Kuolewa

Kuolewa kuna maana gani?
Mwanaume anaposema 'siwez kupika (mfano) kwani mi ndo nimeolewa?'
Does it mean kuolewa haina tofauti na kua mtumwa wa mwanaume?
Does it mean wanaume wanaoongea hayo hawajui maana ya kuoa?
What does kuolewa mean?[Nameless Girl (NG) hebu soma maandiko matakatifu yanasungumza nini juu ya ndoa, ukisha soma utangundua nini maana ya ndoa. Lakini pia ulisha jiuliza ki-unagaubaga juu ya mahari ilitolewayo kwa wanawake watakao kuolewa?]
 
Ndo maana mimi kuolewa sitaki, nataka KUOANA!!!!!!!!!!! LOLEST!

basi wewe kwa hapa AFRCA "utataka" sana! yaani utaendelea kutaka hadi hapo utakapojua uhalisia kwamba haiwezekani kuoana kwa maana ambayo wewe unaitaka then utaolewa!
 
ninaweza kua nimekosea, so definition yako itanipa kitu kipya in my mind.

Hahah!!!

Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 kifungu cha 9, kinatoa tafsiri ya ndoa kama ifuatavyo:

Ndoa maana yake ni Muungano wa hiari kati ya mwanaume na mwanamke unaokusudiwa kudumu kwa muda wa maisha yao yote

Sheria hii ya ndoa katika 'kifungu cha 63' inaendelea kufafanua yafuatayo kuhusiana na wajibu wa mke na mume ndani ya ndoa kwa habari ya kutunzana.

Katika ndoa mume anao wajibu wa kumkimu mkewe kwa kumpatia malazi, Nguo na chakula, na mke mwenye kipato vile vile anao wajibu wa kumkimu mumewe ikiwa mume huyo:

  • Hajimudu kabisa.
  • Hawezi kupata chumo la Maisha yake kwa sababu ya athari ya akili au afya mbaya
 
hahahahaaa! hata unachokiandika ni matokeo ya mfumo dume wenye mizizi mirefu sana. kwa sababu hujengwa toka tukiwa watoto, wala hatuoni kuwa ni tatizo. we take it for granted.
ndo maana hata wanawake wenye kipato kikubwa kuliko waume zao, bado hudai matumizi na mahitaji yao binafsi kutoka kwa waume zao wakiamini kuwa wao(wanawake) ni watu wa kutunzwa. pia wanaume wengine huamua kuwachisha kazi wake zao kwa sababu wao(waume) wana "wajibu" wa kuitunza familia. mwanaume amefanywa aone kwamba ana wajbu wa kuhakikisha familia yake inapata mahitaji yote ikiwa ni pamoja na uliyoyataja. kwa upande mwingine, mwanamke amefanywa ajione ni wa kutunzwa, kudekezwa, n.k hivyo, mume akishindwa kutimiza majukumu ya " kichwa cha nyumba," yafuatayo yanamhusu:

1. mkwewe atamwita mwanaume suruali, hivyo dharau kwa kwenda mbele kutoka kwa mkewe, ndugu wa mke na hata watoto wake na majirani

2. hata mwanaume mwenyewe hawezi kujisikia vizuri kwani anaona "kashindwa" kutimiza wajibu wake. hali hii hutokea hata kama mke ana hela, anaprovide for the whole family na wala hamnyanyasi mume wake.

sikwenda upande huu kwa sababu ningekuwa out of the topic mkuu
Wala usingekuwa nje ya mada mkuu kwasababu mada inaongelea kuolewa hivyo "muoaji" na "muolewaji" atakuwepo. Kiuhalisia, hata iwe kwenye utamaduni upi lazima kuna wajibu ya mume na wa mke kwenye ndoa. Dhana ninayoikataa mimi ni kuangalia wajibu wa mtu mmoja katika hiyo ndoa na kuhitimisha kuwa ni mtumwa kwa sababu ya wajibu alionao (iwe ni kwa sababu za kitamaduni, kisheria au kijamii). Hizi wajibu mara zote ni tofauti na zinahitaji energy tofauti hivyo assessment ya nani ni mtumwa na nasi sio inategemea familia na familia, jamii na jamii etc
 
usiumize kichwa kujiuliza itakuaje, sina mpango wa kuwa 'slave'.

