Kuombwa mchango wa harusi na mpenzi mliyeachana

kiborinangai

Member
Mar 11, 2016
17
5
Habari wanajamvi,

Naomba kuleta uzi huu kuomba ushauri,

Eti ni sawa kuachana na mpenzi wako alafu anakuja kuolewa anakuomba mchango wa harusi yake?
 
Habari wanajamvii
naomba kuleta uzii huu kuomba ushaurii
eti ni sawa kuachana na mpenzi wakoo afu anakuja kuolewa anakuombaa mchangoo wa harusi yake
Binafsi nilishamlipia na matibabu ya oparation kazidiwa na huyo mume wake hana kitu,gharama zikawashinda mwanamke akanipigia kuniomba msaada na nikaenda kulipa tsh laki9.so mchango wa harusi ni jambo ndogo tu ndugu!
 
Mpe tena bila kinyongo.

Kuna mtu niliachana nae (alinipiga kibuti) bahati mbaya fikra zake zikamtuma tumegombana. Siku moja alinipigia simu akaniomba nimkopeshe hela kagota. Nikamtumia tena ndani ya Muda mfupi.

Alipotaka kurudisha nilimwambia "ulikuwa msaada kwangu kwa kipindi tulipokuwa pamoja. Hiyo ni ahsante yangu kwako."

Hadi kesho huyu dada "heshima yake" kwangu ni kubwa.
 
Hiyo hela ya masimango ngekua mm ngerudisha tu
 
Inategemea kama mm nilimuacha afu kaomba mchango natoa ila mshenz alinitema mbavu zao harusi wapike dona NO DONATION AT ALL
 
Mie kuna demu alinimwaga vibaya halafu after a year ananiomba mchango wa send off. Nilimwuliza nimpe kama nani? Akasema eti rafiki. Nikamwambia sinaga utafiki na ex wangu. Na pia, sinaga ex. Kama ulinizungua, we'd never met before.
 
Habari wanajamvi,

Naomba kuleta uzi huu kuomba ushauri,

Eti ni sawa kuachana na mpenzi wako alafu anakuja kuolewa anakuomba mchango wa harusi yake?
tena wewe ndio unatakiwa utoe zaidi ili uonyeshe kua umeridhika na mamuzi yake na na unampongeza,hata tv ya inch 60 pia unaweza muongezea zawadi kudumisha upendo........
 
Kama ulimgegeda kipindi mko wote hapo ni haki yake kudai mchango ila kama alikua anakuzingua kukupa papuchi mpotezee.
 
Back
Top Bottom