Kunguru wananinyea nyea, kulikoni?

Kunguru wananinyea nyea, kulikoni?

silver_back

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2018
Posts
832
Reaction score
813
Habari zenu.

Kwa kweli sina imani na mambo yoyote ila hii kitu inanipa utata. Leo ni siku ya tatu ndani ya wiki Kunguru ananinyea nikipita kwenye barabara yenye miti na yenye nyaya juu.

Yaani Kunguru anakuwa juu mtini au katika waya juu, nikipita chini bila kujua kama juu kuna Kunguru nashangaa kaninyea.

Kulikoni?
 
acha uwoga tena ukimuona kunguru we nenda dukani agiza unachotaka sababu uba uhakika wa kuokota, hela kaka
 
Una wasiwasi na kunyewa wakati mimi alishawahi kutua kichwani tena nikiwa kwenye motion. Ukiendelea kufikiria hilo jambo mwishowe utakamata jogoo kumpelekea mganga
 
Habari zenu. Kwa kweli sina imani na mambo yoyote ila hii kitu inanipa utata. Leo ni siku ya tatu ndani ya wiki kunguru ananinyea nikipita kwenye barabara yenye miti na yenye nyaya juu. Yaani kunguru anakuwa juu mtini au ktk waya juu, nikipita chini bila kujua kama juu kuna kunguru nashangaa kaninyea.
Kulikoni?
Njoo sumbawanga nikusaidie hilo tatizo sugu
 
Habari zenu. Kwa kweli sina imani na mambo yoyote ila hii kitu inanipa utata. Leo ni siku ya tatu ndani ya wiki kunguru ananinyea nikipita kwenye barabara yenye miti na yenye nyaya juu. Yaani kunguru anakuwa juu mtini au ktk waya juu, nikipita chini bila kujua kama juu kuna kunguru nashangaa kaninyea.
Kulikoni?

Ni dalili za awali kabisa na zilizotukuka kwamba unaweza muda wowote kuanzia sasa mwili wako ukaokotwa katika Fukwe za Bahari ya Hindi kama siyo Mto Ruvu au Gari ya Toyota Landcruiser Nyeupe ikapaki mbele ya usawa wa Kichwa chako huku ' Mafundi Feki ' wakiwa wanafanya ' Matengenezo Feki ' kisha mwishowe watakubeba na Wewe kukuweka ndani ya Gari kama wanavyoziweka ' Spana ' zao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom