Kuuliza Bei Kabla ya Kula uwapo Outing ni Akili na kujiamini lakini Malofa huona aibu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,904
KUULIZA BEI KABLA YA KULA UWAPO OUTING NI AKILI NA KUJIAMINI LAKINI MALOFA HUONA AIBU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Mmetoka out, mmefika kwenye mgahawa, mnaagiza chakula. Huoni aibu kuagiza chakula lakini unaona aibu kuulizia bei Kabla ya kuagiza. Hivi unaakili kweli? Ukiitwa Mshamba unarusha ngumi.

Mambo ya kuzingatia ukifika Mgahawani au hotelini kupata Lunch au Dinner;
1. Tafuta sehemu comfortable ambayo ni easy come easy to escape.
2. Hakikisha sehemu utakayokaa ni rahisi kuona kila anayeingia na Kutoka kama hautakuwa karibu na Mlango wa kutokea.

3. Hakikisha familia yako inaku-face wewe na kuupa mgongo Watu wengi wanapoingilia au kutokea au eneo ambalo linawafu wengi. Yaani Mkeo asiangaliane na eneo la kuingilia au kutokea, na pia asitazamane na eneo lenye Watu wengi(Wateja waliopo kwenye huo mgahawa).

4. Mhudumu akija kukuuliza asikae Nyuma yako. Ni aidha asimame katikati ya meza au usawa wa Mkeo ili uwatazame wote Kwa pamoja.

5. Omba Menu ya chakula, kama haipo. Waulize Kwa nini haipo Kwa ukali kidogo Hii itakusaidia Kupata attitude ya wafanyakazi wa huo mgahawa.
Agiza chakula unachokitaka na akupe bei yake Kabla hajaleta kama hakuna menu.

6. Endeleeni kupiga Stori lakini hakikisha Usalama umezingatiwa iwe wako binafsi na WA Mkeo au familia yako.

7. Maliza Kula. Lipia bills zako.
8. Uliza kama kuna yeyote anahitaji Huduma ya haha iwe kubwa au ndogo. Kama hayupo chapeni Lapa.

Epuka urafiki wa stranger unaokutana nao Migahawani au hotelini ambao wamekuja katika namna isiyo tabirika. Yaani unakuta MTU anakuja anacheka Cheka anawasalimia wewe na Mkeo alafu ni kama anataka ukaribu ambao haukuupanga.

Epuka Ofa za Strangers mliokutana Migahawani, Kwenye Resorts au Hotels au motels. Tena Ofa hiyo itolewe Mbele ya familia yako.
Kiuhalifu, ni rahisi kuingilia familia kupitia MKE au watoto.

Epuka na jihami na dharura zinazotokana na Mhudumu labda kumwaga kinywaji Kwa bahati Mbaya juu ya meza, au kumletea tishu au kufanya upendeleo wowote Kwa Mpenzi au mkeo. Hayo yote ni aidha Mkeo au Mpenzi wako afanye mwenyewe ikiwa kamwagiwa kinywaji au ufanye wewe mwenyewe. Tumia tishu aliyokupa mwanzo kisha atakayoleta mwambie akupe wewe.

kiusalama, inatakiwa Mke akae upande ambao hatazamani na watu wengi. Na pia akae upande wa kulia karibu na mkono wa kiume wa mwanaume Kwa sababu ndio wenye nguvu ( Kwa wale wanaotumia mkono wa kuume).
Kuruhusu Mkeo atazamane na watu wengi ni rahisi Kwa wahuni kuutumia mwanya huo kujipenyeza. Mkeo au Mpenzi wako anaweza kukonyezwa( kupewa signals) na wahuni. Kisha mawasiliano baina ya Mkeo na wahuni yakaratibiwa na Mhudumu kirahisi Mno.

Utashangaa Mkeo au Mpenzi wako au Binti yako anainuka anajifanya anaenda Washroom alafu mengine yanaendelea Huko ndani ya dakika mbili tuu.

Usijesema Taikon ninawivu au ninataka umchunge Mkeo au Mpenzi wako au Binti yako. Nop! Najaribu kutoa tahadhari Kwa maana ninajua matokeo ya kutochukua tahadhari.

Epuka kuagiza chakula na ukaitumia pasipo kujua bei yake. Hiyo ni dalili ya kutojitambua. Ni rahisi Watu wasio waaminifu Kutumia udhaifu wako kukuumiza.

Mfano, umefika mgahawani. Umeagiza Maziwa, mayai mawili na saladi.
Ukaletewa. Ukala ukafurahi. Unaletewa Bills unashangaa 12,000/=. Unaanza kujiuma Uma! Sio kwamba hauna hiyo Pesa. Nop unayo lakini unaona kama umepigwa.
Unaulizia imekuwaje, wanakujibu
Maziwa kikombe 6,000/=
Mayai @ 1000. 2,000/=
Saladi. 4,000/=
Jumla elfu 12,000/=
Unabaki unacheka cheka huku ukichomoa noti ya elfu 10 na elfu mbili.

Kabla hujaenda kula mgahawani lazima ujue utatumia shilingi ngapi, ndio maana kuuliza bei ya chakula ni muhimu.
Kisha kwenye hiyo Pesa ndio unaulizia vyakula kulingana na Bajeti yako.
Kuna kutenga Bajeti kisha aina ya chakula.

Kitendo cha kutokuuliza bei ya chakula moja Kwa moja kinatoa tafsiri kuwa huijui Pesa, wewe ni kapuku na Kwa Lugha nyingine huna Bajeti( mipango ya Pesa na matumizi yako).

Ndio maana kwenye mahoteli makubwa, migahawa mikubwa kuna Menu. Walioweka Menu sio wajinga. Kwa sababu wanajua kabisa Matajiri na wenye Pesa lazima wahitaji kujua Bei ya chakula Kabla hawajaagiza na sio vinginevyo.

Ukitaka kutapeliwa katika majiji makubwa jifanye maamuma uagize chakula bila kujua bei yake. Utashangaa unatajiwa bei mara mbili na wahudumu wasio waaminifu alafu chakula hichohicho wenzako wanakula Kwa bei nafuu.

Kamwe, usione haya kuwa na Akili.
Kamwe usikariri Maisha, kwamba ati Kwa vile bei ya Kiepe Yai Huko ulikotoka ni Tsh 2500/= basi ukadhani ukifika mtaa au mji mwingine bei NI Ileile. Utakuja kugombana na watu Kwa upumbavu wako.

Chips inaweza kuwa Ileile Ila bei tofauti Kutokana na Nani ameipika, wapi imepikwa, vifaa gani vimetumika, na mafuta Aina gani yametumika kukaangia.

Sasa wewe let's ulofa na ushamba wako ukadhani chips iliyopikwa na Sele wa buza ambaye hata Cheti Hana ukadhani itauzwa Sawa na Ochu wa Sinza aliyesomea upishi.
Au ukafikiri chipsi iliyokaangwa na Mafuta ya korie au mafuta ya wanyama ukadhani ni Sawa na chipsi itakayokaangwa na Mafuta ya Sunola ya alizeti. Bei lazima itofautiane.

Hiyo ndio Sababu lazima uulize bei Kama hakuna menu, Kwa sababu ya Bajeti yako, lakini pia utengenezaji na uandaji wavyakula gharama zake zinatofautiana.

Mtu alipie Fremu laki tatu Kwa mwezi unataka akuuzie chakula kama kile unachonunulia ambapo wanalipa elfu 50k?

Jiamini. Linda na thamini Jasho lako.
Kwanza ukiuliza tuu bei wahudumu wanajua huyu anajitambua.

Acha nipumzike sasa.

Nawatakia Sabato njema.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Siyo malofa mkuu,pesa,pesa.... wenye pesa.ukiwa na pesa huteseki

Na huwezi kuwa na Pesa kama huna nidhamu.
MALOFA hudhani kuwa na nidhamu ni kuteseka. Hiyo ni attitude Mbaya.

MALOFA hudhani kuwa na nidhamu ni AIBU.
Tangu MALOFA Wakati wanasoma walikuwa wanamtazamo kuwa nidhamu ni kujiabisha na kuteseka.
Yaani yeye kuwahi shule, kuvaa vizuri, kuachana au kunyoa vizuri wanaita mateso.

Sasa wamemaliza shule wapo mtaani wanaendeleza Ileile Tabia Yao.
 
Ukienda Mlimani city una idea ya bei ya soda, at least kadiria 3000, mimi huwa sina haja ya kuuliza maana naenda mahali ninapo class napo. HUWA nimekuwa makini wakati nipo USA na Poland, ila Tanzania? Sina sababu ya kuuliza bei.
 
charrote
 
Mlimani city unaletewa Menu.
Au uzikute mezani.
Ishu bongo wanaiba mpaka Menu
 
Baadhi ya sehemu wana tabia ya kupandisha bei hasa wakijua wewe ni mteja mpya.
 
Niliwahi kwenda Mwanza kwenye shughuli fulani,pembezoni ya hotel tuliyokuwapo palikuwa na mgahawa mzuri tu. Nikaulizia mchemsho samaki unagharimu kiasi gani? Nikaambiwa Tsh.11000.00 nikambiwa hiyo ni samaki kichwa,yaan nusu,nikaona kama ni bei sana.

Basi nkamwambia naomba chai ya maziwa na chapati mbili,hapo sikuuliza bei nkijua itakuwa ni kama bei zetu zile😂😂😂,bill imekuja ni Tsh. 8000.00,nilitukana matusi yote kimoyomoyo ila nikalipa. Kama ningeuliza bei ya chai na chapati basi bila shaka ningechagua mchemsho wa samaki.

Kuuliza bei kabla ya kuagiza ni jambo sahihi kabisa.
 
Mlimani city unaletewa Menu.
Au uzikute mezani.
Ishu bongo wanaiba mpaka Menu

Mimi kabka sijaenda mahali najua how much I want to spend and on top of that lazima uongeze 20%, na pia huwezi enda na hela kamili, mfukoni kila wakati unakuwa kama na extra 50,000.

Kamq makadirio yangu ni kutumia 15000, nitakuwa na 20,000 just incase, na pia lazima mahali popote nilipo na kuwa na 50,000 kwenye wallet, na pia Mpesa na Simbaking?

When I pick a restaurant na kuwa na consideration zote hizi, sasa, swali:

Kwa maelezo hayo, why should I ask of a price?
 
Back
Top Bottom