brenda18
JF-Expert Member
- Sep 17, 2013
- 5,687
- 5,297
- Thread starter
- #101
Nimecheka kama mazuri. 75% yalishawahi kunihusu ndo maana sitakaa nimzodoe mtu anayekaa kwenye mahusiano tasa miaka 2, 3, 5, 10 20.... Akae tu maana akija kufanikiwa kutoka atakuwa amekua sana na akitoa ushauri lazima ueleweke maana ni "first hand information". Ukiona mtu yuko kwenye uhusiano mgumu ukamhubiria mpaka akatoka ujue mchango wako ni mdogo sana - alikuwa ameshafikia kiwango kikubwa cha uelewa na kilichomtoa ni utashi wake. Ukiona mmemwambia lakini hasikii basi ujue dozi ya mateso haijatosha kumfanya afunguke na kuvuka kiwango cha ujinga alio nao ndo maana ana excuse kwa kila kituko anachofanyiwa.
Mlioko kwenye mahusiano sugu si kwamba hamjaambiwa. Mmeshaambiwa sana tena wengine kwa upofu wenu mnawasaliti watu wanaojaribu kuwafungua macho. Unaskia "baby eti rafiki yako fulani ameniambia wewe ni malaya sana, huna fyucha na mimi...unanichuna tu..."!! Ukija kufunguka macho na kuona kila kitu kama kilivyo ndo unaanza kuwakumbuka mitume na manabii wote uliowafukuza na kuwasaliti. Ndo maisha. Unafanya mtihani, unafeli, unasapu, unafeli au unafaulu..ukikata tamaa unadisko halafu unaanza kusema "wanawake/wanaume wabaya!!!" kumbe we ndo tatizo. Kwenye maisha huwezi kuchagua maswali ila unaweza kuchagua kufaulu au kufeli. Nshaanza lekcha sikumbuki hata pointi ilikuwa nini.
Hahahaa,kumbe na we ni muhanga...ndio maisha
Wanawake walio kwenye mahusiano sugu mara nyingi ni wavumilivu sana,so I bet your hubby is lucky
Sisi wengine uvumilivu zero,uhusiano sugu usio na kichwa na mateso ni mengi hatuwezi kwakweli ni kipaji..