Kununua hisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kununua hisa

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mallaba, Feb 22, 2011.

 1. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Salaam wana JF,
  Napenda kuuliza hili sawali ambalo linaweza kuwa dogo sana kwa wengine lakini naamini ni kubwa sana kwangu kwa sababu sina utaalamu na mambo ya hisa.
  Nataka kuuliza je unaponunua hisa mfano kutoka kampuni lolote..je una kuwa unapata faida kivipi?
  Sina uelewa wowote wa kumiliki hisa zaidi ya kujua ya kwamba unakuwa mmiliki wa kampuni kupitia hisa,sielewi nitafaidika vp katika hilo
  Mnaweza kunisaidia hata kama kuna taarifa zingiine kuhusiana na hisa wana JF
  Shukrani
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  nina shares TBL na hivyo basi kila mahesabu ya faida yakishakokotolewa katika mwaka (quarterly or so) basi gawiwo hutolewa kwa kila mwanahisa ...TBL hutuma by postal delivery cheques zenye gawiwo kutokana na idadi yako ya hisa na kwenda kuzicash CRDB bank...pia kuwa mwana hisa haina maana wewe ndiyo mmiliki wa kampuni
   
 3. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  lat UMEMJIBU VIZURI KABISA
   
 4. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  ahsante mkuu,
  je unaweza kutoa amelezo kidogo maana naona umesema tu kuwa un hisa TBL na huwa unapata cash yako.
  napenda kujua zaidi kuhusu huli swala la hisa
  sio siri niko kapa na hili
   
 5. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  hizo share unazinuua aje?
  je kuna kiwango cha kununua hizo share?
   
 6. L

  LAT JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0

  mkuu mallaba ... nilinunua hizi share wakati wa mwanzo kabisa TBL walipoweka public soko la baadhi ya share zao through various media and it was in 1998... hisa hizi zilijulikana kama ordinary shares ..... lakini sasa hivi ....soko la shares lipo Dar es salaam Sock Exchange kwani huko ndipo shares za makampuni mbali mbali zinapotangazwa kuwa zinauzwa na ndipo thamani ya shares/vipande inapojulikana kutokana na uchumi au umahiri wa biashara husika ya kampuni ... hii ina maana kama kampuni inajiendesha kwa faida zaidi hapo ndipo thamani ya vipande/shares inapopanda .... mimi sio mtaalam wa hili somo la shares na stock market lakini ni uelewa wangu kwa vile na mimi ni mdau kwakuwa nina shares zangu TBL ....ninachoweza kusema ni kwamba nikiamua ninaweza peleka shares zangu DSE na wakazipiga udalali na kuziuza .... kama thamani ya shares zangu ilikua TSH X basi nikipeleka DSE watauza kwa bei ya shares iliyopo sokoni yaani Y ambapo Y = X+faida na mtu yeyote anaweza akaenda kununua share hizo katika soko la hisa
   
 7. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2011
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,122
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Kuna njia mbili za kupata faida na hisa.

  Kampuni inaweza ikaamua kutoa part of its profits kama dividends so ndo inakuwa kama LAT anavyosema unapata kiasi fulani kutokana na idadi ya hisa ulizo nazo, MUHIMU: NI UAMUZI WA KAMPUNI KAMA ITATOA DIVIDENDS SIO LAZIMA HATA IKIPATA RECORD PROFITS!

  Njia ya pili ni kusubiri hadi hisa zipande thamani zenu kuziuza so ile tofauti kati ya purchase na sale price ndo itakuwa faida yako. AGAIN: HAKUNA GUARANTEE KAMA HISA ZITAPANDA THAMANI, ZINAWEZA ZIKASHUKA AU KUBAKI PALE PALE.
   
 8. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Thanks LAT for more ellaborations.
   
 9. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  thanx buddy too:usa2:
   
 10. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #10
  Feb 22, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Kununua hisa zenyewe (Secondary market), iwe za TBL au za kampuni nyingine ye yote, unaenda kwa mawakala, ambao ndio wanakwenda soko la hisa kwa niaba yako). Moja wa mawakala wazuri (kwa uzoefu wangu binafsi) ni Orbit Secutities ambao wako Twiga House ghorofa ya 3 (Barabara ya Samora).

