Kuna ubaya gani Zanzibar ikajitenga na kuwa huru kama Zamani?

Mapinduzi yalifanywa na waZanzibari wenyewe. Hivi sasa Zanzibar bado mwarabu ananguvu zaidi kuliko mtu mweusi kwa sababu mbalimbali. Uchumi wa Zanzibar umeharibika kama ulivyoharibika wa Tanzania kwa sababu zinazofanana zaidi na za Zambia kuliko bara, i.e. utegemezi wa zao moja la Karafuu. Huu ulibomoa vipato vya raia na serikali mara pale bei yake ilipoporomoka. Sio kweli kuwa hakuna anayetaka Muungano, ila megafone za wanaoupinga zimekuwa tu kubwa. Lau kama wanaoupinga wangekuwa ni wengi zaidi, serikali ya SMZ isingeweza kuendesha mambo yake.

Si kweli Prof. Wangwe aliwahi kusema kukosekana kwa mwamko wa serikali ya muungano kulitia uzito zao la karafuu ni moja ya sababu iliyochangia kuua zao la karafuu. Serikali ya muungano ilitoa mtazamo zao (subsidies) kwenye kahawa, ndizi na katani ikaliona zao la karafuu halina faida.

Likewise since 1800 zanzibar ilikuwa bandari huru hili lilibadilika baada ya mapinduzi kwa kuhofia SMZ isije kupinduliwa ikawa SMZ inategemea biashara tu badala sector zengine za kiuchumi sasa hebu tufafanulie wewe nchi itasimama kweli!!!!
 
Wabantu walioko Zanzibar ni ndugu za wabara.

Sasa hiyo piga uwa kila baada ya miaka 5 ni kulinda maslahi ya hao wabara ndugu zenu....is that what you mean?

Mwaka 1964 muungano zaidi ulikuwa na faida za kiusalama hasa kwa Zanzibar
Sijuwi kama unajua unachokizungumzia, hivi sababu za kiusalama zinahusisha CIA?...tafuta vitabu usome ili ujue uhalisia, acha kuzungumza pumba ndugu yangu.Motive ya muungano ni Cold War, imeandikwa kwenye vitabu si kimoja wala viwili ni vingi tuu....Sasa nani anataka kuwa bizzi na Cold War?

kuna faida za kiuchumi ambazo pande zote zinafaidika nazo

Siwezi kuisemea Bara/Tanganyika ni faida gani wanazopata kiuchumi, lakini kwa Zanzibar hakuna sababu hata moja.Uchumi wa Zanzibar umekufa au kuuliwa zaidi ndani ya Muungano.

Na imekuwa vizuri ulipoanisha uchumi, kwani uchumi ungelikuwa uko juu asingelipiga kelele mtu yoyote.Uchumi ndio sababu ya kuvunjika miungano yote duniani, no difference na muungano wa TZ kuwa unakumbwa na matatizo hayo hayo....
 
Mdondoaji said:
Si kweli Prof. Wangwe aliwahi kusema kukosekana kwa mwamko wa serikali ya muungano kulitia uzito zao la karafuu ni moja ya sababu iliyochangia kuua zao la karafuu. Serikali ya muungano ilitoa mtazamo zao (subsidies) kwenye kahawa, ndizi na katani ikaliona zao la karafuu halina faida.

Likewise since 1800 zanzibar ilikuwa bandari huru hili lilibadilika baada ya mapinduzi kwa kuhofia SMZ isije kupinduliwa ikawa SMZ inategemea biashara tu badala sector zengine za kiuchumi sasa hebu tufafanulie wewe nchi itasimama kweli!!!!

Mdondoaji,

..Zenj wana wizara zao za Fedha na Kilimo. jukumu la kutoa ruzuku au kuendeleza zao la karafuu liko mikononi mwa serikali ya Mapinduzi kupitia wizara hizo mbili.

..bandari huru mmekuwa nayo toka wakati wa Salmin na hakuna mafanikio yoyote yaliyopatikana. halafu bandari ya Zenj inategemea soko la Tanganyika ambako tayari kuna bandari za Dar,Tanga,na Mtwara.

..Zenj itafute mbinu za kufufua karafuu na kuitumia yote ktk viwanda vyake vya ndani. sijui kwanini hili halijafanyika mpaka leo. pia tafuteni mbinu za kuendeleza utalii. nchi kama Seychelles na Mauritius zimepiga hatua kubwa kwa kutegemea utalii. sekta nyingine inayoweza kuwasaidia ni UVUVI.
 
Kuwa huru kama zamani gani? Hii notion ya kwamba kulikuwa na Zanzibar huru kabla ya muungano ni mythology.

Halafu Zanzibar kujitenga si tu hakuna ubaya, ni vizuri sana tu. I cannot wait for this day.
 
Mdondoaji,

..Zenj wana wizara zao za Fedha na Kilimo. jukumu la kutoa ruzuku au kuendeleza zao la karafuu liko mikononi mwa serikali ya Mapinduzi kupitia wizara hizo mbili.

..bandari huru mmekuwa nayo toka wakati wa Salmin na hakuna mafanikio yoyote yaliyopatikana. halafu bandari ya Zenj inategemea soko la Tanganyika ambako tayari kuna bandari za Dar,Tanga,na Mtwara.

..Zenj itafute mbinu za kufufua karafuu na kuitumia yote ktk viwanda vyake vya ndani. sijui kwanini hili halijafanyika mpaka leo. pia tafuteni mbinu za kuendeleza utalii. nchi kama Seychelles na Mauritius zimepiga hatua kubwa kwa kutegemea utalii. sekta nyingine inayoweza kuwasaidia ni UVUVI.

Hayo yote ya uchumi ni jukumu la serekali na uongozi, na vitu hivyo vyote vimekwama au kuwekewa mguu na Butiama.

Ikiwa uongozi wa Zanzibar ni ule ambao hauna uwezo, ni vipi nchi hiyo itaweza kufanya kitu chochote?

Bara inatakiwa iache demokrasia ifanye kazi yake, wananchi watoa maamuzi yao na yaheshimiwe.Halafu ndio muone kama Zanzibar itakwenda mbele au itarudi nyuma.Kwa hiyo simamisheni kwanza kupeleka JWTZ kwa wingi na usalama wote wa TZ kuwashusha Zenj ili kunyakua ushindi.
 
Mr.Froasty said:

Mr.Froasty,

..hebu nikumbushe ni uchaguzi gani mliofanyika Zenj ukamalizika bila manunguniko na mifarakano.

..siku zote serikali za Zanzibar zimekuwa propped up in one way or another by external powers. nakumbuka kusoma kwamba ati "wenyeji" wa Zenj waliwahi kuwakaribisha Waarabu kuwasaidia kumkabili Mreno. baadaye Muarabu naye akamuita Muingereza. Muarabu alipofurumushwa, wazalendo wakamkaribisha Mtanganyika.

..labda lawama mnayoweza kuielekeza kwa Tanganyika ni kwamba tumeshindwa kuwasaidia kujenga UMOJA ktk jamii yenu.

..baada ya Mapinduzi na Muungano hazikufanyika juhudi za dhati kuondoa ubaguzi na mifarakano iliyopelekea kufanyika kwa Mapinduzi ya 1964.

..CCM na CUF ni walewale ASP na Hizbu. bora kianzishwe chama kingine cha wazalendo wa Zenj ambao hawataendekeza siasa za pre-revolution Zanzibar.
 
Kama kweli tulikwenda zenj bila kuombwa na wazalendo, nitakuwa wa kwanza kusema kwa huu muungano..yaani sipendi kukaa nchi ambayo ina colonize other peoples country...hata kama ni nchi yangu
 
Mr.Froasty said:
Hayo yote ya uchumi ni jukumu la serekali na uongozi, na vitu hivyo vyote vimekwama au kuwekewa mguu na Butiama.

Mr.Froasty,

..kuhusu uchumi wa Zenj mimi nina swali moja tu: kinachowazuia wa-Zenj kuinyonya Tanganyika na kuendeleza nchi yenu ni nini?

..wa-Zenj mna access na ardhi pamoja na kila rasilimali zilizoko Tanganyika. Afrika Mashariki nzima; Rwanda,Burundi,Kenya,Uganda, wanalilia kile ambacho wa-Zenj mnacho. wanalilia free movement of labor na free access to land and its resources na Tanganyika. nyinyi wa-Zenj mmeachiwa milango wazi halafu mnalalamika??!!
 
Nafikiri hawafahamu watakachokosa. lakini mimi nimefikia uamuzi huu muungano ufe tu kifo cha mende.
 
Hivi kuna wanaofahamu msimamo wa kiongozi wa mapinduzi ya Zanzibar, Field Marshal John Okello kuhusu muungano? Ulikuwaje?
 
hatuwezi kudumisha mawazo ya kina marehemu let us create a new foundation for our coming new generation
 
WAHARAKISHE kujitenga.

Mwisho tutanaanza kuzungumzia mengine na wengine tuanze deal za silaha kwenda Zanzibar.
 
Deal za silaha, vipi wewe silaha kwa ajili ya ulinzi au unafikiri kuua binadamu wenzako kweli watu wengine wanapenda mauaji!
 
kila siku nashindwa kupata majibu ya kujitosheleza kutoka mtu wa upande wa zanzibar anieleze, kwanza mimi ni mbara na ktk suala la muungano sioni madhara yoyote kama utavunjika kwa upande wetu na nashindwa kuelewa wazanzibar hoja yao kwamba sisi tunawalazimisha kua ktk muungano, labda mzanzibar mmoja atueleze faida tunazopata kwa icho kinachoitwa tunawang'ang'ania wazanzibar!
nadhan ili ni fumbo ambalo wengi wabara hatuwaelewi wazanzibar wanachokisema labda waje wazi watueleze nini wangeendelea kama muungano utavunjika na kwa sasa vikwazo ni nini na wabara wanafaidika vipi!
kumbuka kwamba Tanganyika inatumia mwevuli wa jina la Tanzania katika mahusiano ya kimataifa, huku wazanzibari tumepigwa changa la macho na kiserikali chetu ambacho mwisho wake chumbe! Unaikumbuka kesi ya zanzibar kutaka kujiunga OIC? chukua hicho kama ni kigezo, nje ya muungano au ndani ya muungano wa serikali tatu tungeweza kujiunga na OIC na kunufaika na misaada ya shirika hilo, ni mfano mmoja katika mingi sana.
 
Mdondoaji,

..Zenj wana wizara zao za Fedha na Kilimo. jukumu la kutoa ruzuku au kuendeleza zao la karafuu liko mikononi mwa serikali ya Mapinduzi kupitia wizara hizo mbili.

..bandari huru mmekuwa nayo toka wakati wa Salmin na hakuna mafanikio yoyote yaliyopatikana. halafu bandari ya Zenj inategemea soko la Tanganyika ambako tayari kuna bandari za Dar,Tanga,na Mtwara.

..Zenj itafute mbinu za kufufua karafuu na kuitumia yote ktk viwanda vyake vya ndani. sijui kwanini hili halijafanyika mpaka leo. pia tafuteni mbinu za kuendeleza utalii. nchi kama Seychelles na Mauritius zimepiga hatua kubwa kwa kutegemea utalii. sekta nyingine inayoweza kuwasaidia ni UVUVI.
hizi za zenji siziiti wizara naziita idara, unakwenda wizara ya elimu kuulizia scholarship unaambiwa uvuke bahari uende wizara husika ya muungano bara, giv me a break my bro!
 
Hivi kuna wanaofahamu msimamo wa kiongozi wa mapinduzi ya Zanzibar, Field Marshal John Okello kuhusu muungano? Ulikuwaje?
huyu okello alikuwa kibaraka tu, masterminders wa mapinduzi ya zanzibar wanajulikana ila wanafichwa, kama yeye ni kiongozi wa mapinduzi ilikuwaje akapewa masaa kuikimbia Tanzania na kwanini asitafutwe alipoelekea na akaenziwa kwavile tunaambiwa mapinduzi yale yalikuwa matukufu?
time will tell!
 
Mr.Froasty,
..hebu nikumbushe ni uchaguzi gani mliofanyika Zenj ukamalizika bila manunguniko na mifarakano.

Tatizo sio manung'uniko ya wazenji, tunazungumzia elections standards.Fuatilia International observers reports kupata ushauri wa kitaalamu juu ya elections zinavyofanyika visiwani Zanzibar.

Kukusaidia kupata report hiyo, nitakupa nyaraka kutoka maktaba yangu ili upate picha kamili...halafu utajua kama ni manung'uniko au nazungumzia scientific data.

Mimi sio mwanasiasa (sijafungamana na CUF wala CCM)...wala sikuwepo kipindi cha kabla ya Mapinduzi.Ninachozungumza ni vitu vya kitaalamu na jinsi akili yangu inavyoweza kupembua.

Chaguzi za Zanzibar (nazungumzia 95-00-05 sio mambo ya ukoloni).

Nisikuchoshe, katika kufuatilia report hii kimbili kwenye sehemu za tables utagundua JWTZ wako mstari wa mbele kupiga kura Zanzibar...

http://www.scribd.com/full/25447355?access_key=key-a9c7e2bfyj2qy65ddzx
 
Mr.Froasty,

..kuhusu uchumi wa Zenj mimi nina swali moja tu: kinachowazuia wa-Zenj kuinyonya Tanganyika na kuendeleza nchi yenu ni nini?
Jibu moja tuu...muungano!

..wa-Zenj mna access na ardhi pamoja na kila rasilimali zilizoko Tanganyika. Afrika Mashariki nzima; Rwanda,Burundi,Kenya,Uganda, wanalilia kile ambacho wa-Zenj mnacho. wanalilia free movement of labor na free access to land and its resources na Tanganyika. nyinyi wa-Zenj mmeachiwa milango wazi halafu mnalalamika??!!
Labda nikuulize wewe hivi unajua Zanzibar ina mamlaka gani ya kujiendesha?Kama utaweza kunitajia mamlaka yaliyo chini ya SMZ, ndio utajua hizi lawama na kelele za wazanzibari kutaka kujitenga na kuona wanadhulumiwa ...zote ni sababu ya kuwa Zanzibar hawana mamlaka yao, yametekwa na kuhamishiwa Butiama.

Kwa hiyo hizi tuhuma za kuwa Tanganyika inaikandamiza Zanzibar sio propaganda na kelele zisizokuwa na mshiko.

Uchumi na pato la serekali linatokana na ukusanyaji kodi-lipo chini ya Muungano.Hayo mabenki yote unayoyasikia yanafanya kazi Zanzibar, hakuna centi hata moja inakusanywa na ZRB...zote zinakwenda TRA (aidha ni kiasi gani kinarudi kwa mlango wa nyuma...hapo utata)...lkn hii confirmed na Dk.Mwinyihaji kuwa hawapati kitu!

Zanzibar uchumi wake unategemea Bandari na Biashara, hivi vyote vimebanwa kwa jitihada za makusudi...Bandari imekwama na uboreshaji wa Bandari...almost this port is dead!

Hivi munajua nyinyi humu JF, kama Zanzibar wanalipa kodi mbili?ZRB na TRA...wakati nyie huko Bara munalipa TRA pekee??

Sasa mimi nikukuulizeni sababu gani kwa mfano Zanzibar ikazuiliwa kujiunga OIC?...Sasa ni mambo kama haya, ndio wazenji huona muungano ni nuksi tuu kwa maisha yao na ni kheri uvunjike!
 
Mdondoaji,

..Zenj wana wizara zao za Fedha na Kilimo. jukumu la kutoa ruzuku au kuendeleza zao la karafuu liko mikononi mwa serikali ya Mapinduzi kupitia wizara hizo mbili.

..bandari huru mmekuwa nayo toka wakati wa Salmin na hakuna mafanikio yoyote yaliyopatikana. halafu bandari ya Zenj inategemea soko la Tanganyika ambako tayari kuna bandari za Dar,Tanga,na Mtwara.

..Zenj itafute mbinu za kufufua karafuu na kuitumia yote ktk viwanda vyake vya ndani. sijui kwanini hili halijafanyika mpaka leo. pia tafuteni mbinu za kuendeleza utalii. nchi kama Seychelles na Mauritius zimepiga hatua kubwa kwa kutegemea utalii. sekta nyingine inayoweza kuwasaidia ni UVUVI.

