HYIP Investment Platforms ni nini na kwanini unapaswa uziepuka

Kainetics

Senior Member
Jun 20, 2022
131
259
Kainetics - Platform za Uwekezaji, Utapeli na Pesa.jpg


Habari wana JamiiForums. Leo nimeona sio mbaya nikjaribu kuongelea swala la hizi investment platforms ambazo zina claim kuwa unaweza zitumia kujiingizia pesa mtandaoni kwa kuwekeza nazo.

Kwenye pita pita zako online lazima utakuwa ushawahi kutana na link ya watu wanakushawishi kwenye platform fulani fulani ambako unaeka hela na kupata faida baada ya muda fulani au pale utakapoalika watu wengine na wao kuweka hela. Zimevuma nyingi, Idea Debator, SME sijui RichNet, na kadhalika. Wengi wamezijaribu, baadhi wamepata hizo faida na wengi wamelizwa.

Platform hizo nlizotaja na nyingine nyingi ambazo zina endelea kuexist hutambulika kama HYIP Investment platforms, na hata wengi ambao wamekuwa wakizitumia wamekuwa hawafahamu hizi Platforms zinaitwaje, zinafanyeje kazi na kwanini karibia 99.9% ya Platform hizi ni za kitapeli. Jambo ambalo naenda elezea kwa kina.

Utangulizi
HYIP - Ni kifupisho cha neno la kingereza, "High Yields Investment Platforms" ambalo hutumika kubainisha tovuti, application na mifumo yote ya uwekezaji isiyo rasmi inayotumiwa na watu mbali mbali kujaribu bahati yao ya kuwekeza hela yao na kupata faida kwa njia zaidi ya moja.

Sana sana au kwa wingi, mifumo hizi hu uperate kwa namna tatu kuu;

✍️ Binary MLM
✍️ UniMatrix MLM
✍️ Matrix MLM

Kwenye hizo namna zote tatu; mtu hushawishiwa na kuaminishwa kuwa atapata faida ya asilimia fulani itakayomuwezesha kujiingizia faida ya kiasi x kila saa/siku/wiki au mwezi baada ya kuwekeza kiasi y.

Mbali na hapo, watu hupewa namna zaidi za kujiingizia pesa kama;
• Kualika watu kupitia link na kupewa kamisheni
• Kupewa point unaponunua bidhaa zao
• Bonus za kuwekeza
• Na baadhinya mifumo uhadi zawadi mtu anapoweza alika watu kufikia level fulani.

Mifumo hizi hu operate in form of levels, na hii ndio inayotofatisha kati ya Binary, Uni na Matrix. Mambo ambayo sitoingilia kwa kina maana bado ni maneno mazuri mazuri yanayopaswa ya kuchanganye ili iwe rahisi kwako kutapeliwa.

So, Mifumo Hizi Zinaingizaje Pesa Ya Kukupa?
HYIP Investment yoyote ile, zilizokuna na kupotea au hata zile zijazoz watakuambia hela yako huwekezwa kwenye miradi mbali mbali sehemu kadhaa duniani, pamoja na kwenye uuzaji na ununuaji wa hisa, crypto currency, indicies kama mafuta na dhahabu na nyingine kukwambia wanafanya bitcoin mining pia.

Wakiwa wamejipanga, na wakawa ready kutarget specific type of people haswa wamama na wadada, huleta sera kuwa wao ni kampuni maarufu ya vipldozi, skin care na dawa za kupunguza unene hivyo ukiwa member wa kampuni yao utaweza nunua hizo bidhaa husika na kwenda kuwauzia wengine ili uweze pata faida. Mifumo ya hivi hutoikuta mitandaoni peke ake. Huko nje hutambulika kama Network Marketing. Nadhani ushawahi kutana na watu wa Good Morning.

Je, Ni kweli wanafanya hizo BTC Mining? Au wananunua hisa au hayo majitu kibao wanayoweka kwa homepage? Hamna. Maana ingekuwa simple hivyo wangechukua hela zao na kuendelea jiingizia faida na kuwekeza hizo faida kuingiza faida nyingine watajirike na wewe usijue. Sasa kwanini watu wanaosema wanaingiza mamillioni ya fedha wanataka uwekeze hela yako kwao ili nawe upate faida? Jibu ni wewe ndie faida husika.

