Kuolewa

l used the word kuolewa ambalo linatumika kwetu tu (kiafrika)
Sihitaj kugeza mambo ya kizungu, ila nataka kujua heshima ya mwanamke kwa maana ya 'kuolewa'.
Kama hakuna tofauti na utumwa then its humiliation, can't you see that Sir?


Mimi huwa nasema 'mapenzi ' ni utumwa wa hiari
as long as unampenda mtu,tayari uko kwenye utumwa wa aina fulani
uwe mume au mke,
sasa wewe unaweza tu kuwa uko sensitive au umeolewa na usiempenda
mwanamke akianza kuhoji hoji kwa nini mwanaume anamwambia fanya hivi na fanya vile
mostly inakuwa hampendi yule mwanaume,aliolewa ili aolewe
wenzio walio in love na wanaume wao...wanarudi home wamechoka na still wanapika
na mume sometimes hata hiko chakula hajatoa pesa...na ukiwaambia waombe talaka wanakuchukia ...
 
Kuolewa kuna maana gani?
Mwanaume anaposema 'siwez kupika (mfano) kwani mi ndo nimeolewa?'
Does it mean kuolewa haina tofauti na kua mtumwa wa mwanaume?
Does it mean wanaume wanaoongea hayo hawajui maana ya kuoa?
What does kuolewa mean?

Nakuozesha vile alivyoamrisha m/mungu. Nayo ni kuishi kwa wema. Na ikitokea kuachana bas muachane kwa wema. Maneno hayo kila muislam lazima ambiwe wakat anaozeshwa. Ktk qur aan tunaambiwa. Wao me ni vivaz kwenu ke nyinyi na nyinyi ni vivaz kwao wao me. Asie na mke na anauwezo ni kama anatembea uchi. Kazi ya Mwanamke pindi anapoolewa c kupika Wala kuosha vyombo hivyo anafanya kwa hiari yake tu. Na huruma alizowaumba nazo mungu. Kazi yake yeye ni moja tu kukuzalia watoto hiyo haina option kwao kwamba mume safari hii zamu yako kuzaaa ! Vile vile mke ni pambo muda pambo linatakiwa kuwa ktk hali nzur.
 
Kuolewa si lazima/ ila inaongeza heshma/ina hadhi yake/haijalishi we ni mke wa kigogo au mkulima_mwanafa.
Wengine wanaolewa ili wapate tu respect kuwa yeye sio nungayembe!!
hapo kwenye red ndo sisi ambao hatujaolewa , halo ya nyau
 
hapa ndipo ninashindwa kuelewa kwanini niwe chini ya himaya yake???ni kwanini sote tusiwe chini ya kila mwenza?kwamba yeye yuko juu nad mwenye final says???

Hata maandiko yanasema Mungu alimuumba mwanamke kuwa msaidizi wa mwanaume.....

Na ndo hvyo mwanamke anakuwa chini ya mwanaume......ukitaka kuwa juu ndo hvyo mtaishi kwa mafarakano....
 
ni mtazamo wangu tu jamani.....kiafrika, kuolewa ni sawa na kuikana nafsi yako na kuwa chini ya "kichwa cha nyumba". mfumo dume uko hata miongoni mwa wanawake wengi tu. baadhi ya wanawake hawapendi kuwaona waume zao wakifanya "kazi za wanawake" including cooking, washing, etc. na ikionekana mume anafanya hayo kwa ridhaa yake, watu husema kapigwa kipapai/limbwata.

mfumo dume is deep rooted and it can't be easily uprooted.

omba Mungu akuongoze upate mume aliyekombolewa ,kifikira ili asikufanye mtumwa wake.
Ongelea upande wa pili wa majukumu ya mume (in the same african marriage) ili usiwe biased. Chakula kinapokosekana nyumbani, ada ya shule wa watoto ikikosekana, makazi bora etc ni nani anawajibika? au wanawake hayo hawayaoni?
 
Mimi nadhani hii ya kupika, kudeki n.k. ni kazi za wamama (kiafrika) kwa sababu toka wakiwa wadogo mama zetu wanaweka msisitizo kwenye kufundisha dada zetu kujifunza kazi hizo.
 
Kuolewa kuna maana gani?
Mwanaume anaposema 'siwez kupika (mfano) kwani mi ndo nimeolewa?'
Does it mean kuolewa haina tofauti na kua mtumwa wa mwanaume?
Does it mean wanaume wanaoongea hayo hawajui maana ya kuoa?
What does kuolewa mean?

Hapo kwenye red; ina maana mwanaume akikuoa yeye hawi mtumwa kwako? Mi nadhani kila mtu anakuwa mtumwa wa mwenzake ila hujajushughulisha kufikiri ni kwa jinsi gani mwanaume naye anawajibika kwenye ndoa kwa nafasi yake kama mume. Ukiainisha majukumu ya mume na mke utakuta kila mtu ni mtumwa wa mwenzake ila kwa namna tofauti. Kama umelelewa kwenye familia ya wazazi wawili kumbuka majukumu gani Baba yako alikuwa anastruggle nayo na hata Mama yako alikuwa anasema ngoja tumwambie baba yako.
 
All in all jamani africa ibaki kua ni africa tuu tusiige ya wazungu ...kwa mila za kiafrica mwanaume kukaa jikoni mkewe yupo tu kakaa sidhani kama itatokea hii na ikainekana ni good thing so mwanamke kama mzima hauna kazi nyingine yakufanya kwa nini usipike tu....maisha ya kwenye tamthilia za kifilipino kamwe usiyalete kwenye tamaduni zetu za kiafrika.....full stop.
 
Mwanamme anaoa ,
Mwanamke anaolewa
Kuoana ni jinsia moja mfano ,guys merriage,au lesbian merriage
 
All in all jamani africa ibaki kua ni africa tuu tusiige ya wazungu ...kwa mila za kiafrica mwanaume kukaa jikoni mkewe yupo tu kakaa sidhani kama itatokea hii na ikainekana ni good thing so mwanamke kama mzima hauna kazi nyingine yakufanya kwa nini usipike tu....maisha ya kwenye tamthilia za kifilipino kamwe usiyalete kwenye tamaduni zetu za kiafrika.....full stop.

The issue ni maana ya kuolews tu, maswala ya kupika huo ni mfano tu nimetoa bt si maswala ya kuleta tamthiliya za kifilipino.
 
Mimi nadhani hii ya kupika, kudeki n.k. ni kazi za wamama (kiafrika) kwa sababu toka wakiwa wadogo mama zetu wanaweka msisitizo kwenye kufundisha dada zetu kujifunza kazi hizo.

Tatizo haliko kwenye kufanya kaz za ndani my dear. Swali lipo kwenye statement hii "Nifanye hivo kwani mi nimeoa ama nimeolewa"
hapo ndipo pananifanya nitafute maana ya kuolewa.
 
utumwa ni mfumo wa maisha unaongozwa na amri na maagizo toka kwa bwana kwenda kwa mtwana lakin kuoa ama kuolewa ni mfumo wa maisha ya ndoa unaoongozwa na hisia za mapenzi na maridhiano baina ya wawili,wawili hao wanakua wameamua kwa ridhaa yao kuisha kama mme na mke na kushirikiana na kuvumiliana kwa hali na mali katika shida na raha.Kumbuka utumwani hakuna hiari na upendo bali ndoani kuna upendo,hiari na makubaliano iwe katika mapishi,usafi,ujenzi na mengineyo.
 
Back
Top Bottom