Narudi kijijini kulima, maisha ya kwenye jiji la Dar nimeshindwa, nimekubalii🙌🏽

Bata Boy Official

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
259
308
Wakuu natumai mko poa kabisa
Mimi ni kijana ambaye nimeamua kuwa muwazi kuwa asiyekubali kushindwa si mshindani.

Jiji la Dar es Salaam limenishinda, Nimekubali na sitaki tena maisha ya jiji lolote. Sina degree, diploma wala cheti chochote, pesa yote niliyokuwa najichanga mwisho wa siku inaishia kwenye Kodi, umeme, maji, usafi, ulinzi, taka, chakula, na kulipa madeni. Sasa huu mchezo nimeuchoka. Maana hii ni mark-time, hakuna chenye nna fanya, hata zile raha za jiji wanazozisema sizifaidi maana nikisema nitenge 30k au 50k nikale Bata, ohoo nimeishaa...siioni future kabisa.

Hivyo wakuu nimeamua kwenda kijijini kushika jembe kulima kwa bidii na uaminifu, na kuishi maisha ya chini kabisaa...maisha yangu ikibidi niyamalizie huko huko kabisa. Kusali, kulima, kula, kulala ivyo yaan.

Kwahiyo wanajukwaa naombeni kwa ambaye ni mkulima au anamashamba huko vijijini, au ni mwenyeji wa mikoa ya kilimo sana na ameelewa hali yangu naomba anipokee , hata kama hakuna umeme, au nyumba ya kulala...nipo tayari kulala hata kwenye mahema nje humo humo mashambani endapo hakuna wanyama wakali lakini.

Hata kama sitalipwa pesa yoyote, ilimradi nipate chakula na niwe na amani ya moyo inatosha kabisa. Maana jiji limeninyoosha.

NB: Sijayakatia tamaa maisha, nimelikatia tamaa jiji.

Asanteni sana kwa maoni na michango yenu mnayoenda kuitoa.

Mungu azidi kutupa Amani na Upendo na Mshikamano.
images (8).jpeg
 
Kila kitu kina gharama zake.

Hata huko kijijini kwenye kilimo hakuna urahisi kama watu wa mjini ambao hawakuwahi kuishi kijijini hufikiria,hususani mtu mwenye mtazamo kama wako ..kwamba umeshindwa maisha ya mjini umeamua urudi kijijini kulima.

Ukifika kijijini inakubidi ukubali kupokea matokeo yoyote shambani. Mwanzo wa kilimo Huwa mgumu,miezi Sita ya mwanzo inabidi upambane kweli kweli ,kuna muda unaishi kijijini unakosa hata buku mbili,full ukata. Lakini pia hata baada ya kuvuna masoko muda mwingine yanazingua.

Kuna muda mazao ya Biashara kama nyanya,matikiti na vitunguu mnapoamua kuleta mjini kwa mauzo hukutana kutoka mikoa mbalimbali.mfano unakutannyanya ya morogoro,nyanya ya Lindi,nyanya ya Arusha nk,jambo ambako hupelekea bei kushuka sana. Hapa ndipo unakuta mkulima anakimbia mzigo wake maana mzigo auhuziki na mwenye gari uliyemkodi anasubiri chake kama mliambizana mtapeana Hela baada ya mzigo kuuza.

Wakati mwingine madalali wanazingua sokoni. Mzigo unao,ila dalali pale stereo anataka kukulalia.

Ila kwenye kilimo ukikutana msimu mzuri wa hayo mazao unatoboa,maana Kuna kipindi nyanya Moja mjini huuzwa hadi mia 2,kitunguu pia kinauzwa hadi mia mbili,alafu kidogo. Hapa ndiyo unakuta dalali anakupokea na mzigo kama Rais wa nchi na anakupangia gesti Kali Huku akiuza mzigo wako.

Mkuu hii ni nyeupe na nyeusi nakupa maana haya ndiyo maisha ya kilimo unayokwenda kuyachagua.

Nakushauri ukifika huko kijijini,kwa kuanzia wakati unajiandaa na kilimo cha muda mrefu,hakikisha unatafuta eneo la kukodi kandokando na chanzo cha maji kisha unalima bustani za mbogamboga kama mchicha,bamia,nyanya chungu,matembele na majani ya maboga ambazo ndani ya mwezi na nusu unakuwa imeshaanza kutengeneza vihela vya sabuni na kubadilisha dagaa siku ukichoka majani. ( Mfano mchicha kuanza kuandaa matuta hadi kumwaga mbegu na kuvuna hazizidi wiki sita). Uzuri wa mbogamboga hautegemei kupelekea mjini maana hata watu wa eneo lako hapo kijijini watakuungisha mchicha,au matembele au bamia nk.

Mimi nimewahi kuitumia hii mbinu ya kulima bustani za mbogamboga na ilinisaidia sana vihela vidogo vidogo. Vi 10k,20k vilikuwa haviniaumbui. Namwagilia zangu nyanyaau vitunguu unakuta kaja mama anataka umuuzie biringanya au mchicha wa buku. Masisha yanasonga.