Kitu ambacho hutokea....
Anaekualika, anae kushawishi kampuni inalipa na imemsaidia hivyo nawe unapaswa ujiunge.... Hupata kile anachokuhubiria endapo weww kweli ukijiunga na kuweka hela. Maana hela yako ndipi faida anayopewa yeye hutoka. Na ili cycle iendelee. Nawe mbali na kuweka hela yako, itabidi ulete wagu wengine ambao wataweka hela yao ambayo wewe utapata asilimia kadhaa ya kile watakachotoa.

Hivyo basi, ili uweze kuendelea kupata zaidi lazima ulete watu wengi. Na siku ikifika watu waaojiunga na kutoa hela wakawa wachache kuliko wale wanaotegemea kupewa faida, ndipo mifumo hii huanguka. Kitu kinachoitwa Pyramid Scheme au Ponzi Scheme.

Kwa mfano rahisi; Ni sawa ukutane na tangazo langu linalosema nilipe Elf 50 nikuoneshe namna ya kuingiza pesa mtandaoni, then ukishanipa hela nikuelekeze kujipa jina kama Kainetics kisha kutafuta namba ya Lipa na kukuambia ukatengeneze tangazo kama langu watu wakuoe hela uwaoneshe kutengeneza hilo tangazo cycle iendelee.

Mambo Ya Kukudhihirishia Una Deal na Matapeli
✍️ Utasikia kampuni husika lilianzia marekani au sijui wapi wapi huko na wameingia nchini hivi karibuni lakini contact info pamoja na ofisi zao hazijulikani.

✍️ Watu watakupea ma screenshot ya withdrawals za malaki kukuconvince ujiunge. Kwanini?

✍️ Hela inakotoka : Karibia platform zote zina miradi mbali mbali ambayo hata hujawahi isikia. Karibia kampuni zote zinafanya BTC Mining na karibia kampuni zote zinafanya ununuzi wa hisa, na bangi bangi nyingine kibao.

✍️ Tofauti kati ya kuweka na kutoa hela; Pale unapoenda deposit hela, kila kitu hufanyika kwa wepesi ila kuwithdraw huwa na miyeyusho kibao

✍️ Zile post za wekeza x upate y. Post yoyote ya hivyo ukiiamini tayari umekubali kuliwa kirahisi. Lakini kwanini ambao huzifuata na kutapeliwa mwisho wa siku huwa wengi?

Kwanini Japo Ya Hizo Red Flags Zote Wengi Hutapeliwa?
🛍️ Wale ambao huwa targetted ni wale wenye tamaa. Ambao wanataka ingiza pesa ndani ya siku , masaa na wiki.

🛍️ Sana sana mbali na wenye tamaa, walio rahisi kutapeliwa na hizi platforms ni wale ambao wana natatizo na wako desperate kupata hela ya haraka.

🛍️ Kutotumia common sense. Ni wachache ambao ukaa na kutafakari au hata kuuliza maswali kisa kuogopa kuonekana wajinga.

🛍️ Wale wafanyao kazi za serikaliz kama waalimu au watumishi wa umma huwa victims wa hizi mambo kwa kuwa huwa referred na watu wanaowaamini au wale waliojuu ya chain of command.

🛍️ Nirudie tena, kutouliza maswali ya msingi.

🛍️ Nirudie, kutotaka fahamu hela inakotoka.

🛍️ Bila kutaka fahamu nani wako nje ya pazia na wanapateje faida.

Ko Inamaanisha HYIP Investment s zote ni za Kitapeli?
Jibu fupi ni ndio. Jibu refu ni karibja 99.9% ya platform zote ni za kitapeli. Maana hujaribu kuwaamisha watu wanaweza nunua vitu visivyo na value (kama Packages) na kugeuza hela zilizotumika kununua Packages husika kuwa faida kitu ambacho hakipo. Maana ili biashara iweze kuhesabika kuwa imefanyika, lazima iwepo exchsnge ya bidhaa na fedha au kitu chsnye thamani saawa na bidhaa husika.