Inaonekana hata nilichoandika hujakielewa

Na kikubwa zaidi usichokielewa ni kuwa sijaumiza kichwa
Halafu hujui ukweli siku ukijua hutaongea haya maneno yako

Subiri muda uongee

Kila la kheri!
 
Inaonekana hata nilichoandika hujakielewa

Na kikubwa zaidi usichokielewa ni kuwa sijaumiza kichwa
Halafu hujui ukweli siku ukijua hutaongea haya maneno yako

Subiri muda uongee

Kila la kheri!

Refer post yako.
Sijacopy ulichosema, nimecomment uliyoyasema.
Upo?
Usiku mwema.
 
Hahah!!!

Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 kifungu cha 9, kinatoa tafsiri ya ndoa kama ifuatavyo:

Ndoa maana yake ni Muungano wa hiari kati ya mwanaume na mwanamke unaokusudiwa kudumu kwa muda wa maisha yao yote

Sheria hii ya ndoa katika 'kifungu cha 63' inaendelea kufafanua yafuatayo kuhusiana na wajibu wa mke na mume ndani ya ndoa kwa habari ya kutunzana.

Katika ndoa mume anao wajibu wa kumkimu mkewe kwa kumpatia malazi, Nguo na chakula, na mke mwenye kipato vile vile anao wajibu wa kumkimu mumewe ikiwa mume huyo:

  • Hajimudu kabisa.
  • Hawezi kupata chumo la Maisha yake kwa sababu ya athari ya akili au afya mbaya

Thank you sir.
 
Kuolewa kuna maana gani?
Mwanaume anaposema 'siwez kupika (mfano) kwani mi ndo nimeolewa?'
Does it mean kuolewa haina tofauti na kua mtumwa wa mwanaume?
Does it mean wanaume wanaoongea hayo hawajui maana ya kuoa?
What does kuolewa mean?[Nameless Girl (NG) hebu soma maandiko matakatifu yanasungumza nini juu ya ndoa, ukisha soma utangundua nini maana ya ndoa. Lakini pia ulisha jiuliza ki-unagaubaga juu ya mahari ilitolewayo kwa wanawake watakao kuolewa?]

Umeongelea maana ya ndoa.
Naongelea maana ya kuolewa mpendwa.
 
Wala usingekuwa nje ya mada mkuu kwasababu mada inaongelea kuolewa hivyo "muoaji" na "muolewaji" atakuwepo. Kiuhalisia, hata iwe kwenye utamaduni upi lazima kuna wajibu ya mume na wa mke kwenye ndoa. Dhana ninayoikataa mimi ni kuangalia wajibu wa mtu mmoja katika hiyo ndoa na kuhitimisha kuwa ni mtumwa kwa sababu ya wajibu alionao (iwe ni kwa sababu za kitamaduni, kisheria au kijamii). Hizi wajibu mara zote ni tofauti na zinahitaji energy tofauti hivyo assessment ya nani ni mtumwa na nasi sio inategemea familia na familia, jamii na jamii etc

you're very right. kwa jamii zingine, wanawake huonekana wanatumikishwa na huo utamaduni wenye mfumo dume. kuna vitu wanawake wengine hufanyishwa ndani ya familia zao hadi unajiuliza kama yeye ni mtumwa au mke. however, kwake inaweza kuwa sio tatizo na atakwambia huo ndio utamaduni.

