Kuoa si jambo dogo, unatakiwa uwe umejiandaa

Kuoa si jambo dogo, unatakiwa uwe umejiandaa

Mi nadhani watu wangechangiwa pesa za kuanza maisha si kunywa na kula na kuweka matambala tambala kwa ghalama tele.lol!
 
Inanikumbusha harusi ya mtoto wa mama ha....kariakoo
jamani kila mwanakamati alitoa laki 2 mfukoni plus kusambaza kadi michango
tukafanikisha kitchen party,sendooff na mdundiko,henna party,kibaokata day tukaweka(sisi wazaramo atii)
tukampa zawadi zote vitu vya ndani kuanzia kitanda zuria mpaka ufagio
kwa kweli tulijitahidi sana wanakamati na pia ilichangiwa na mama harusi alikuwa mtu wa watu (yeye kukodi kingoma kuja kukutunza siyo kazi kwake)
yaani mchoko wa shuguli hiyo ilibidi nipumzike siku 3
bint kaenda kwa mume baada ya miezi miwili kaachika
aibu kariakoo kurudi noma kaishia kwenye magheto huko migomigo
 
Mi nadhani watu wangechangiwa pesa za kuanza maisha si kunywa na kula na kuweka matambala tambala kwa ghalama tele.lol!

Karibuni kulikuwa send off fulani ya jamaa yangu, nikapangiwa kiasi cha kutoa. Nikawauliza wanakamati kwa vile sikuwako karibu huko inakofanyika send off, je bibi arusi mtarajiwa mmepangia apate kiasi gani? Wakanijibu kuwa kila aliye nacho atoe na pesa tunazohitaji ni party ya kumwaga.

Kilichofuata niliwaambia simo katika mpango huu kuchangisha mamilioni mnayokusudia kisha yaishie kwenye ulaji, unywaji, miziki na vicheko na kesho yake hawa wanaharusi wanabaki na hali mbaya ya maisha hadi wasetirike itawachukua muda.

Nilichofanya kiwango walichonipangia nikamtuma mtu siku hiyo ya send off amkabithi bibi arusi mtarajiwa iwe kwa ajili ya kuanzia maisha badala ya kumaliza palepale.

Nilieleweka vibaya, lakini niliwaambia nataka kuanza kuonyesha mfano wa nini kinatakiwa katika nafasi kama hii badala ya sherehe hizi na kuwanufaisha wenye kumbi hizi.


Yule dada alifurahi baada ya ile Send Off kwa kuniambia ni mimi pekee ambaye nilimpa kitu kikubwa cha kuanzia maisha kwani mumewe amechomolewa kila kitu kwa ajili ya harusi.

 
ngoja waliooa wathibitishe
maana yake huku mtaani mambo tofauti
mahali 50000
Msagasumu na mziki wake 80000
ukumbi nje ya nyumba --------
wakwe wanakaa mbagala nauli 600-700 na haulali pale
chakula cha 20000
kitchen party 100000
siku ya ndoa gharama ya chakula na maji ya uhai madogo 200000
kama una laki 5 chenji inabaki
 
na mwanamke mwenyewe alishapitiwa na watu kibao,na ile pete ya uchumba ulionunua laki 3 utaipeleka wapi? na hivyo sijui blanket sijui nini siviko kwenye milion 2 au? na mwisho wa yote ndoa wiki 2 mbali na zaidi ya yote mwanamke wanakugongea.kuoa kwa garama hizo bado ni asubuhi sana
 
hahaha mbavu zangu wakuoa oeni me michango ntazid i kuwachangia ila me bado sana
 
Kama ni hivi miaka 40 itagonga tu bado kwenye safari ya uchumba tu labda kama serikali litawagusa waanzishe LOAN BOARD YA NDOA ndiyo itakuwa pona yetu wengine.
 
Kama ni hivi miaka 40 itagonga tu bado kwenye safari ya uchumba tu labda kama serikali litawagusa waanzishe LOAN BOARD YA NDOA ndiyo itakuwa pona yetu wengine.
hapo mkuu, Marehem Col.Gaddafi alikuwa akiwapa wananchi wenyekuoa eqv: $20000- na gari nakuwasaidia flat ya kuishi !!!
Sasa hiyo kwishen..
 
Gharama ya arusi inategemea vitu vifuatavyo:

1. Uwezo wa bwana arusi na familia yake
2. Uwezo wa ndugu, jamaa na marafiki wa bwana arusi
3. Jinsi ya familia ya bwana arusi wanvyoshiriki arusi/shughuli za watu wengine (ndugu/marafiki/majirani nk)
4. Uwezo wa familia ya bibi arusi mtarajiwa. Je wana uwezo wa kujigharamia vitu kama nauli nk – ukweli ni gharama zao. Bwana arusi kutoa ni hisani tu.

