Kuna umuhimu gani wa kuwa na vioo vinavyofunguka na kufunga katika madirisha ya mabasi?

Mia ya noti

JF-Expert Member
Dec 30, 2018
850
1,176
Nimejiuliza hivi kwa sababu ni kawaida kusafiri ndani ya basi lenye abiria zaid ya sitini bila hata mmoja kufungua kioo cha dirisha.
Na pia ukifungua wa siti ya nyuma analalamika upepo unampuliza.
Watu mnasafiri muda mrefu bila hewa mpya kuingia ndani ya basi madhara yake ni kuumwa kichwa na uchovu mwingi baada ya safari.
Kuna wale hata gari ikiwa na AC wanalalamika inawaletea matatizo kwenye kifua, hawa sijui kwa nini wanapanda gari zenye AC.
Hivi haiwezekani vioo vya mabasi vikawa Kama vya milango ya gari za binafsi (kupanda na kushuka) ili mtu aweze kukifungua nusu kupunguza upepo?
Angalau hii itaokoa afya zetu watanzania tusiopenda kufungua vioo vya madirisha.
Nawasilisha.
 
Itakuwa ni uchafu Kila seat kuwe na mashine ya power window Kwa ajili ya vioo.

Mabasi ya kisasa saizi vioo Huwezi kufungua ni Sealed hata ukifika Sehemu ya nyanya,chungwa na mahindi hufungui. AC Kila abiria hata control eneo lake
 
Itakuwa ni uchafu Kila seat kuwe na mashine ya power window Kwa ajili ya vioo.

Mabasi ya kisasa saizi vioo Huwezi kufungua ni Sealed hata ukifika Sehemu ya nyanya,chungwa na mahindi hufungui. AC Kila abiria hata control eneo lake
Sijawahi kupanda basi la hivyo mkuu.
Hapo ni Kila abiria anakuea na siti yake au mnakaa wawili? sabbu mkikaa wawili tu inawezekana mwenzako hapendi AC tayari tabu unaanza.
 
Weee mim nafungua dirisha na wala sijali.mwanzo mwisho kwanza sipend hewa nzito.
Unakuta gar inatoka mwanza mpaka dar mtakua watu humo
 
Kuna watu wakipanda gari, Vioo kama vimeshushwa, analalamikia baridi, au upepo, Wakati hizi gari ndogo, ukipandisha vioo, bila kuwasha AC, baada ya dakika kadhaa, mnapata punzi kwa taabu.
 
Back
Top Bottom