Je, HISA zako zitakuwepo hata kampuni ikifirisika?

Labile

Member
Dec 9, 2016
58
63
Habari ya muda wanajamvi? Napenda kujua kitu kimoja kuhusu HISA, inasemekana kampuni inapopata hasara basi hakuna gawio.

Swali ni kwamba je, HISA zako zitakuwepo hata kampuni ikifirisika na ili uziuze kwa bei ya hasara au ikifirisika unakosa kila kitu.

=========

1619342852831.png
Makampuni mengi yanayokuwa na mitaji mikubwa si kwamba huo mtaji wameupata wenyewe bali kuna michango midogo midogo ya watu wengine ambao wanaitwa wanahisa.Je hisa ni nini? Hisa ni kipande cha umiliki wa sehemu ya kampuni.Watu hualikwa kununua vipande hivyo katika kipindi Fulani inaweza kuwa wakati wa kuanzisha kampuni au baada ya kampuni kuanzishwa pale inapotaka kujipanua kimtaji na hasa inapo ingia katika soko la mitaji.

Vipande hivyo vinakua na thamani Fulani na unapo nunua kipande hata kimoja unakua na wewe kisheria unamiliki sehemu ya kampuni hiyo kwa kiasi cha thamani ya hisa ulizo nunua.Kwa mfano kama kipande kimoja ni sh 500 na ukanunua vipande 1000 tunasema umenunua hisa 1000 na utakua unamiliki hisa za shilingi laki tano 500 000 kwa muda huo.

Unaweza ukajiuliza je unafanikiwaje kupitia umiliki wa hisa katika kampuni? Ni swali zuri kujiuliza.Kila mwisho wa mwaka kunaitishwa mkutano mkuu wa wanahisa ambapo mambo mbalimbali hujadiliwa kuhusu kampuni husika mojawapo ya mabombo hayo ni kuhusu faida ambayo kampuni imepata na uamuzi kuhusu kuigawa au kuendelea kuiwekeza ili izae zaidi na zaidi.

Kama kampuni moja ya mipango yake ni kuendelea kuwekeza faida inayopatikana ili kampuni ikue haraka basi hapo swali la kila hisa kupewa gawio lake ndio linachukua nafasi.Kwa mfano kampuni itachua faida iliyopata baada ya kulipa madeni na kodi inayodaiwa na kugawanya kwa idadi ya hisa zilizopo na kupata faida kwa kila hisa na hapo ndipo kila mtu ataweza kujua faida aliyopata kwa kumiliki hisa katika kampuni.
Atajuaje?

Ni rahisi tu.Atachukua idadi ya hisa anazomiliki na kuzidisha kwa kiasi cha faida kwa kila hisa iliyotangazwa na kampuni anayomiliki kihisa katika mkutano mkuu wa kampuni.Cha muhimu kufahamu hapa ni kwamba kiasi cha faida inayopatikana hutegemea jinsi kampuni itakavyofanya biashara yake katika mwaka husika na siyo kwamba gawio kwa kila hisa litakua halibadiliki.Linaweza kwenda chini au kupanda kutokana na mazingira ya kibiashara na sababu nyingine kiuchumi.

Kuna faida nyingi za umiliki wa hisa kwa mmiliki na kwa kampuni yenyewe.Kwa kampuni ni kwamba inakua na uhakika wa mtaji kuendelea kubaki kwa muda mrefu kwa sababu hata mtu akiamua kuuza hisa zake nafasi itabaki pale pale maana zitanunuliwa na mtu mwingine ambayo ni faida pia kwa mmiliki pale anapoona kuwa hana huitaji wa kumiliki hizo hisa katika hiyo kampuni kwa muda huo.

Ni faida pia kwa kampuni kutoa fursa ya hisa kuliko kwenda kukopa kwenye taasisi za kifedha.ili taasisi ya kifedha ikopeshe kampuni ni lazima kampuni hiyo isiwe na madeni mengi ili uwezekono wa kulipa uwe mkubwa.Na hisa hazijumuishwi kwenye idadi ya madeni ya kampuni kama ilivyo mikopo.Hivyo basi kampuni zinazotoa hisa huwa na nafasi kubwa ya kwenda kukopa na kukuza mtaji wake.

AINA HISA NAZO NI

1. HISA za wamiliki
Hizi ni aina za hisa ambazo huwa ndio nyingi katika kampuni. Wale wanaomiliki hisa nyingi katika kampuni hisa zao huitwa hisa za wamiliki. Huitwa hisa za wamiliki kwakuwa hawa huhesabika kama ndio kampuni yenyewe na hivyo wenye hisa hizo ndio wamiliki wa kampuni. Nimesema hapo juu kuwa wanahisa hawana haki sawa, wajibu pamoja na uwajibikaji.

Wenye hisa hizi wana haki kubwa ya kimaamuzi katika shughuli zote za uendeshaji wa kampuni kwakuwa wao kila hisa moja huwa ni kura moja na kwahiyo kila kitu hupitishwa kwa kura zao. Pia wana haki ya kupata mgao mkubwa kuliko wengine. Hata hivyo wanawajibika zaidi linapotokea tatizo kwa mfano inapotokea hasara wao ndio hupoteza zaidi. Kwa jina jingine hisa za hawa huitwa HISA ZA SIMBA( LIONS SHARE). Hii ni kwasababu huko mwituni simba hupata mgao mkubwa wa nyama kati ya wanyama wote.

2. HISA za kiwanda
Hizi ni zile hisa ambazo humilikiwa na watu wengine wa kawaida katika kampuni. Mara nyingi hawa ndio huwa wengi japo kila mtu huwa na hisa kidogo kidogo. Mgao wao wa faida hutokana na asilimia ya kile mtu anachomiliki. Maamuzi yao katika kampuni huwa ni madogo ukilinganisha na wenye zile hisa za umiliki( equity shares). Hata hivyo uwajibikaji wao nao ni mdogo pia kwani hupata hasara kidogo pale kampuni inapopata hasara. Pamoja na hayo sheria imewapa kipaumbele cha kupewa mgao wa faida kabla ya kundi jingine lolote.

3. HISA za waanzilishi
Hizi ni hisa ambazo hutolewa kama zawadi kwa waanzilishi wa kampuni. Mgao wa faida wa hisa hizi huwa sio wa moja kwa moja isipokuwa hutegemea na faida inayozidi. Kawaida mgao wa faida kwa wanahisa wengine hutoka katika faida ya kawaida lakini hawa hawapewi mgao kutoka faida ya kawaida isipokuwa hupata pale faida inapozidi au kuvuka kiwango ilichotegemewa.

4. HISA za kampuni
Zote nilizotaja juu ni hisa za kampuni lakini bado jina hili hupewa hisa hizi kutokana na kuwa ni hisa maalum ambazo hutolewa kwa waajiriwa/wafanyakazi katika kampuni husika. Waajiriwa hutengewa hisa zao na mwenye uwezo huweza kuchukua hisa hizo kwa kiwango cha uwezo wake. Mwajiriwa huendelea kuwa na hisa hizo hata baada ya utumishi wake kukoma . Kwa ufupi sana niseme tu kuwa hisa sio hisa ila hisa ni una hisa za aina gani.
 
Habari ya muda wanajamvi? Napenda kujua kitu kimoja kuhusu HISA, inasemekana kampuni inapopata hasara Basi hakuna gawio, swali ni kwamba je HISA zako zitakuwepo hata kampuni ikifirisika na ili uziuze kwa bei ya hasara au ikifirisika unakosa kila kitu.
Unakosa kila kitu, na wewe utapata hasara.
 
Back
Top Bottom