Usinichekeshe Joka Kuu, Zanzibar kuna wizara au idara, bajeti ya wizara ya fedha zanzibar inatoka Tanzania Bara unategemea kuna wizara hapo au kijewe tu cha kahawa. Halafu zanzibar wanakuwaga hawana moto kama umekuwa mwingi wa observation mara nyingi moto zao (yaani mission kwa wasiofahamu) inatokea serikali ya muungano, mfano maisha bora nao wameiga zanzibar eti maisha bora na vyote vinatokea ndani halmashauri ya chama cha Chukua Chako Mapema (CCM) sasa pana uchumi hapo!!!!!

Unadhani kama moto (mission ya CCM) ni kuipa mkazo zaidi biashara kuna mtu atakuwa na interest na kilimo acha kutudanganya bwana wazanzibari wako makini mzee hadanganywi mtu eti wizara zao kuna wizara zanzibar au ni vijiwe tu. Chai za wizara zinatengenezwa chini ya miti na jiko la mkaa, I mean wizara nzima inakosa hata jiko!!!!.

Tuje katika bandari huru Salmin ndio alianzisha bandari but unakumbuka ni kwakiwango alivyopata tabu kupata ridhaa ya Muungano? Likewise Muungano ikakubali lakini wakadai eti wanakosa mapato ya bandari ikapigwa zengwe eti TRA wawe na kodi zao na ZRB pia (hili ndio kwa kiwango kikubwa kimeua biashara zanzibar). Mfanyabiashara zanzibar analipishwa kodi mara mbili wakati dar analipa mara moja. Sasa bandari huru ipo au bandari kilio!!!!!
 
Jibu moja tuu...muungano!

Labda nikuulize wewe hivi unajua Zanzibar ina mamlaka gani ya kujiendesha?Kama utaweza kunitajia mamlaka yaliyo chini ya SMZ, ndio utajua hizi lawama na kelele za wazanzibari kutaka kujitenga na kuona wanadhulumiwa ...zote ni sababu ya kuwa Zanzibar hawana mamlaka yao, yametekwa na kuhamishiwa Butiama.

Kwa hiyo hizi tuhuma za kuwa Tanganyika inaikandamiza Zanzibar sio propaganda na kelele zisizokuwa na mshiko.

Uchumi na pato la serekali linatokana na ukusanyaji kodi-lipo chini ya Muungano.Hayo mabenki yote unayoyasikia yanafanya kazi Zanzibar, hakuna centi hata moja inakusanywa na ZRB...zote zinakwenda TRA (aidha ni kiasi gani kinarudi kwa mlango wa nyuma...hapo utata)...lkn hii confirmed na Dk.Mwinyihaji kuwa hawapati kitu!

Zanzibar uchumi wake unategemea Bandari na Biashara, hivi vyote vimebanwa kwa jitihada za makusudi...Bandari imekwama na uboreshaji wa Bandari...almost this port is dead!

Hivi munajua nyinyi humu JF, kama Zanzibar wanalipa kodi mbili?ZRB na TRA...wakati nyie huko Bara munalipa TRA pekee??

Sasa mimi nikukuulizeni sababu gani kwa mfano Zanzibar ikazuiliwa kujiunga OIC?...Sasa ni mambo kama haya, ndio wazenji huona muungano ni nuksi tuu kwa maisha yao na ni kheri uvunjike!

Yap nilikuwa nakuja huko kwamba Zanzibar TRA kodi inakusanywa katika kila sekta, ZRB iko kama kipepeo tu na kupelekwa muungano halafu wanarejeshewa fungu lao Zanzibar kutoka na population yao na sio mapato yao. Unadhani kuna kitu cha maana hapo.

Tuje katika OIC wakati wa Salmin (Mie naweza kusema zanzibar hapa ilipata rais basi tu) aliona hili tatizo la zanzibar cashflow akaona ni vizuri tukajiunga na OIC kwani kuna misaada ilikuwa iletwe from OPEC countries BOT ikaizuia isipelekwe Zanzibar kisa eti ni sehemu ya Tanzania (Wakati walioenda kuomba ni wazanzibari). Badala yake ile misaada ikamezwa na Muungano ndipo jamaa akaona ni vema zanzibar iende ikawa mwanachama OIC kwasababu wanachama wengi wa OIC pia wamo OPEC hii ingelisaidia kupata misaada zanzibar. Hata misaada zanzibar inanyimwa kwa kisingizio eti mahitaji yake ni kidogo. Jamani huu si ukoloni tu hamna zaidi
 
Back
Top Bottom