Ila kumbuka hii :

"stress is the gape between expectations and reality. The more the gape,the more the stress".

Katika maisha Fanya kazi kwa bidii zote lakini punguza matarajio. Hii point ndiyo imekufanya umepaona mjini jau na hapakufai,umeamua upakimbie. Kuwa makini uendako usije ukapakimbia pia na huko,ukaishia kuyachukia maisha jumlajumla.

Mwenyezi Mungu akubariki sana katika safari yako ya kutafuta uhuru.
 
Tulipanda Mahindi mvua zikawa nyingi hayakuota saiz mpunga maji yamekauka yote majarubani kalibu kijijini.
Hivi ni vitu vya kawaida sana katika maisha.

Hata mijini watu wanatia mitaji katika Biashara kisha inaungua na wanaanza upya tena.

Inawezekana pia hayo mahindi yangeota na ungevuna vizuri,lakini wadudu wangeharibu,au ungetia dawa,lakini ukakosa wateja.

Kuna wakati kijijini kilo ya mahindi hufika hadi mia 2,mfano vijiji vya Songea maana mahindi yanakuwa mengi sana.

Maisha haya hayajawahi kuwa mepesi.

Wakati mwingine ni "wakati na bahati humpata mtu", kama Biblia inavyosema.
 
Kwahiyo wanajukwaa naombeni kwa ambaye ni mkulima au anamashamba huko vijijini, au ni mwenyeji wa mikoa ya kilimo sana na ameelewa hali yangu naomba anipokee , hata kama hakuna umeme, au nyumba ya kulala...nipo tayari kulala hata kwenye mahema nje humo humo mashambani endapo hakuna wanyama wakali lakini.
Kuna uzi wa jamaa wa wilaya ya Tanganyika, Mwese namba 4 humu utafute ukaungane naye. Lakini huko uende na adabu zote kuna akina ngosha ukileta ujinga wa mjini wanakugawana! Kilimo chenyewe kule kinakubali! Ni wewe tu na nguvu yako ya kufyeka mapori!
 
Kilimo cha jembe la mkono ni kigumu. Kama huna pesa ni bora ubaki kuwa hata dalali mjini.

Nyumbani kuna mashamba kadhaa sasa kutokana na umasikini huwa tunaenda kulima kifamilia asee mnapiga jembe la mkono balaa ukija kwenye mavuno nisawa na hakuna ilikuwa inanipa maumivu kiasi kwamba kama kijana unatakiwa kutafuta njia uwatoe wazazi kwenye hiyo jehanamu.

Mimi naona ili kilimo kiwe na tija inatakiwa uwe na mtaji fulani wa kuanzia kukodi, kulima, palizi,mbolea, mbegu bora ukifeli kwenye hivyo vitu hapo nibora usiende kupoteza nguvu bure.
 
Nataman kukuchukua ILA IT'S TOO LATE niko na wenzako watatu mwaka huu mahindi kuna kibanda wanakaa kazi yangu ni kuwaletea dagaa na Unga tu. Pole mwaka huu TAFUTA Shamba lima mapema mvua tu zikianza piga Maharage au karanga kama ardhi itakuruhusu mtafutaji hachoki/hakosi.
 
Wakuu natumai mko poa kabisa
Mimi ni kijana ambaye nimeamua kuwa muwazi kuwa asiyekubali kushindwa si mshindani.

Jiji la Dar es Salaam limenishinda, Nimekubali na sitaki tena maisha ya jiji lolote. Sina degree, diploma wala cheti chochote, pesa yote niliyokuwa najichanga mwisho wa siku inaishia kwenye Kodi, umeme, maji, usafi, ulinzi, taka, chakula, na kulipa madeni. Sasa huu mchezo nimeuchoka. Maana hii ni mark-time, hakuna chenye nna fanya, hata zile raha za jiji wanazozisema sizifaidi maana nikisema nitenge 30k au 50k nikale Bata, ohoo nimeishaa...siioni future kabisa.

Hivyo wakuu nimeamua kwenda kijijini kushika jembe kulima kwa bidii na uaminifu, na kuishi maisha ya chini kabisaa...maisha yangu ikibidi niyamalizie huko huko kabisa. Kusali, kulima, kula, kulala ivyo yaan.

Kwahiyo wanajukwaa naombeni kwa ambaye ni mkulima au anamashamba huko vijijini, au ni mwenyeji wa mikoa ya kilimo sana na ameelewa hali yangu naomba anipokee , hata kama hakuna umeme, au nyumba ya kulala...nipo tayari kulala hata kwenye mahema nje humo humo mashambani endapo hakuna wanyama wakali lakini.

Hata kama sitalipwa pesa yoyote, ilimradi nipate chakula na niwe na amani ya moyo inatosha kabisa. Maana jiji limeninyoosha.

NB: Sijayakatia tamaa maisha, nimelikatia tamaa jiji.

Asanteni sana kwa maoni na michango yenu mnayoenda kuitoa.

Mungu azidi kutupa Amani na Upendo na Mshikamano.
View attachment 2945601
Halafu ukiweza lima bange msimu mmoja tu.
 
Back
Top Bottom