Kuna watu hawakustahili kufa

Kuna watu hawakustahili kufa

Sina hata maneno mengi ya kusema wote ni wake na kwake tutarejea PUMZIKA KWA AMANI BABA ANGU KIPENZI ALLAH AKUPUNGUZIE ADHABU ZA KABRI NA KABURI LAKO LIKAWE NYUMBA KATKA NYUMBA ZA PEPON NA MEMA YAKO YAKAWE TAA KATKA MATAA YA PEPON TUNAZIDI KUKUOMBEA BABA ETU KIPENZ ALLAHUMA AMIN
 
Kuna baadhi ya watu ukiishi nao hufikirii kama ipo siku atakufa, na siku akifa huamini hadi anazikwa ndo unaamini
 
Mamaang ni kila kitu kwangu,hata nikiwa na wakati mgumu kiasi gani nnapompigia simu nkasikia sauti yake ya upole na ya kubembeleza huwa najihisi amani sanaa,ni mama ambae nakosa hata jinsi ya kumuelezea, anajua kufariji , anajua nn mtt wake anataka akiwa kwenye wakati mgumu,ni mama jasiri katukuza kwa namna ya kipekee pamoja na kuwa alikuwa na shida. Ni mtu pekee ambae alinifundisha maisha ni nn na kuishi na watu ni nn,kikubwa najivunia sababu ni mama ambae ameokoa na kumpenda Mungu na siku zote anatuambiaga wanang ukipata tatizo hata liwe gumu kiasi gani mtu pekee wa kumtegemea ni Mungu muumba wa Mbingu na nchi
Nampenda sana sanaaa na nnamuombea kwa Mungu aishi miaka mingi mnoooooo.
 
Brother Mshana...una huge spirit ya fatherhood in you..i bet wanaume wengi wanayo ila ya kwako imeenda mbali kidogo. Kusoma huu ujumbe kumenikumbusha mengi..kumtegemea Mungu in all times....kuheshimu na kutambua uwepo wa watu muhimu kwenye maisha when we have them as hapa duniani wote tunapita...na kila mtu ana mapito yake binafsi...especially kwenye kuwapoteza watu wa karibu kwenye maisha..
[emoji120] [emoji120] [emoji115] [emoji817] [emoji111] [emoji817] [emoji817]
 
Aiseee Mshana Jr. Hii mada imenigusa sana.. Mungu ni mwema na mwaminifu sana, mama Yangu aliwahi sema"Mungu siogopi kufa, nakufa hawa watoto namuachia nani? Mungu baba watoto wangu uwatunze" jamani wana jf sijawahi kupata shida wala kujuta km labda mama angekuwepo ingekuwa hivi/ vile zaidi nasema angekuwepo awaone wajukuu zake, angekuwepo aone tukihitimu shahada zetu, kweli Mungu hakosei wala hapangiwi, hufanya kinachompendeza na huwasikiliza waja wake. Apumzike kwa amani, amina.
 
Kama kuna Zawadi kubwa Mungu aliyotuumba nayo ni hii nguvu kubwa ya kuweza KUSAHAU, vinginevyo maisha yangekosa mantiki kabisa hapa duniani.
Mkuu kweli kabisa.marehemu analiza sana akiwa hajahifadhiwa kwenye nyumba yake ya milele, ila Mara baada ya mazishi. Anasahaulika.
 
You know the story behind, hii mada nimeiandika kule nilikokuwa... Niliwaza mengi sana but God is good God is wondeful ametenda muujiza
Wow that's good news kwakweli,glory to God...

Asubuhi nilikusaka sijakupata,nakuja huku nakutana na huu Uzi wako dooh...
 
upload_2017-4-5_16-2-41.jpeg
 
Suala la kifo bhana, sina ujasiri wa kusema nani atangulie jamani. Mungu tu ndo afanye venye amepanga, ila angeniachia tu mdogo wangu Jane bado alikuwa kijana mdogo sana.

Nakushukuru Mungu kwa kumchukua Jane wangu, apumzike kwa amani!!
Pole sana mkuu. Nimemkubuka dadangu pendo, alikuwa Wa kwanza kununulia simu ya Nokia asha 200, from Nokia tochi 30,000 na nikaifahamu jamii forums. Pumzika pema dadangu kipenzi.
 
