mito
JF-Expert Member
- Jun 20, 2011
- 10,811
- 11,028
sijui maisha ya brenda na atoto lakini asikudanganye mtu kwamba ukiwa unajiweka mjini mwenyewe utaondoka kwenye uhusiano mgumu kirahisi. Watu wananaswa kwenye mahusiano magumu kwa sababu nyingi hasa za kisaikolojia. Unajikuta unamlewa mtu kaa teja kwa sababu labda za majeraha ya utotoni ambayo hata huyajui, au kwa sababu ya mahusiano mabaya ya wazazi, au kwa sababu umewahi kuwa kwenye uhusiano mbovu zaidi kwa hiyo unauona huo wa afadhali (yaani umezoea shida), au uko kwenye malipizi (karma) - huku kwenye dini yetu wanasema kupatilizwa maovu yako mwenyewe au ya wazazi n.k. Wengine wanajiona wa thamani ndogo (low self esteem) kwa hiyo wanaona sawa kufanyiwa ubaya, tena wanajiona wenye bahati kuwa na wenza husika; wengine hawana malengo kwa hiyo hawaoni shida kukaa kwenye uhusiano miaka hata 10 - wanaendeshwa na matukio tu; wengine wengi wana picha mbaya kuhusu mahusiano - wameshaamini hakuna mahusiano matamu hata akiona couple imeshikana mikono anaamini inaigiza tu ila maisha yao ya ndani ni kama yake n.k.
Daah aisee, haya mambo ya mahusiano ni very complicated kabisa aisee, yaani ni shida tupu. Wakati mwingine najiwaziaga ukiweza kuvumilia basi vumilia tu maisha yaende, ukishindwa kuvumilia basi sepa tu ukaanze maisha upya! manake mahusiano ni pasua kichwa akyanani