RRONDO
Platinum Member
- Jan 3, 2010
- 57,858
- 129,804
sijui maisha ya brenda na atoto lakini asikudanganye mtu kwamba ukiwa unajiweka mjini mwenyewe utaondoka kwenye uhusiano mgumu kirahisi. Watu wananaswa kwenye mahusiano magumu kwa sababu nyingi hasa za kisaikolojia. Unajikuta unamlewa mtu kaa teja kwa sababu labda za majeraha ya utotoni ambayo hata huyajui, au kwa sababu ya mahusiano mabaya ya wazazi, au kwa sababu umewahi kuwa kwenye uhusiano mbovu zaidi kwa hiyo unauona huo wa afadhali (yaani umezoea shida), au uko kwenye malipizi (karma) - huku kwenye dini yetu wanasema kupatilizwa maovu yako mwenyewe au ya wazazi n.k. Wengine wanajiona wa thamani ndogo (low self esteem) kwa hiyo wanaona sawa kufanyiwa ubaya, tena wanajiona wenye bahati kuwa na wenza husika; wengine hawana malengo kwa hiyo hawaoni shida kukaa kwenye uhusiano miaka hata 10 - wanaendeshwa na matukio tu; wengine wengi wana picha mbaya kuhusu mahusiano - wameshaamini hakuna mahusiano matamu hata akiona couple imeshikana mikono anaamini inaigiza tu ila maisha yao ya ndani ni kama yake n.k.
Nimecheka kama mazuri. 75% yalishawahi kunihusu ndo maana sitakaa nimzodoe mtu anayekaa kwenye mahusiano tasa miaka 2, 3, 5, 10 20.... Akae tu maana akija kufanikiwa kutoka atakuwa amekua sana na akitoa ushauri lazima ueleweke maana ni "first hand information". Ukiona mtu yuko kwenye uhusiano mgumu ukamhubiria mpaka akatoka ujue mchango wako ni mdogo sana - alikuwa ameshafikia kiwango kikubwa cha uelewa na kilichomtoa ni utashi wake. Ukiona mmemwambia lakini hasikii basi ujue dozi ya mateso haijatosha kumfanya afunguke na kuvuka kiwango cha ujinga alio nao ndo maana ana excuse kwa kila kituko anachofanyiwa.
Mlioko kwenye mahusiano sugu si kwamba hamjaambiwa. Mmeshaambiwa sana tena wengine kwa upofu wenu mnawasaliti watu wanaojaribu kuwafungua macho. Unaskia "baby eti rafiki yako fulani ameniambia wewe ni malaya sana, huna fyucha na mimi...unanichuna tu..."!! Ukija kufunguka macho na kuona kila kitu kama kilivyo ndo unaanza kuwakumbuka mitume na manabii wote uliowafukuza na kuwasaliti. Ndo maisha. Unafanya mtihani, unafeli, unasapu, unafeli au unafaulu..ukikata tamaa unadisko halafu unaanza kusema "wanawake/wanaume wabaya!!!" kumbe we ndo tatizo. Kwenye maisha huwezi kuchagua maswali ila unaweza kuchagua kufaulu au kufeli. Nshaanza lekcha sikumbuki hata pointi ilikuwa nini.
hata wanaume wabaki wawili duniani kuna aina za wanaume hatutakaa tuwachukue. Acha tusome namba huku huku nje kuliko kuzisomea vyumbani. Kwani maisha ni nini hata umgande mwanaume kama luba kama mwili, akili na roho havijakupa go ahead? Pamoja na wingi wetu wanawake wanawake wanaofaa kuolewa nao ni scarce kwa hiyo hata wanaume wanapata shida kupata wenza wazuri. Usifikiri mambo ya mahusiano ni magumu kwa jinsi moja na marahisi kwa jinsi moja. Kama kuoa ni rahisi wanaume wote "eligible" kwa umri na hadhi wangeshaoa.
Ukiona mume anaibiwa (sijui ni baiskeli??) basi ujue hakujiandaa kwa ndoa na si sababu ya competition. Hao waume waliotulia unataka kusema wana wake wakamilifu au competition hawaioni au hawana viwango vinavyotosheleza mahitaji ya soko hili lenye ushindani??
too smart my teacher......