Upi ni mtizamo wako kuhusu ndoa?

Upi ni mtizamo wako kuhusu ndoa?

Credio

Member
Joined
Aug 24, 2016
Posts
12
Reaction score
19
Habari wana jamii.

Nimeanza na hilo swali kwasababu ya kisa ambacho nahitaji kumpa mtu ushauri

Je, upi ni mtizamo wako kuhusu ndoa?
1. Uoe au uolewe kwaajili ya kupenda/kupendwa au
2. Uoe au uolewe kwaajili ya connection, future na fursa zinazofuatia
Hapa naomba nieleze kidogo

Ki historia watu wenye nguvu/mamlaka mara nyingi watoto wao walioa au kuolewa kwaajili ya kukuza power, utajiri na mamlaka ili vizazi na vizazi vinavyofuatia visijepata kadhia au shida. Na ndio maana huwezi kukuta mtoto wa GSM au Mwinyi ameolewa na nobody eti kisa mapenzi.

Na ndio maana mara nyingi ndoa zao zinakuwa arranged, hivyo kupenda au kupendwa utakukuta huko huko ndani ya ndoa.

Lakini hata zamani wazazi wetu kabla ya binti yao au kijana who kuoa au kuolewa walikuwa wanafanya uchunguzi kuhusu historia ya familia, magonjwa ya kurithi, imani, uchapakazi na uadilifu n.k na ndio maana ilikuwa rahisi wao kupoint uende sehemu au familia flani ukaoe au kuolewa kwasababu kuna gain utazipata

Ila hili la kuoa au kuolewa kisa kupendana mm siliafiki kwasababu vipi mapenzi yakiisha kipi kitawaunganisha l, hili limesababisha divorce rate iwe kubwa na ongezeko la single mothers na single fathers.

Wengine wamefikia hatua ya kupenda harusi zaidi bila kujiandaa kuhusu ndoa.

Na ndio maana mwingine unasikia mi nataka harusi yangu ashereheshe Gara B na shela litoke uturuki, na barnaba aje kuperfom.

Upi mtazamo wako wewe mwana jamii
 
nasubiri maoni :peepoSit:
IMG-20260610-WA0057.jpg
 
Ndoa ni muunganiko wa hisia, imani, upendo, na baiolojia kwa lengo la kutengeneza familia na kuendeleza ufalme wa Mungu duniani
 
Ndoa ni Pesa.
Mnaweza kuanza vizuri na upendo wenu wa kula nyanya chungu na ugali lakini mkaishia kuachana baada ya mmoja wenu kushindwa kuvumilia umasikini wa kuishi chumba kimoja.
 
Ndoa ni Pesa.
Mnaweza kuanza vizuri na upendo wenu wa kula nyanya chungu na ugali lakini mkaishia kuachana baada ya mmoja wenu kushindwa kuvumilia umasikini wa kuishi chumba kimoja.
Sio kweli
 
Kwan kuish singo rumu ni umaskin?
Ndoa ni Pesa.
Mnaweza kuanza vizuri na upendo wenu wa kula nyanya chungu na ugali lakini mkaishia kuachana baada ya mmoja wenu kushindwa kuvumilia umasikini wa kuishi chumba kimoja.
Ku
 
Ndoa ni jambo la asilia so usibabaike na material things ,dunia umevurugwa ila kizazi hiko cha sasa hakifai...kikubwa muendane tu ,na kila mtu atumikie ndoa .

Ninachojua hayo mambo ya kupendana wala hayapo kabisa ,mimi naelewa haya mambo tangu mtoto ndio maana sijawahi kuwa na mahusiano wakati nasoma ...Ninachojua siwezi kuoa mtu wa mbali labda wa karibu hata wazazi wanamjua hata wangechagua fresh ....

Hizo nyash na sura au rangi kawaida sana huku kwetu hakuna kipya ,maisha ya kugombana ni kawaida ..Umri nao umesogea kila kitu naona kawaida ,hata kusema nitamani mwanamke naona kama ni utoto ,kutembea na vitoto hivi Gen Z naona bado vinanuka kamasi.

Ndoa nyote muwe na akili ,utoto unasumbua kila mtu ana type yake so kama hamuendani kwisha ..Ila nilioka mtu anasaliti mke naona bado mtoto sana na akili yake ina ujinga sana ,hawa wanawake ni kukamilisha asili sio kujifanya kibora chunya ;unajichoresha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom