Wamiliki wa mabasi fanyeni service za bodi na ndani ya mabasi siyo injini tu

Mantombazane

JF-Expert Member
Sep 7, 2014
572
356
Kuna kitu nimeona wamiliki wa mabasi ya abiria wanajisahau kuhusu service za magari yao. Wengi wanajikita kwenye injini, spring na mabush tu lakini hawajali kabisa service za ndani ya mabasi na bodi kwa ujumla ambazo ni sehemu muhimu kwa abiria zitakazo wafanya wapende kusafiri na mabasi yenu.

Unapanda basi unakuta USB zimekufa na hazifanyiwi service wakati ni sehemu ya muundo na mahitaji ya abiria kwa mujibu wa watengenezaji. Sasa unaingia na simu haina chaji unashangaa zote hazifanyi kazi, mikanda mingine haifungi, viti havi adjust, madirisha hayana handle za kufunga na kufungua, viti vimechanika, basi ndani ni chafu wao wanafagia tu lakini hawapeleki hata siku moja basi likaoshwe vizuri likapigwe hata polish ndani kuondoa inta za uchafu wa mafuta yaliyoachwa na abiria au vumbi. Mbaya zaidi unakuta mengine frem za vioo zimelegea au ile mipira au bushi za vioo zimekufa basi njia nzima makelele ya mitetemo ya vioo paraaaaaaaa paraaaaa na usiombe likapita rough road yaaani itabidi uzibe masikio. Mengine unakuta staff carrier imelegea basi ni kelele njia nzimaaa!

Halafu acheni uongo kama huduma hakuna msimwandikie abiria kuwa mnatoa wakati ni uwongo. Unaingia unakuta wameandika FREE WI-FI lakini ukiwa humo hakuna kitu kama hicho. Kwanini kutudanganya wateja? Mara ooh Full AC ukiingia hakuna kitu. Hebu wamiliki badilikeni basi linatakiwa likamilike kila kitu na limuwezeshe abiria asafiri kwa raha kama alivyotarajia hivyo kuendelea kutumia huduma zenu. Kwa hili niwapongeze DELUX bus la Iringa. Nimesafiri nao mara nyingi USB charges zao zipo vizuri sana labda kwasababu zipo chini ya kiti ndiyo maana zinadumu au mmiliki yuko makini. Mabasi mengine majina makubwaaaaa lakini hamna kitu.
 
Kwani wanaoharibu hiyo miundo mbinu humo ndani ni ng'ombe au binadamu?

Kwanini huwaombi wasafiri kuwa japo na ka ustaarabu kidogo?

Ukisikia tozo miamala ya simu ujue hao unawaita kwenye mabasi:

IMG_20210821_183300_715.jpg

IMG_20210824_125202_848.jpg

Wako huko, dhoofrey bin taabani.

Labda kama umedhamiria kuwakamata uchawi tu mkuu.
 
fummigation tu mtihan mule mavyakula yanatupwa kungun wapo badala ziwe zinaoshwa na kupigwa deki wao wanampa teja anapisha pisha kafagío imetoka
 
Back
Top Bottom