Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,176
- 48,460
Nasikia kuna watu wapo bize kutafuta habari za yule Ng'ombe kutaka kujua hali yake baada ya ile ajali.
Kuna diaspora mmoja kasema kama huyo Ng'ombe atahitaji matibabu mazuri zaidi anaijua Hospitali moja mahiri ya UC Davis Veterinary Hospital iliyoko California huko Marekani.
Na kama aliuawa kwenye ile ajali Kuna watu wamejitolea kugharamia mazishi yake kwa hoja kuwa mashujaa hawaliwi bali huzikwa kwa heshima zote ili iwe kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.
Lakini habari za chini chini kutoka Katoro kuwa kuna tajiri mmoja mmliki wa Ng'ombe kasema kama yule Ng'ombe yupo hai basi yeye atabadilishana na mmiliki wake Ng'ombe mmoja kwa Ng'ombe wake mia Moja.
Msukuma huyo "chapa ya Ng'ombe" amesikika akisema kuwa ni heri kuwa na Ng'ombe mmoja mpigana vita kuliko kuwa na Ng'ombe mia wala majani wasio na faida.