Kuna tofauti kubwa kati ya mwanaume kuwa baba wa mtoto wako na mwanaume kuwa mwanaume uliyezaa naye

QEEN ADEMU1

Senior Member
Dec 24, 2019
134
324
Kuna tofauti kubwa kati ya mwanaume kuwa baba wa mtoto wako na mwanaume kuwa mwanaume uliyezaa naye.
Kuzaa na mwanaume fulani haimaanishi kuwa yeye ni baba kwa mtoto huyo.

Kuna wanaume hawajui jinsi ya kuwa baba, wanajua tu kugawa mimba, kisha wanatelekeza mimba na watoto. Kisha wao wanaendelea kula bata na kuku. Wengine umri mkubwa tu lakini hooooovyooooo!

Wanatelekeza watoto!

Mwisho wa siku mtoto amekua kwa jitihada za mama tu ndipo nao wanajipendekeza kwa mtoto eti "Fulani ni mtoto wangu".

Wasipopata msaada wa watoto hao wanahisi watoto hawawajali. Wanasahau kuwa nao waliwatelekeza hao watoto enzi zile.
.
MWANAMKE: Usifikiri kuwa kuzaa tu na mwanaume fulani kutamfanya awe baba wa mtoto wako. Sahau, kuwa makini. Usikurupukie tu kuzaazaa kama mbwa. Unataka kuonesha na wewe una uzazi kila rungu likipita mimba tuliaoa zipo ukiwa makini ndoa. Mimba sio gundi ya kukufanya uolewe.
.
MWANAUME: Jifunze kuwa baba. Umempa binti wa watu mimba muhudumie. Kutelekeza mimba na mtoto ni upumbavu. Halafu baadaye unaanza kujipendekeza, "Ile damu yangu kabisa lakini kanitupa. Nitammwagia radhi." Mwaga tu, zitakumwagikia mwenyewe.

Leo yako unayeiandaa ni wewe, ukicheza vibaya hao unaokula nao bata unaagiza bia mezani zinajaa unaona ujanja wakati watoto wako wako kwa bibi yao suruali zimechanika, hawana mashati. Hivi wewe ni mwanaume kweli?
Hao unaofurahia nao kuna siku watakuacha huna hata wa kukulipia bili ya dawa hospitali, utaaanza niitieni mwanangu!

MWANAMKE: Jifunze kujiongeza njia za uzazi wa mpango zipo nyingi sipendi nizitaje. Usitake tu kuzaaa halafu watoto unampelekea mama yako unarudi tena mjini. Unajua huzuni juu ya hao watoto unaowazaa na kuwaficha huko kijijini, hivi umewahi kulifikiria hilo?

Wanaume wenzangu najua wengi ukiulizwa una watoto wangapi unataja idadi unasahau wengine wapo wengi tu. Unakumbuka mimba uliyompa housegirl mama yako akamtimua; unajua mtoto ana umri gani sasa?

We mwanaume unakumbuka uliyempa binti yule dada muuza chakula halafu ukahama na kwenda kula pale? Hata kama humpendi mjali basi mwanao.

#Sijakasirika
#Usitelekeze #mimba #Mtoto

Sent using i phone x
 
Suala la mapenzi ya watu wawili waliolala kitandani wakapeana mimba ni complicated saana.

Ogopa jambo linaloendeshwa kihisia zaidi... usimlaumu yeyote hadi ujue kwa undani ilikuaje.

Kuna siku nilikuwa anaangalia paternity court.

Kuna mdada aliolewa 1992...nyuma yake alikuwa na makando kando mengi saana. Sasa akakutana na mwanaume wakawa wapenzi mwaka huo huo wakaona.

Baadae akajifungua akazaa mtoto wa kike. Mwaka 2013 wakiwa na mwanae wakakutana na ex wake. Yule ex akastuka mbona huyu mtoto anafanana na mwanangu. Ikabidi a claim mtoto anaweza kuwa wake maana umri wa mtoto unalingana na kipindi toka waachane.

Kesi ikawa kubwa... mme wa mdada anajua mtoto ni wake huyu ex mtu naye ana claim mtoto ni wake. Ikabidi kesi iende mbele wakapima DNA.

Majibu yaliyotoka ni kwamba mtoto sio wa wanaume wawili waliokuwa wanavutana...kuna mwanaume mwingine alikuwa anatoka naye kwa siri kipindi yupo na ex wake.

Mapenzi yana mengi saana.
 
Tunashukuru kwa ujumbe murua dada/kaka.

Ngoja yaje mafurushi ya humu usikie mapovu yao na uone yanavyojazana ujinga. Akili hamna.
 
Duuh very complicated... Sasa hapo ndoa ilidumu kwel?

Too bad mwisho wa siku wanaoteseka ni watoto wasio na hatia

Sent using Jamii Forums mobile app
Tayari anawatoto 2 wengine na huyo mama...ilibidi nao DNA zichukuliwe. Wote wakawa wake.

Ndoa iliendelea ila uaminifu baina yao nadhani utakwisha.
 
Kwann utiwe mimba bila kukusudia?
Kwanini upende bata kwa pesa za watu?
Kwanini ufanye ngono bila kukusudia kisa umelewa?
Kwanini mara kwa mara unaachana na huyu na kwenda kwa huyu?
Kwanini wewe kila siku unakosea kuchagua?

MY BROTHER SAY BIG BRAIN MATTER MORE.

Aki niko kwa relationship mala kwa mala naishia kufanya nae unpenetrated sexual intercourse.
Sijui naibiwaga🤔 ila namuamin japo kanipa mala chache. (Four years ago)
 
Back
Top Bottom