Kuna uwezekano mkubwa Hamas ni kundi maalum la Israel lenye lengo la kutimiza Mipango ya Wazayuni hapo Palestina

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
Kwema Wakuu!

Kwa jinsi mambo yalivyo ninawasiwasi mkubwa kuwa Hamas sio vile wengi tujuavyo. Wengi tunajua Hamas ni kundi la kiharakati la kupigania haki za Wapalestina ikiwemo haki za kukataa Ukoloni wa Wayahudi katika Ardhi yao. Kwa nje inaonekana hivyo lakini ukichunguza ndani unaona kitu kingine cha tofauti.

Mbinu wanazotumia Hamas haziendani na malengo na mipango yao. Mipango na malengo ya Hamas mikuu ni kuchukua ardhi yao inayokaliwa na wayahudi. Kutetea haki za Wapalestina dhidi ya Wayahudi. Kumbuka haki namba moja ya mwanadamu ni Haki ya kuishi.

Katika mikakati na harakati za kupambana na Wayahudi ni lazima walinde Haki ya Wapalestina, ndugu zao hasa haki kuu ya kuishi.

Tangu kundi hili lianzishwe hakuna mafanikio yoyote yaliyopatikana katika harakati zao. Zaidi ninaona kama ndio wanawasaidia Wayahudi kutimiza malengo yao.

Ukiangalia tukio la 7 October, Kwa jicho la ndani utagundua pasi na shaka kuwa lile tukio ni mpango wa Wazayuni kuendelea kutimiza mipango yao ovu ya kuchukua na kudhorotesha haki za Wapalestina.

Naamini kwa asilimia 90% kuwa Hamas ni kundi la Kizayuni. Ingawaje wengine watabisha lakini kama wakitumia jicho la ndani watagundua kile nikisemacho.

Yaani Hamas waliowaarabu wanajua kabisa wakianzisha vita na Wayahudi zama za leo watashindwa, na watasababisha madhara makubwa kwenye jamii na nchi yao alafu waanzishe vita. Sidhani kama Wapalestina ni wajinga kwa kiwango hicho. Hata wanyama hawawezi kuanzisha vita wanaojua kabisa watashindwa na kusababisha maafa kwa familia zao.

Hamas ni kundi maalum lililoanzishwa na Wazayuni. Kutokana na namna wanavyojaribu kupambana.

Mbinu wanazotumia zitumia zote zimelenga kuwadhuru wao wenyewe kwa asilimia 100% hivi kweli hapo huoni kuna tatizo.

Iran yupo Smart. Anajua kabisa yeye kwa muda huu bado hana uwezo wa kupambana na Wayahudi na Magharibi. Hivyo hatakuwa tayari kuanzisha kile ambacho hataweza kukimaliza na ambacho kitamdhuru yeye mwenyewe na kumrudisha nyuma miaka mia.

Poleni sana Palestina. Hamas wamewasaliti.
 
Israel inapigana na Hamas, Sio Palestina.

Hamas anachofanya ni kurusha roketi sehemu zenye raia wa Palestina kama kwenye misikiti, day care za watoto, ahule, kambi za wakimbizi, n.k. ngao ya Hamas ni raia wema wa Palestina.

Ndio maana mara nyingi Israel ikiona sehemu flani ya Gaza inarusha makombora huwa inatoa notice hilo jengo watu wake watoke kabla ya kulipua, baadhi ya vyombo vya habari hawaonyeshi hizi notice kwa maksudi ili kuwachafua Israel.

kuna muda kunakuwa hakuna namna unakuta jengo linarusha makombora kibao na Hamas wanatishia raia wa Palestina hakuna kuondoka, hapo inabidi tu jengo lilipuliwe kuzuia maafa ya watu wengi upande wa Israel
, na hii ndio furaha ya Hamas kusingizia Israel inaua raia wema wa Palestina.

Kinachofanyika sasa ni kuwatoa kwa dharura wapalestina Gaza ya kaskazini wahamie kusini kwa muda na tayari mazingirs ya malazi, chakula, dawa, n.k. yameandaliwa, kaskazini ndio ngome kuu wabaki Hamas wenyewe iwe ni ile vita original zipigwe kavu bila Hamas kujificba nyuma ya raia.
 
Unataka kusema Israel iruhusu wafe raia wake 1400 eti watafute sababu ya kuivamia Gaza? Ni hivi Hamas walikosea hesabu zao walipoishambulia Israel na kuchukua mateka walitegemea Israel itaogopa kuivamia Gaza kisa mateka na mikwara mbuzi ya Iran na Hezbollah ila kiukweli kichapo Gaza inachopata ni cha kutia huruma hawakutegemea.

Sent from my Infinix X663 using JamiiForums mobile app
 
Yote yanawezekana Kwa sababu ukiangalia na shambulizi la sep 11 kule USA inafikirisha sana, basi hamasi watakuwa wanatunia mafawa ya kulevya wakishavuta wanaona IDF si chochote, na kwa usalama wa Israel inatakiwa walifute kundi la hamasi kwenye uso wa Dunia halafu eneo Hilo apewe Mahamoud Abas ili alisimamie pamoja na wanachama wa Fatah.
 
Israel inapigana na Hamas, Sio Palestina.

Hamas anachofanya ni kurusha roketi sehemu zenye raia wa Palestina kama kwenye misikiti, day care za watoto, ahule, vyuo, n.k. ngao ya Hamas ni raia wema wa Palestina.

Ndio maana mara nyingi Israel ikiona sehemu flani ya Gaza inarusha makombora huwa inatoa notice hilo jengo watu wake watoke kabla ya kulipua, baadhi ya vyombo vya habari hawaonyeshi hizi notice kwa maksudi ili kuwachafua Israel.

kuna muda kunakuwa hakuna namna unakuta jengo linarusha makombora kibao na Hamas wanatishia raia wa Palestina hakuna kuondoka, hapo inabidi tu jengo lilipuliwe kuzuia maafa ya watu wengi upande wa Israel
, na hii ndio furaha ya Hamas kusingizia Israel inaua raia wema wa Palestina

Na hii ndio Siri ya Hamas. Inawatumia raia wema Kama Kinga. Ndio maana watu wengi wanakufa , maana jamaa wanarusha makombora kutokea kwenye kambi ya wakimbizi.
 
Unataka kusema Israel iruhusu wafe raia wake 1400 eti watafute sababu ya kuivamia Gaza? Ni hivi Hamas walikosea hesabu zao walipoishambulia Israel na kuchukua mateka walitegemea Israel itaogopa kuivamia Gaza kisa mateka na mikwara mbuzi ya Iran na Hezbollah ila kiukweli kichapo Gaza inachopata ni cha kutia huruma hawakutegemea.

Sent from my Infinix X663 using JamiiForums mobile app

Nadhani walichukulia business as ussual. Hawakujua Israel amaeamua kuwasambaratisha.
 
Back
Top Bottom