Kuna tofauti kubwa kati ya utani na udhalilishaji

Baada ya kuona neno "kweri kweri" nimegundua upeo wako ni level ipi hivyo ushauri wa bure ni kajiendeleze na elimu uelimike.
Ila kabla ya kukuacha nikuambie kuwa kufuatiliwa sana sio kuwa in kupendwa au kuku admire maana jee utasema hivyo hata kwa Dr Shika? matendo ya ajabuajabu yaweza kukufanya ufatiliwe sana

In kupendwa > ni kupendwa
Jee > Je
Ajabuajabu > ajabu ajabu
Ufatiliwe > ufuatiliwe

Unapokosoa wenzako hakikisha kwanza wewe unao huo unaouita ‘upeo’ sio unabwabwaja tu, kukosea ni sehemu ya maisha yetu ila tukosoane kwa heshima lengo ikiwa ni kuelekezana..... nawe nakushauri ukajiendeleze kielimu.


Usile Mbegu.
 
Je na mume wa huyo mama anajisikiaje Khantwe? Ataelewa kama ni utani? Hawezi kuhisi labda kuna jambo nambari moja analijua kati ya Kitwanga na huyo mama cheupe hasa ukizingatia ugonjwa wa wasukuma kwa wanawake wa hiyo rangi
halafu si ajabu alikuwa anaona wivu kuona mwenzie yuko na mwanamke mweupe
 
hahahahaha BAWACHA BHANA YANI WEWE UNAFIKIRI KIBOGA INA MAANA KAMA YAKO UNAYO ISEMA? KIBOGA INA MAANA NYINGI SANA WENGINE HUKO KANDA YA ZIWA NI TUNDA TAMU.....
BAWACHA ACHA KUJIPA PRESSURE
Mkiwa Wajinga msifikiri watu wote ni wajinga...so kwa kuwa Kanda ya Ziwa matusi na Ngono kwenu ni fahari basi iwe hivyo kwa TAIFA zima?

And what do you mean by the way...Japan wakituletea Balozi anayeitwa K**amoto hapa atapewa accreditation? ACHA UJINGA BASI
 
Nimekuwa nikimsikiliza ndugu yetu kwa Miaka yake minne ambayo amekuwa akiliongoza taifa..

Katika hotuba zake zote hulazimisha kuchomekea Utani Lakini utani huo Mara zote unakuwa centred kwenye Mapenzi, Ngono na Kujamiiana...KWA NINI ANAKUWA VILE?

Maneno mengine ni machafu sana na huyatamka mbele ya Mkewe, Mawaziri wa Kike na hata watoto wa shule ambao katu Katika mikutano yake hawakosekani...Mfano alipokuwa Kahama aliposema usipomtendea vema Mkeo hatakupa KIBOGA...hii Lugha ni chafu na haifai, Why akili yake Inakuwa hivi, kuna Tatizo la KISAIKOLOJIA kwenye Kichwa chake?

Nashauri Washauri wake waifanyie kazi hii kasoro, IT IS TOO MUCH NOW AND IT IS DISGUSTING


Ambacho hakijui huyu baba ni kwamba si kila mtu ana sense of humour. Baba wa Taifa Hayati Nyerere, Mzee Kikwete na Mzee Mwinyi walikuwa na sense of humour kiasili na nature huwa hailazimishwi. Mkapa hakuwa na sense of homour na alikuwa analitambua hilo vizuri so hakutaka kuforce kuwa nayo. Ukiwa huna sense of humour ukaforce utaishia kutukana na ndicho kinachoendelea kwa huyo baba. Akitaka utani kwenye hutuba basi uandaliwe mapema kwani yeye haya uwezo wa kutengeneza utani wa kwake papo kwa papo vinginevyo ataishia kutukana tu kila siku kitu ambacho si kizuri.
 
Mimi nilisikitishwa sana na maneno " wanawake weupe hoyee"

Miss Universe 2019 ni Black Beauty anayeitwa Zozibini Tunzi ambaye ni Miss South Africa 2019. Ni mweusi na ni mzuri. Najiuliza wanawake weusi wanajisikiaje wanaposikia " wanawake weupe hoyee" Nadhani kuna haja waandika-hotuba wa mzee wamwandikie hotuba ambayo ataifuata ili baadhi ya watu wasimwelewe vibaya.
 
In kupendwa > ni kupendwa
Jee > Je
Ajabuajabu > ajabu ajabu
Ufatiliwe > ufuatiliwe

Unapokosoa wenzako hakikisha kwanza wewe unao huo unaouita ‘upeo’ sio unabwabwaja tu, kukosea ni sehemu ya maisha yetu ila tukosoane kwa heshima lengo ikiwa ni kuelekezana..... nawe nakushauri ukajiendeleze kielimu.


Usile Mbegu.
Spell mistake na typing error ni vitu viwili tofauti. Walijua hilo?
 
"Kitwanga umemuacha mke wako, umeenda kwa mwanamke mweupe," alisikika mzee baba akimwambia aliyewahi kuwa waziri kwa kukaa pembeni ya mama mmoja mwenye rangi ang'avu. Kwa jamii iliyostaarabika utani wa namna hii unavuka mipaka. Kitwanga alidhalilishwa na yule mama alivunjiwa heshima.

Aghalabu utani wa mzee baba unavuka mipaka hasa akihusisha wanawake.Hii tabia inabidi ikome.

Aidha kuhoji kwa mzee baba hasa akiwa anahoji watendaji mbele ya wananchi ni kwaajili ya kudhalilisha na si kueleweshana. Mtakumbuka wakati anamuhoji mkandarasi kule Dodoma; Mkurugenzi wa Nachingwea; Afisa Polisi kule Butimba nakadhalika. Wote hao ni watu wazima wenye familia zao na mamlaka katika maeneno yao ya kazi, kwa kuwadhalilisha mbele ya kadamnasi anawavunja molari na kuwatisha watendaji wengine. Tabia hii inabidi ikemewe kwa nguvu zote. Nani atamfunga paka kengele?
Mzee Mzindakaya Je pale Sumbawanga?
 
Back
Top Bottom