Huwezi kuwa na shida ya Super glue af uamue kwenda dukani ukalipa mia tano kisha urudi home ukute viatu vimejigundisha. Kama ambavyo huwezi enda kwa mwenye duja ukampa heka na kurudi nyumban kulala bila kuchukua kitu. Lazima akupe kitu chenye thamani sawa na hela uliyompa. Ndio maana ukinuua kifuruahi cha DSTV Family kuna valu unapata ndo maana hustuki. Au ukilipa karo ya mwanao unachopata ni elimu, nk.

Sasa kwanini ununue vitu visivyokuwepo? Sijui VIP 1 au VIP 2? , afu huamini hela yako inaongezeka? Fungua macho. Hakuna mambo kama hayo.

Mbali na ya hayo yote, ukiwa na akili, hizi Platforms zinao uwezo wa kukuingizia pesa. Japo kwa asilimia kubwa ni kuoitia namna ambazo zitakufnya ujutie.

Wengi huzivamia hizi platform zikiwa bado mpya na za moto, wiki ya kwanzs hadi ya tatu. Huwekeza hela yao ya kutosha na kuwithdraw maana kwenye hii period watu wanakuwa wengi wanaoingia hivyo uhakika wa hela unakuwa mkubwa. Basda ya hapo, huanza viswahili sheria kibao na siku moja tu unaweza amka ukakuta Platform husika haipo.

Sema kwanini ufanye mambo ya wasi wasi kama hayo? Kwa ufupi wake hizo ndizo HYIP Investments, siku nyingine ukikutana na mtu anakushawishi kujiunga kupitia link yake sijui ueke 12,000 au 5,000 nk. Kwa asilimia kubwa utakutana na mambo kama hayo.

Nawasilisha.
Kainetics

🏷 Telegram Channel : Kainetics Blog 🇹🇿

🏷 Blog : Kainetics
 
umeandika kitu kizuri sana, kuna jamaa anaitwa Adam Fayed yupo sana Quora anajitangaza sana na anayo platform yake anauza package za investment kwa bei tofauti na anadai zina returns nzuri..... unamsemeaje huyu?
 
umeandika kitu kizuri sana, kuna jamaa anaitwa Adam Fayed yupo sana Quora anajitangaza sana na anayo platform yake anauza package za investment kwa bei tofauti na anadai zina returns nzuri..... unamsemeaje huyu?
Kwa bahati mbaya huyo Adam Fayed simfahamu maana Quora siitumii saana.

Ila program yeyote ile inayohusisha kuwekeza hela kwa kununua kitu(package) ambacho kina promise faida wakati chenyewe hakiko tangible. Hio ni Ponzi Scheme.

Kinachotafutisha zile platform za kitaoeli na zile zinazoonekana genuine, ni wanavyo control money supply, hierachy na transparency.

Hizo ndo features zinazofanya baadhi ya hizi Platform kulast miaka na nyingine wiki.

Japo mwisho wake huwa ule ule.
 
Kwa bahati mbaya huyo Adam Fayed simfahamu maana Quora siitumii saana.

Ila program yeyote ile inayohusisha kuwekeza hela kwa kununua kitu(package) ambacho kina promise faida wakati chenyewe hakiko tangible. Hio ni Ponzi Scheme.

Kinachotafutisha zile platform za kitaoeli na zile zinazoonekana genuine, ni wanavyo control money supply, hierachy na transparency.

Hizo ndo features zinazofanya baadhi ya hizi Platform kulast miaka na nyingine wiki.

Japo mwisho wake huwa ule ule.
Kuna mtu mmoja Marekani alikuwa anaitwa Ponzie aliwatapeli sana wamarekani miaka hiyo ya nyuma kwa scheme za kitapeli kama hizo.Alipokamatwa na vyombo vya sheria,uhalifu wake ukatungiwa jina Ponzie Scheme.
 
Back
Top Bottom