mtoa mada anaonyesha kuhoji uhalali wa utamaduni huo katika jamii zetu. mfano, mume na mke wamekwenda shamba alfajiri. mke anabebs mtoto mgongoni, ndoo ya maji kichwani. mkono mmoja ameshika gelani na mkono mwingine ameshika kikapu chenye chakula/kifungua kinywa. mume kavaa koti lake, amebeba panga na jembe huku akitembea mbele au nyuma akipiga mluzi. watalima weeee. jioni wanaporudi, mume anabeba gogo moja pamoja na panga. jembe anamwachia mke mwenye mtoto mgongoni, mzigo wa kuni kichwani uliofungwa pamoja na majembe mawili: lake na la mumewe. juu ya mzigo wa kuni kuna koti la mumewe. mkono mmoja amebeba gelani yenye maji. wakifika nyumbani mke huyu huyu amwandalie mumewe maji ya kuoga, aandaye chakula, amlishe mtoto.........majukumu ni mengi. ukimuuliza atakujibu ni utamaduni . utamaduni my nose!

anyway, you may take it or leave it lakini kuna mambo yanawaumiza sana wanawake
 
Nakubaliana na wewe mfumo dume ndio tatizo na unawaathiri wote wanaume na wanawake.

kabisaaa mkuu. jamii ijikomboe au ikombolewe kifikira japo najua tuna safari ndefu. namshukuru mleta mada kwa kuanza kujikomboa kifikira
 
Maisha ya kufikirika yatawaumizeni sana mabinti

Hakuna mahali maisha yameweza kwenda bila kuwa na mtu wa kauli ya mwisho
Ni bora ungedai wewe uwe na kauli yamwisho ungeeleweka
Lakini kudai mue sawa,haiwezekani

Hebu fikiria tu kama kuna aina hiyo ya maisha,kutakuwa na maamuzi kweli?
Wewe unakuja na kusema salary zote za mwezi huu tunakwenda kumalizia nyumba ya mama kule kijijini
Mumeo anakuja na kusema salary zote za mwaka huu tutazitumia kwaajili ya kufungua kampuni ya usafirishaji
Si vurugu tu hizo?

Au wewe unadhani mtaweza kwenda kwa style hiyo?
I doubt it!

kuna vitu huhitaji kauli ya mwisho lakini isiwe wewe tu ndo wa kutoa kauli ya mwisho. kuna wakati mwenzio akawa na mawazo ya kujenga zaidi kuliko yako lakini kwa sababu ya kuwa na "kauli ya mwisho" mkaangamia. mume au mke anaweza kutoa kauli ya mwisho kuwa watoto wa kike wasiende shule..... kiwanja kisinunuliwe mwaka huu......lazima tuzae watoto watano.... n.k bila sababu za kuridhisha kwa kila kauli. hali hii haikubaliki ktk jamii

kwa nini kusiwe na majadiliano? kuna wanaume wengine hawana busara na hekima. wakiwa na kauli za mwisho itakuwaje?
kuna wanawake wengine busara na hekima zao zinawatosha wenyewe. nao wakiwa na kauli za mwisho tutafika?
 
usiumize kichwa kujiuliza itakuaje, sina mpango wa kuwa 'slave'.

You are already a slave! Waiting to be approached to get laid is another form of slavery!

Ruka mkojo, kanyaga mavi.. unknowingly! Ujana mzuri sana since you have options, hence choices to make! But time flies, najua utatudi humu siku moja na malalamiko!
 
Were you the one who sold me?
Or you are a slave master?
Dont be ......
Back off...
Gud mng.
 
kuna vitu huhitaji kauli ya mwisho lakini isiwe wewe tu ndo wa kutoa kauli ya mwisho. kuna wakati mwenzio akawa na mawazo ya kujenga zaidi kuliko yako lakini kwa sababu ya kuwa na "kauli ya mwisho" mkaangamia. mume au mke anaweza kutoa kauli ya mwisho kuwa watoto wa kike wasiende shule..... kiwanja kisinunuliwe mwaka huu......lazima tuzae watoto watano.... n.k bila sababu za kuridhisha kwa kila kauli. hali hii haikubaliki ktk jamii

kwa nini kusiwe na majadiliano? kuna wanaume wengine hawana busara na hekima. wakiwa na kauli za mwisho itakuwaje?
kuna wanawake wengine busara na hekima zao zinawatosha wenyewe. nao wakiwa na kauli za mwisho tutafika?

Absolutely right!!!! Nimeipenda sana hii!!
 
Back
Top Bottom