ajili ya hiyo deal.

Jibu ni "Ndiyo" na "Hapana"

Kutegemea na unayotumia, namna unavyotumia, na routine yako nzima inaweza kuangukia kwenye ndiyo au hapana.

Nimegoogle ili niupate uzi kirahisi badala yake nimekuta hivi


Moderator rudisheni baadhi ya nyuzi mlizonifutia nashindwa kumpa mtu reference.
 
Nimekuwa mrefu sana na nimepungua mno

Nimekuwa kwenye uhitaji wa kuongeza kidogo kamwili nimejaribu kufuatilia protein suppliments hususani whey lakini Bado kuna hisia nyuma inanisukuma nisitumie
 

Mkuu mimi na tatizo la tumbo nataka lipungue tuna fanyaje?
 
Nimekuwa mrefu sana na nimepungua mno

Nimekuwa kwenye uhitaji wa kuongeza kidogo kamwili nimejaribu kufuatilia protein suppliments hususani whey lakini Bado kuna hisia nyuma inanisukuma nisitumie
Mkuu ni kaishu karefu ila kwa ufupi ni hivi;

Tumia supplements kwa vipindi, mfano unatumia miezi 3 kisha unaacha kwa miezi 2 au 3 kabla ya kuanza tena.

Pia kunywa sana maji kipindi unatumia supplements, angalau lita 5 kwa siku.

Pia jua kwamba supplements siyo replacement ya chakula so ration ya chakula ibaki palepale.

Pia hutakiwi kuacha kufany mazoezi, in fact kwa sasa ndiyo inabidi udouble struggle hustle..

Whey protein siyo supplement ya hatari kama baadhi mfano steroids. So waweza tumia whey protein bila kufanya hii rotation. Whey protein ni supplement ya kawaida isiyo na madhara.

So tumia whey haina ishu unayoifikiria. Ukianza kuzijua zile nyingine hapo sasa itabidi ufanye rotation.
 
Whey protein unapatikana wapi mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…