Kuna tofauti kubwa kati ya utani na udhalilishaji

Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
5,669
2,000
"Kitwanga umemuacha mke wako, umeenda kwa mwanamke mweupe," alisikika mzee baba akimwambia aliyewahi kuwa waziri kwa kukaa pembeni ya mama mmoja mwenye rangi ang'avu. Kwa jamii iliyostaarabika utani wa namna hii unavuka mipaka. Kitwanga alidhalilishwa na yule mama alivunjiwa heshima.

Aghalabu utani wa mzee baba unavuka mipaka hasa akihusisha wanawake.Hii tabia inabidi ikome.

Aidha kuhoji kwa mzee baba hasa akiwa anahoji watendaji mbele ya wananchi ni kwaajili ya kudhalilisha na si kueleweshana. Mtakumbuka wakati anamuhoji mkandarasi kule Dodoma; Mkurugenzi wa Nachingwea; Afisa Polisi kule Butimba nakadhalika. Wote hao ni watu wazima wenye familia zao na mamlaka katika maeneno yao ya kazi, kwa kuwadhalilisha mbele ya kadamnasi anawavunja molari na kuwatisha watendaji wengine. Tabia hii inabidi ikemewe kwa nguvu zote. Nani atamfunga paka kengele?
 
USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
2,685
2,000
Hivi Kitwanga anaakili gani kumuacha mkewe na kwenda kupiga soga na wanawake wengine, sisi waafrika mapenzi ni pale unapokuwa na ashiki tu.

USSR
 
Khantwe

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
50,439
2,000
Hapo kwa Kitwanga mimi naona ulikuwa utani jamani ila huko kwa watendaji naunga mkono hoja. Mbaya zaidi hata watendaji wake wanaiga hiyo tabia na kuitumia kwa watendaji wa chini yao.
 
sweettablet

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
5,109
2,000
Huu ni ushahidi kuwa mnampenda sana Rais Magufuli. Kila anapoonekana kwenye TV na kusikika redioni mnakuwa makini kweri kweri kutafuta cha kupost. Halafu mwisho wa siku mnashangaa kwanini amekuwa mtu maarufu zaidi Tanzania na Afrika kwa ujumla!!!
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
22,760
2,000
Mzeebaba nadhani kichwani kuna nut imelegea! Lisu alisema kila mmoja apaze sauti pale alipo. Wenye akili walimwelewa, praise team wakakejeli!
 
Laki Si Pesa

JF-Expert Member
Dec 20, 2018
3,042
2,000
jamaa anapenda sana kusifia wanawake weupe, sasa sijui mkewe anajisikiaje ukizingatia sio mweupe, basi tu tumuache , Post Trauma Psychology Disorder inatutesa wengi
 
Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
12,194
2,000
Kama sio Kitwanga kuchemsha akiwa waziri mpaka leo hii angekuwa sehemu ya baraza la mawaziri.

Kitwanga na JPM ni watu wenye kufahamiana kwa miaka mingi ni marafiki wa karibu.

Rais ni binadamu kama mwingine yoyote yule, anao marafiki wa kikazi na wale wa karibu.
 
Wasukuma na kanda nzima ya ziwa wanawake weupe ni dili.

Mkewe yupo nae miaka mingi, wanajuana na kuvumiliana na kusameheana.
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
34,403
2,000
Huu ni ushahidi kuwa mnampenda sana Rais Magufuli. Kila anapoonekana kwenye TV na kusikika redioni mnakuwa makini kweri kweri kutafuta cha kupost. Halafu mwisho wa siku mnashangaa kwanini amekuwa mtu maarufu zaidi Tanzania na Afrika kwa ujumla!!!
Baada ya kuona neno "kweri kweri" nimegundua upeo wako ni level ipi hivyo ushauri wa bure ni kajiendeleze na elimu uelimike.
Ila kabla ya kukuacha nikuambie kuwa kufuatiliwa sana sio kuwa in kupendwa au kuku admire maana jee utasema hivyo hata kwa Dr Shika? matendo ya ajabuajabu yaweza kukufanya ufatiliwe sana
 
inchaji

JF-Expert Member
Jul 5, 2019
929
1,000
wanaosema huyu mtu ni mnyarwanda wanaweza kuwa sahihi. kwa kawaida msukuma hawezi kumtania msukuma.
 
sweettablet

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
5,109
2,000
Baada ya kuona neno "kweri kweri" nimegundua upeo wako ni level ipi hivyo ushauri wa bure ni kajiendeleze na elimu uelimike.
Ila kabla ya kukuacha nikuambie kuwa kufuatiliwa sana sio kuwa in kupendwa au kuku admire maana jee utasema hivyo hata kwa Dr Shika? matendo ya ajabuajabu yaweza kukufanya ufatiliwe sana
Mtu ambaye humpendi unamfuatilia wa nini? Kwa taarifa yako anayependwa "kweri kweri" maana yake na taarifa zake zinapendwa "kweri kweri". Leo hii hamuandiki taarifa za Lissu kwasababu kwanza hazipo na pili hazipendwi ndio maana sasa hivi uko runingani umekodolea TBC1 ili tu umuone Rais Magufuli amevaa nini, anatembeaje, anaongeaje na kaongea nini kisha uwe wa kwanza kupost. Huo unaitwa umaarufu na kupendwa " kweri kweri"!
 
zipompa

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
5,798
2,000
Kama sio Kitwanga kuchemsha akiwa waziri mpaka leo hii angekuwa sehemu ya baraza la mawaziri.

Kitwanga na JPM ni watu wenye kufahamiana kwa miaka mingi ni marafiki wa karibu.

Rais ni binadamu kama mwingine yoyote yule, anao marafiki wa kikazi na wale wa karibu.
Uko sahihi sana kitwanga na jpm ni washkaji sana hivyo utani baina yao ni kawaida.

sijaona ubaya katika hili,maana kuna clip ile jpm anasema akipewa uraisi watz watalimia meno kitwanga yupo anamzingua jpm kwamba tulia ueleweshwe haya mambo huyajui (kiutani ) hawa jamaa kuchukulia serious utani wao nk kuhangaika tu.
 
Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
12,194
2,000
Uko sahihi sana kitwanga na jpm ni washkaji sana hivyo utani baina yao ni kawaida.

sijaona ubaya katika hili,maana kuna clip ile jpm anasema akipewa uraisi watz watalimia meno kitwanga yupo anamzingua jpm kwamba tulia ueleweshwe haya mambo huyajui (kiutani ) hawa jamaa kuchukulia serious utani wao nk kuhangaika tu.
Mleta mada anahamishia machungu ya maisha yake kwenye urafiki wa Kitwanga na JPM, ataishia kuumia tu moyoni.
 
Abul Aaliyah

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
2,402
2,000
Nafac hyo p1 na ubinaadamu ila inahtaji umakin sana ktk kutenda na kutamka kila jambo
 
Top Bottom