  Hawa pia wanakupa ushauri na maelezo mazuri ya hayo mambo ya hisa. Kutokana na uzoefu wangu wa kutoka 1998 hisa ambazo zinatoa magawio mazuri mara kwa mara ni pamoja na TBL, TCC, Tanga Cement. Baadhi ya zinazofanya vibaya (kutokutoa magawio ni pamoja na TOL na NICOL.
   
 11. Mtanganyika

  Mtanganyika JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2011
  Joined: Jul 18, 2007
  Messages: 1,613
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 180
  Mkuu,

  Nadhani waliojadili hapo juu wengine wapo sawa wengine wamechanganya habari. Hisa maana yake ni kununua umiliki katika kampuni kwa kiasi fulani. Maana nyingine unakuwa mmoja wa wamiliki, kutokana na ukubwa wako wa share. Kama kampuni ina share 100, na wewe unamiliki 10 maana yake wewe una own 10% ya ile kampuni. Faida ni kwamba wewe unahusika katika maamuzi ya kuchagua mkurugenzi mkuu, na mambo mengine kutegemeana na sheria na kanuni za share yako. Vile vile kumbuka ya kwamba kama kampuni inapata hasara na wewe unapata usara, lakini share zako zinabaki vile vile quantity, ila bei yake nitazungumzia badae.

  Kampuni inapokwenda kujiandikisha ikapewa certificate of incorporated, inaruhusiwa kuhuza share kadhaa. Let say TBL wameruhusiwa kuuza share 100,000 (huu ni mfano). Maana ya kwamba TBL maximum number of shares wanazo weza kuuza ni 100,000 wakitaka zaidi inabidi warudi kwa serikali and other procidure zifanyike (beyond the scope of this explaination). Sasa TBL wakisha kubaliwa kwamba wao wata issue 100,000, then wao wanakaa chini na kuamua labda wanauza only 50,000 kwa sasa. Na hamsini watauza badae..... So, TBL wataweka bei share ambao wao wanaamini ni fair kutokana na asset, earnings na mambo mengine. Kisha wanauza kwa primary buyers, then hawa primary buyers ndio wanakuja kuuza kwa sekondary buyers kama mimi na wewe pale DSE.

  Mmiliki wa share anapata faida kwa njia mbili, kwanza kwa kupanda kwa share yake sababu ya demand and supply forces. Maana chukulia wewe umechukua shares 100 za TBL kwa shili 50 kwa shares mwaka 1998, mwaka 2000 demand ya shares za TBL imekwenda juu na soko lime determine price ni 70 TSh, wewe ukaamua kuuza nusu ya share zako 50 maana ni kwamba umepata faida ya shilingi ishirini kwa share. Kitaalamu tunaita Capital Gain.

  Njia ya pili ni pale kampuni inapopata faida, CEO na uongozi wa kampuni unaweza kuamua kwamba kiasi fulani cha faida zinagawiwa. na hapa ndio wengine wamepazungumzia, hii ni dividend payout. Maana ule mfano wetu wa TBL kama wana share 50,000 kwenye market (outstanding), na wanataka kugawa dividend kiasi cha shillingi 50,000 then kila share itapata 1 shilling (50,000/50,000) dividend. Sasa wewe kama una share 100, utapata shilling 100. Hii ni mara moja kwa mwaka, na ugawiwa only kampuni ikiwa imetengeneza faida na baada ya kulipa TAX.

  Nimezungumzia faida tuu, lakini kumbuka hasara ni pamoja na share kuanguka vibaya kwenye soko. Maana less demand with high supply. Nadhani mfano kama Tanzania Oxygen walivyo issue share zao mwanzoni kabisa.

  Soko la share la Tanzania bado linasafari ndefu sana.... Nimeshawai kuandika huko zamani kwenye gazeti mmoja la biashara hapo nchini kuhusu share. Nitaitafuta ile article na kuiweka hapa.
   
 12. serio

  serio JF-Expert Member

  #12
  Dec 11, 2013
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 5,927
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Very important information
   
Loading...