Kuna umuhimu gani wa kusali kabla ya Kula?

Show Game

JF-Expert Member
Nov 7, 2023
318
1,083
Naomba mnielezee kwa kina kuhusu hii kitu

Umuhimu wake hasa ni upi maana sasa naona naendeshwa na imani nyingi sana mpaka nashindwa kuishi kwa amani

Au kusali kabla ya kula kunaweza kukuepusha na chakula chenye sumu ya Panya?

Au LIMBWATA?
 
Kama vile unavyosali ili Mungu akupatie mafanikio katika maisha na kazi yako. Basi chakula ni moja ya sehemu unazopata kupitia mafanikio yako ya kazi na utafutaji wako. So mshukuru Mungu kwa kufanikisha umepata chakula ili kiendelee kukujenga kimwili na kiroho.
 
Ni muhimu mkuu kusali kabla ya kula,siyo kuepuka sumu tu na limbwata Chakula chenyewe tu kinaweza kukuletea mushkeri mpaka ukashangaa,
Chakula unachokula kinaweza kukukaba au unaweza kupaliwa au kadhia yoyote ile kutokana na chakula ambacho wewe unaona kawaida tu kula..
 
Ni uamuzi wako mkuu, mimi kikifika mezani ni kunawa na kula tu.
 
Tumeagizwa yote tufanye kwa jina la Yesu, ikiwemo kula,kusafiri,kwa wanandoa hata sex ifanywe kwa jina la Yesu.Yaani kumtanguliza Mungu kwani hicho chakula tumepewa na Mungu hata kama tumekinunua kwa fedha zetu ila Mungu ndie alietupa nguvu za kupata hiyo fedha, lakini pia chakula kinapaswa kutakaswa kwani hatujui kimepitia kwenye njia ipi mpaka tunakipata,kwa uthibitisho zaidi soma hapa;

Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.

1 Wakorintho 10:31
Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.

Wakolosai 3:17
 
Naomba mnielezee kwa kina kuhusu hii kitu

Umuhimu wake hasa ni upi maana sasa naona naendeshwa na imani nyingi sana mpaka nashindwa kuishi kwa amani

Au kusali kabla ya kula kunaweza kukuepusha na chakula chenye sumu ya Panya?

Au LIMBWATA?
1Wakorintho 10:31,Inasema hivi

1 Wakorintho 10
31 Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.

Kumbe tunasali kabla ya kula/kunywa ili kumpa Mungu Utukufu kwa kutujalia riziki.

Katika Barua yake Mtume Paulo kwa Warumi,Paulo anasema tunapokula tunakula kwa Bwana,kiufupi anazungumzia hbr za ulaji wa vyakula fulani na ishu ya watu kutokula vyakula fulani kuwa hao wote wanafanya kwaajili ya Bwana.

Warumi 14
6 Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; : kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu.

Kumbe kusali pia ni ishara ya kutambua kuwa kila kitu kimetoka kwa Mungu na hivyo tunamshukuru kwa kusali.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Ni muhimu mkuu kusali kabla ya kula,siyo kuepuka sumu tu na limbwata Chakula chenyewe tu kinaweza kukuletea mushkeri mpaka ukashangaa,
Chakula unachokula kinaweza kukukaba au unaweza kupaliwa au kadhia yoyote ile kutokana na chakula ambacho wewe unaona kawaida tu kula..
Hayo yote yanaweza kukupata hata ukisali. Kusali kabla ya kula ni imani tu, nothing else.
 
Kama unanijua vema dunia na madhara yaliopo kwenye ulimwengu.na kama unamwamini M
Mungu muumba mbingu na nchi hutokaa uulize hili swali
 
Naomba mnielezee kwa kina kuhusu hii kitu

Umuhimu wake hasa ni upi maana sasa naona naendeshwa na imani nyingi sana mpaka nashindwa kuishi kwa amani

Au kusali kabla ya kula kunaweza kukuepusha na chakula chenye sumu ya Panya?

Au LIMBWATA?
Zaidi ni kutoa Shukran kwa rizki hiyo!

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom