Mchekeshaji wa Kenya, Crazy Kenna, anaendelea kupata umaarufu kote barani Afrika kutokana na maudhui yanayoakisi maisha na uzoefu wa Waafrika. Ameteuliwa kuwania Tuzo za AFRIMMA za mwaka 2026, kutokana na mchango wake mkubwa na ushawishi katika nyanja ya burudani ya kidijitali barani Afrika.