Kuna uhusiano wowote kati ya malezi na kujifungua kwa operation?

Mamujay

Senior Member
Dec 24, 2022
150
342
Habari wana jamvi,

Nina jambo hapa naomba kuuliza. Je, kuna uhusiano gani kati ya kujifungua kwa kisu na malezi ya binti husika?

Bila kumkwaza mtu naomba kuleta hii mada mezani, mimi nachowaza nasema hivi uhusiano upo.

Mabint wengi ambao wamelelewa kwa kudekezwa ndio wanajifungua kwa operation.

Ukitaka kuli-prove hili fikiria kipindi cha nyuma mabibi zetu, wengi wao walikuwa wanajifungua bila operation lakini siku hizi mabinti wengi wanapenda operation.

Nitaendelea, mwenye nondo alete hoja.

NB: Hayo ni maoni binafsi.
 
Screenshot_20230120-225240_WhatsApp.jpg
 
Mimi naomba nicheke kwanza😂 ingekuwa mikiki mikiki ni sababu ya kujifungua kirahisi basi Mimi ningejifungua huku nakunywa juisi....nyumbani sikulelewa kizembe....Hadi ujauzito unatimiza miezi 9 Sina house girl, nilikuwa napambana mwenyewe, ...full kufanya mazoezi.

Kubwa zaidi nikakimbia kujifungulia Kairuki nikajipeleka Mwananyamala gvt na bima nikaficha.....nilikuwa natamani kupush, sitaki kabisa kusikia C section.....lakini wapiiii😂😂😂 Sasa hivi nna mshono wangu safi😂😂😂😂 Haya mambo ni kuomba Mungu tu.

Hata hiyo zamani unayoizungumzia, rate ya vifo vinavyotokana na uzazi ilikuwa juu tofauti na Sasa.
 
hakuna mahusiano ya malezi na kujifungua kwa C/S.
Miili yetu inabadilika kila siku kutokana na vyakula tulavyo, utaratibu wa maisha etc
 
Mimi naomba nicheke kwanza ingekuwa mikiki mikiki ni sababu ya kujifungua kirahisi basi Mimi ningejifungua huku nakunywa juisi....nyumbani sikulelewa kizembe....
Kwa hiyo ulitaka uwe na house girl wakati hujajifungua,ni walewale.
 
Kwa hiyo ulitaka uwe na house girl wakati hujajifungua,ni walewale.
Umeelewa lkn au unataka tu ulicho sema. Hakuwa na msaidizi kazi zake alifanya mpaka siku anaenda kujifungua.... Na wewe mada yako inahusu malezi, kwamba walodekezwa ndo wanao jifungua kwa operation.

Subiri ukue kwanza ndo utaelewa zaidi nikiendelea kukujibu napata hasira.
 
Wadada wengi wafupi wanajifungua kwa operation
Una utani na wapare.

Kwa sasa wanawake wengi hupenda Operation ili maumbile yasiongezeke
Wengine aibu kutokana na ufirwaji

Zamani

Operation ilifanyika kwa wanawake ambao mimba zimekaa vibaya, mtoto mkubwa kupita kwa njia ya kawaida

Kuchelewa jifungua etc

Siku hizi watoto wengi huzaliwa kabla ya muda wao
 
Habar wana jamvi,

Nina jambo hapa naomba kuuliza. Je, kuna uhusiano gani kati ya kujifungua kwa kisu na malezi ya binti husika...

Mambo ni mengi:
1: Upatikanaji wa huduma husika
2: Maendeleo ya teknolojia
3: Kuzingatia miongozo kwa watoa huduma
4: Wagonjwa kuhusishwa kuwa na haki ya uchaguzi wa aina ya matibabu na majadiliano ya haki zao
5: Pesa zitokanazo na aina ya uzazi/kujifungua.
6.......nk.

NB: Sekta husika inafatilia na kujitahidi kusisitika kila mtoa huduma kufuata miongozo katika suala husika.
 
Una utani na wapare.

Kwa sasa wanawake wengi hupenda Operation ili maumbile yasiongezeke...
Hiyo kutokana kwa mpalange nakubaliana na wewe. Lkn ukiacha hiyo fanya uchunguzi ni wadada wafupi
 
Hiyo haina ukweli mm siyo daktari lakin nmeshudia wanawake wachapakaz vizur tu n wanapat delivery complication hivyo wanafanyiwa operation.

Me naona hiyo shida inatokana tu na mambo ya hormones mwilin au bint kama atapewa mimba katika umri mdogo
 
Back
Top Bottom