Mambo mengine umeweka naona kama mbwembwe tu. Labda inategemea mila na desturi za watu. Kwa mfano bwana arusi umeenda kwa wakwe kujitambulisha – ni lazima? Kama haitoshi eti unawaalika tena kwako. Gharama juu yako – lazima hilo?
 
Hivi jamani, mnazijua gharama anazoingia bwana harusi hadi anapooa? Katika hali ya kawaida kabisa, kama wewe ni mwanaume na unataka kuoa, jiandae kwa mambo haya: (hizi ni gharama utakazoingia nje ya michango ya harusi)


1. Kujitambulisha ukweni. Hapo utatakiwa uende kijijini alikozaliwa mkeo mtarajiwa ukajitambulishe huko. Kama mfano mkeo anatokea Mwanza, na mnaishi Dar, andaa nauli ya watu wawili, malazi kwa siku mbili, na utagharamia shuhuli hiyo ya utambulisho. We tenga 500,000. Hapo tuna assume mkeo atajitegemea. Otherwise 800,000 itakutoka.

2. Kumtambulisha mkeo kwenu. Kama nyie nyumbani ni Arusha, utatakiwa umpeleke huko Ngarenanyuki. Sio umlete hapo Tabata mlipopanga. Hapo sio kwenu! Andaa nauli yako na atakaekusindikiza, nauli ya binti na mwenzie, na gharama za vinywaji na chakula siku hiyo. Utahitaji kama 700,000

3. Kifuatacho ITV ni kuwaalika wakwe zako nyumbani. Uwatoe watu kama nane Mwanza, uwalete Arusha. Wale, walale, wajisaidie, kwa gharama zako. We acha ubishi, tenga 800,000 tu.

4. Kwani we wazazi wako wanajua unakooa? Sasa je? Wasafirishe kwenda Mwanza! Watu watano. Utahitaji kuwa na 500,000. Beba pia ATM card yako, kuna imejensi.

5. MAHARI ndio topic inayofuata sasa. Ukiwa mjanja, unganishia kwenye hiyo safari hapo juu uue ndege wawili. Pamoja na hayo, itabidi ubebe 2,000,000.

6. Sasa kijana unaweza kumvisha mchumba wako pete. Nunua ya kawaida kabisa ya dhahabu. 350,000. Tukio lenyewe la kumvisha pete unaweza ita marafiki wawili watatu ukatumia 200,000. Au fanya sherehe kabisa. Mi simo

7. Oke, sasa unaweza kuitisha vikao vya harusi. Tengeneza kadi za mwaliko wa kamati kwa 200,000, kikao cha kwanza gharama zote ni juu yako. Andaa 500,000. Swali la kwanza kwenye kikao: “We una shing ngapi?” Sema 1,000,000.

8. Utahitaji 100,000 ya sms na simu kukumbushia michango. (Shukuru Mungu kuna cheka time)

9. Wakati vikao vinaendelea, utatuma 200,000 kwa m-pesa ili mambo ya kimila yaendelee kule nyumbani. We unaelewa

10. “Darling, sasa mi kwenye kitchen party ntavaa nini?” 300,000!

11. “Darling, kuna mahali nimeona gauni zuri la send…” 400,000!

12. “Baby, rafiki yangu alinunua gauni la harusi China yani lilimpende…..” 700,000!

13. Wakati huo wewe mwenyewe hujajua utavaa nini, hujanunua pete za harusi, hujamvalisha best man na mkewe. Tuseme unahitaji kama 1,500,000 maana utalia lia sana. Kumbuka, gharama hizi huchangiwi na kamati. Wala hutarudishiwa.

14. Siku ya send off lazma uende Mwanza. Utaenda mwenyewe? Ndugu wawili watatu na mshenga 600,000. Kwenye send off utatakiwa kutoa sijui blanketi la bibi, vitenge vya mashangazi, na vikorokoro kibao. Nunua hivyo vitu 300,000 uende navyo ili kupunguza gharama. Beba 200,000 za wale mashangazi watakaoibuka ghafla!

