Kunusuru Tanzania yetu na kizazi dhaifu naomba wabunge wapitishe sheria zifuatazo

winnerian

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
335
530
1. Matumizi ya pombe kwa vijana walio na umri chini ya miaka 25! Hali ni mbaya sana vijijijini na mijini. Vijana wameharibika sana na nguvu kazi ya taifa inapungua kwa kasi. Najua pombe ni sehemu serikali ilipojiegemeza kwenye ukasanyaji wa mapato lakini pia kwa kupitia hii pombe serikali inapoteza uzalishaji mkubwa sana kwakua na taifa lenye vijana wenye hari na kasi ndogo sana kwenye maendeleo.

2. Uzalishajia holela wa pombe upigwe marufuku. Kila kona kwasasa kuna uzalishaji usiofuata vigezo na mashariti ya viwango vya afya. Visa vya kansa vitakuwa vingi sana miaka ya karibuni. Sheria zitungwe na zisimamiwe kikamilifu.

3. Anasa zimekuwa kawaida sana kwasasa. Vitoto vya shule vinaendekeza maadili ya hovyo na hakuna usimamizi thabiti katika hili. Bunge pitisha sheria kali juu ya hili. Watoto na vijana wabaki kwenye mstari na hapo tutapata viongozi na watendaji kazi imara.

4. Mazingira yetu yameharibiwa kwa uharibifu wa hali ya juu. Miti imefyekwa kama nyasi, mawe, mchanga na udongo vimechimbwa kila mahali ni maandaki utadhani ipo siku tutahamia sehemu nyingine baada kufanya uharibu wa kutosha. Bunge pitisha sheria kali na zisimamiwe juu ya suala la mazingira.

5. Elimu yetu ifanyiwe marekebisho kila baada ya mwaka mmoja na kuwepo na kitengo maalumu cha kumonitoa na kufanya maboresho kuhusu elimu yetu.

6. La mwisho katiba mpya ipatikane mapema. CCM, CHADEMA, TLP, NCCR n.k. hivi ni vikundi vya kupita tu ila TANZANIA itabaki milele. Tuache uchama tuitangulize Tanzania kwanza tuokoe vizazi vijavyo.
 
Back
Top Bottom