LILENDI
JF-Expert Member
- Oct 27, 2013
- 1,400
- 496
Ongelea upande wa pili wa majukumu ya mume (in the same african marriage) ili usiwe biased. Chakula kinapokosekana nyumbani, ada ya shule wa watoto ikikosekana, makazi bora etc ni nani anawajibika? au wanawake hayo hawayaoni?
hahahahaaa! hata unachokiandika ni matokeo ya mfumo dume wenye mizizi mirefu sana. kwa sababu hujengwa toka tukiwa watoto, wala hatuoni kuwa ni tatizo. we take it for granted.
ndo maana hata wanawake wenye kipato kikubwa kuliko waume zao, bado hudai matumizi na mahitaji yao binafsi kutoka kwa waume zao wakiamini kuwa wao(wanawake) ni watu wa kutunzwa. pia wanaume wengine huamua kuwachisha kazi wake zao kwa sababu wao(waume) wana "wajibu" wa kuitunza familia. mwanaume amefanywa aone kwamba ana wajbu wa kuhakikisha familia yake inapata mahitaji yote ikiwa ni pamoja na uliyoyataja. kwa upande mwingine, mwanamke amefanywa ajione ni wa kutunzwa, kudekezwa, n.k hivyo, mume akishindwa kutimiza majukumu ya " kichwa cha nyumba," yafuatayo yanamhusu:
1. mkwewe atamwita mwanaume suruali, hivyo dharau kwa kwenda mbele kutoka kwa mkewe, ndugu wa mke na hata watoto wake na majirani
2. hata mwanaume mwenyewe hawezi kujisikia vizuri kwani anaona "kashindwa" kutimiza wajibu wake. hali hii hutokea hata kama mke ana hela, anaprovide for the whole family na wala hamnyanyasi mume wake.
sikwenda upande huu kwa sababu ningekuwa out of the topic mkuu