Kuna ubaya gani Zanzibar ikajitenga na kuwa huru kama Zamani?

Marekani unafahamu ziko Nchi ngapi zilizoifanya kuwa - ( United State of America)
Sasa nakujulisha ziko Nchi 52. Ndiyo inaitwa Amerika.
Ulaya wameungana na hata kuwa na pesa yao yaani EURO.
Tanganyika na Zanzibar ziliungana kwa ridhaa ya sehemu zote mbili Tanganyika na zanzibar, Ikaitwa Tanzania.
Wewe unayelisemea hili nadhani wakati yote haya yanafanyika wewe hukuweko Duniani.
Ujue Mkishawachagua Viongozi hufanyamambo kwa matakwa ya wananchi na sio vinginevyo.
Hayo unayoyasema kama yatatokea basi Utaamini kuwa waliofanyakazi ya kuunganisha Nchi hizo walikuwa na akili ya kuona mbeli tofauti na wewe.
Usisahau kuwa mtu wa Bara ni vigumu kupata hata Kiwanja cha kujenga Zanzibar, Lakini Wazanzibar wengi wanaviwanja bara pamoja na majumba makubwa mbakubwa zikiwepo gorofa.
Hilo watu wa bara hawajasema lolote.
Wazanzibar ni Ndugu zetu sisi hatuna matatizo waje bara Viwanja Vipo, Wajenge na kufanyabiashara kubwa kubwa.
Ujue zanzibar wanazaliana pindi kwao kukijaa wanakaribishwa sana bara.
Moja wapo ya kuungana ni pamoja kuhakikisha tunakuwa na uhusiano mzuri na kupeana nafasi ya maisha ikiwa ni pamoja na Ardhi.

Unayedai Tuvunje Muungano huwatakiimema Wazanzibar.
Wazanzibar bara yako Mikoa yote na ni Watu Wema hawana Matatizo.
Na ninyi Wazanzibar Potoshweni na wahuni wachache muiache pepo yenu.
Ninyi mko kwenye pepo, Kama hamuamini Jitengeni, Au Vinjeni Muungano, Joto litawawakia hamtoweza kurudinyuma kamwe.
Mtalia na kusagameno.
Jihadharini ndugu zanguni.

Nadhani wewe hufahamu linalozungumzwa hapa. Katika muungano wowote lazima kuwepo na mutual agreement as kwanini tunaungana. Hizo unazozingumzia wewe ni habari za kuota kwani muungano wa Tanzania haukuwa na mutual agreement bali Karume kwa kuhofia kupinduliwa akaamua ajiunge na Tanganyika na nyerere kwa kuhofia zanzibar isiwe na maendeleo akakubali tuungane ili akimalize kisiwa sasa hebu tuambie pana mutual agreement hapo.

Hivi hujiulizi kwanini watanganyika wengi hawataki muungano!!!! na wazanzibari wengi hawataki muungano!!!! nani anautaka muungano???? Tizama kipimajoto kinaonyesha nearly 70 hauwautaki muungano je nani anautaka????
 
Lakini, hudhani alichosema Mwl kuhusu possibility ya Zanzibar kugawanyika (Unguja, Pemba!) endapo itajitenga na bara kina mantiki? Maana nje ya muungano hakutakuwa na 'wazanzibari', probably kutakuwa na 'waunguja' na 'wapemba'! Naona kuna mantiki kwa kiasi fulani hapa.

sielewi hizo mantik za nyerere...kalba ya muungano wa zanzibar na tanganyika ...jamuhuri ya zanzibar ilidumu kwa miaka mingapi? kwa nini kigezo kiwe alichokisema nyerere? for me nyerere was just a selfish dictator...and never was a saint as many of you portray him to be...
 
sielewi hizo mantik za nyerere...kalba ya muungano wa zanzibar na tanganyika ...jamuhuri ya zanzibar ilidumu kwa miaka mingapi? kwa nini kigezo kiwe alichokisema nyerere? for me nyerere was just a selfish dictator...and never was a saint as many of you portray him to be...

Unajua Nyerere alitufanya tuwe scaremongers ili apate kupandikiza siasa zake nchini. Maswali naulizaga kila siku humu jamvini sijibiwi bali ni mvua za lawama tu zinashushwa moja je mliwapa wazanzibari uhuru wao wa kujitawala wakashindwa? Je nani anautaka muungano maana wazanzibari hawautaki, watanganyika pia je nani anautaka? Mwisho je muungano huu ni lazima? Nikijibiwa maswali haya tutakuwa nadhani tumepata picha halisi on what is going on in zanzibar. Otherwise it is a typical scaremongering tactics tu!!!!
 
Siku hizi kelele za kuvunja muungano zimekufa kabisa.

Imegundulika kuwa zile huwa ni kelele msimu.
 
Back
Top Bottom