15. Mshonee baba mkwe suti 100,000 mama mkwe yeye atavaa gauni la 50,000.

16. Fotokopi hiyo hapo juu (namba 15) kwa wazazi wako. 150,000

17. Watu watakaopenda kuvaa sare wajitegemee! Mimi sina hela! Ila utavishonea nguo vile vitoto kwa 80,000.

18. Siku mbili kabla ya harusi, utaanza kupokea wageni. Unatakiwa uwatafutie malazi na chakula. Kwa ujumla utahitaji kama 500,000

19. Jioni watoe auti mashemeji zako ambao hawajawahi kufika Dar ukawanunulie bia ili wakuone wa maana. 200,000

20. Siku ya harusi bibi harusi na mwenzie na watoto na ma maids watatakiwa wakapambwe saluni. 200,000

21. We na mwenzio mtaenda kunyoa hapo kwa nanii. Ndevu na nywele 10,000

22. Siku ya harusi beba sadaka 10,000. Wakati huo umeshamtuma kijana akakulipie hoteli mtakayofikia baada ya harusi. Kamati haitoi hela hiyo, so utalipa malazi ya siku mbili200,000

23. Kama mtaenda honeymoon sehemu yoyote nzuri nzuri nje ya mji, si chini ya 800,000 kwa angalau siku 5.

24. Wakati uko huko honeymoon, huna hata kumi, mwanakamati mmoja ambae hakuchanga anakupigia simu “ Sasa tunavunja lini kamati?” Pesa yote iliyochangwa ilitumika kwenye harusi, sasa gharama za kuvunja kamati ni za nani?? 500,000!

25. SASA MNAANZA MAISHA YA UNYUMBA. TSHS. 14,150,000/= poorer.

Na hapo makadirio yote nimeweka ya chini.
Muongo wewe,nimeoa last two weeks attendants 120,pamoja navyoote nimetumia MIL.5.5 tuuuuuu na ni harusi nzuri saaaaana,thankx God nina nyumba nzuri na gari ya kutembelea na ni mwl.Sema nilijipanga na kukima ufuta saana singida na Vitunguu Moshi.
Acha kuwatisha watu wewe,Shetani wa Kukatisha tamaaa potelea mbali
 
huku kwetu uswahilini kuna jamaa alioa kwa laki na 20 tu
mkesha aliwalisha watu ugali maharage kesho siku ya tukio wakala pilau nyama na maisha yao mazuri mpaka leo
ila hapo kwenye kikao eti useme una milion1 iyo shereh yako itagota milion4 au 5 hapo ni sawa na kuruka mkojo kukanyaga mavi....bora useme una milion4 ukiongezea na 4 za mchango 8 hapo utafanya shereh ya uhakika na hakuna lawama kwa watakaokuja
 
Mwenye haki wa Mungu ataishi kwa imani. Pia Mungu asipoulinda mji wao walindao wakesha bure. Mtaogopa sana huku wengine wakiweka vitu ndani na maisha yanakwendaaa.
 
ngoja waliooa wathibitishe
maana yake huku mtaani mambo tofauti
mahali 50000
Msagasumu na mziki wake 80000
ukumbi nje ya nyumba --------
wakwe wanakaa mbagala nauli 600-700 na haulali pale
chakula cha 20000
kitchen party 100000
siku ya ndoa gharama ya chakula na maji ya uhai madogo 200000
kama una laki 5 chenji inabaki

Mkuu umesema maisha halisi sio huyu jamaa aliyepost kwa ku assume watu wengi wako hivyo, kwa watanzania tulio wengi kuoa ni rahisi sana, ila tatizo ni jinsi ya kuendesha maisha wakati utapokua na huyo mkeo mara amejifungua, mara mtoto anaumwa, hapo ndo pagumu tena usipokua makini na maisha ya hapa mjini hata sembe na dagaa mchele utashindwa kuwamudu.
 
Gharama ya arusi inategemea vitu vifuatavyo:

1. Uwezo wa bwana arusi na familia yake
2. Uwezo wa ndugu, jamaa na marafiki wa bwana arusi
3. Jinsi ya familia ya bwana arusi wanvyoshiriki arusi/shughuli za watu wengine (ndugu/marafiki/majirani nk)
4. Uwezo wa familia ya bibi arusi mtarajiwa. Je wana uwezo wa kujigharamia vitu kama nauli nk – ukweli ni gharama zao. Bwana arusi kutoa ni hisani tu.

Mambo mengine umeweka naona kama mbwembwe tu. Labda inategemea mila na desturi za watu. Kwa mfano bwana arusi umeenda kwa wakwe kujitambulisha – ni lazima? Kama haitoshi eti unawaalika tena kwako. Gharama juu yako – lazima hilo?

Well said
 
Back
Top Bottom