Huwa nasoma hizi post Za JF, nawasiliana na watu pm, wengine tunakutana mitaani, na baadhi tunasoma habari zao
Naamini kwa dhati ya moyo wangu, wengi wetu hapa na kwingineko tumewapoteza watu muhimu sana kwetu kijamii na hata kitaifa na wakati mwingine kimataifa
Tuna wengi katika jamii yetu hii wako katika hali fulani kimaisha na wanakumbuka kwamba Kama fulani angekuwa hai Leo hii nisingekuwa hivi ama nisingekuwa hapa au nisingekuwa na haya mateso
Hawa ni wazazi wetu walezi ndugu marafiki jamaa na hata watu baki.. Wanatokea katika maisha yetu na kuwa watu muhimu mno watu wa msaada sana watu wa upendo sana....halafu ghafla wanazimika na kuzima ndoto nyingi, matumaini mengi fursa nyingi na hata misaada
Mambo yanapokuwa magumu, shida zinapozidi, unapopoteza matumaini Unakumbuka na kujisemea fulani angekua hai haya yote yasingetokea
Bahati mbaya ama nzuri mipango ya Mungu si ya mwanadamu, yeye ndie ajuaye Kutoka kwetu na kuingia kwetu....kila jambo linafanyika na kutokea kwa sababu..
Mungu hawezi kamwe kuziba milango yote lazima kuna mmoja atauacha wazi... Jitahidi uuuone.....
Cha kusikitisha ni kwamba wema anawachukua wabaya anawaacha... Imagine Leo hii ungeambiwa nani angestahili kufa ama kubaki ungempendekeza nani?
Kwani tunaishi ili iweje?
 
Mwenyezi Mungu atupe uvumilivu wa kuhimili uchungu wa kifo. Naamini hakuna kitu kitamuuma mzazi kama kufiwa na mwanaye anayempenda. Kifo hakizoeleki iwe kwa rafiki,mzazi,ndugu au mtoto.
 
Kama baba akifika level za kukaa na ujauzito miezi 9, kutanua miguu na kuzaa, kulea kichanga - usiku na mchana bila kulala, kunyonyesha, na kuwa nguzo kuu kipindi chote basi naweza kumweka ligi 1 na mama. Kwa tukio 1 tu la kutafuta chakula baba siwezi mfananisha na mama hata chembe - wamama kibao ni watafutaji wazuri sana, tunawaona mitaani wanafungua vigenge, wanachoma vitumbua, wanafagia mabarabara, wanabeba hata zege.

Mama yupo kwenye ligi la kibabe la aina yake kabisa. Nihitimishe kwa kusema "usimfananishe mama na vitu vya kawaida kawaida".
Mama kubeba ujauzito,kunyonyesha yote ayo ni wajibu wa mwanamke na wanaume anayoyake ila huwezi kuyaona kama nimajukum makubwa kwasababu unayaangalia ayo majukum ya jinsia zote mbili kwa hisia.Ila jibu ni hili wakati mama aliambiwa atazaa kwa uchungu mwanaume aliambiwa atakula kwa jasho.kwaiyo wakat mwanamke yuko chumba chakujifungulia akilia kwa uchungu na mwanaume yuko duniani anajenga dunia kwa jasho.Kwaiyo watu unaowaona leo kwa wingi ni matokeo ya utungu wa mwanamke na dunia unayoiona leo nimatokeo ya jasho la mwanaume.Kwaiyo usifananishe wajibu kwa hisia.
 
Pole sana mkuu. Nimemkubuka dadangu pendo, alikuwa Wa kwanza kununulia simu ya Nokia asha 200, from Nokia tochi 30,000 na nikaifahamu jamii forums. Pumzika pema dadangu kipenzi.
Pole sana mkuu, tuamini tu wako sehemu salama kuliko hapa duniani
 
Kama ulivyosema uyo MTU wa muhimu akiondoka lazima atatokea mwingine mlango ukifunga lazima mungu anakufungulia mwingine
Mungu alifunga mlango mmoja wa muhimu kwangu lakini ukatokea mwingine sijutii kumfahamu mtu huyu hajawahi kunichoka ingawa mara kwa mara huwa na mkwaza na kutokumsikiliza lakini hanichoki namuombea mungu ampe maisha marefu yenye baraka na amani tele
 
Baba yangu aisee!!alikuwa genius sana mzee yule....akili zake zilikuwa za hali ya juu!!subira,busara,hekima na upendo kwa watu alitunukiwa..
Nilideka sana kwa baba,alikuwa tegemezi kwa Hospital nzima,mkoa na taifa kwa ujumla...

My Daddy alikuwa hero[emoji22]!nammis sana baba, Natamani asingekufa,sijaamini mpaka leo kama hayuko nasi,ni miaka 5 sasa ila bado siamini...R.I.P Daddy
 
Pole sana mkuu, tuamini tu wako sehemu salama kuliko hapa duniani
Na hili ndo tumaini pekee na nadhani ndo mantiki kuu ya kuwepo kwa dini na yote yanayofungamana nayo. Pasingekuwepo na kifo hata Mungu asingepata uungwaji mkono wa leo.
 
Back
Top Bottom