Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,252
- 113,647
Hatimaye siku ya siku imetimia.
CCM wamemtimua Bernard Membe.
Sababu ambayo inazungumziwa na wajuvi wa mambo ya kisiasa na siasa za Tanzania ni kwamba katimuliwa ili ashindwe kugombea uteuzi wa kuwa mgombea nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi hapo baadaye mwaka huu kwenye Uchaguzi Mkuu.
Kama angegombea uteuzi huo, basi kitendo hicho kingeandika sura mpya katika siasa za CCM kwani sikumbuki kabisa kama imewahi kutokea huko nyuma Rais kutoka CCM kupata ushindani toka ndani ya chama chake wakati wa kugombea muhula wa pili.
Kitendo hiki cha leo kimenikumbusha yaliyotokea miaka michache iliyopita katika CHADEMA.
CHADEMA waliwafukuza Zitto Kabwe, Kitila Mkumbo, na Samson Mwigamba kwa kile kilichodaiwa kuwa walikuwa wanasuka njama za kumuondoa Mwenyekiti wao, Bw. Freeman Mbowe.
Sasa kama hivyo ndivyo ilivyokuwa, kimsingi, kuna tofauti gani na walichokifanya CCM leo?
Sioni kilicho tofauti. Nyie mnaona?
NB: Naweza nikakosea, lakini sidhani kama Membe atadumu sana kuwa nje ya CCM. Ni suala la muda tu.
I see them kissing and making up at some point....