Kuna tofauti gani kati ya wale na huyu?

Bwashee, kama hii kitu siyo MPASUKO na kwamba sio CCM ilompokonya uanachama bali ni A GANG ndani ya chama, kwa maana kambi iliyo tofauti na "wenye CCM" basi naaminishwa kwamba hii muvi haitoishia hapo. Kama hili lilitarajiwa, was an expected move, contingent measures zitathibitika kimkakati siku za usoni. Kama ni kweli kwamba hata TAASISI imeathirika na "mwambafication" na consolidation ya POWERS nategemea hii iwe nafasi ingine ya kutimia ule unabii .... kwamba upinzani wa kweli sasa utatokea ndani ya CCM. Watu wote hawatodanganyika all the time ila huenda ramli ikathibitisha, safari hii aloguswa atanuka.
 
Bwashee, kama hii kitu siyo MPASUKO na kwamba sio CCM ilompokonya uanachama bali ni kambi iliyo tofauti na "wenye CCM" basi naaminishwa kwamba hii muvi haitoishia hapo. Kama hili lilitarajiwa, an expected move, contingent measures zitathibitika kimkakati siku za usoni. Else kama ni kweli kwamba hata KITENGO imeathirika na "umwambafication" katika consolidation ya POWERS, then hii pia ni nafasi ingine ya kutimia ule unabii.... " ya kwamba upinzani wa kweli utatokea ndani ya CCM". NIGUSE NINUKE?. Au TIMING ilishawezesha kupatikana kwa MARASHI mahsusi kwa hilo. Mwisho wa siku kama kinachogombewa ni MADARAKA na sio nafasi ya kuwapa Wadanganyika UTUMISHI ULIOTUKUKA basi hapo HAFAI MTU. Thithi thio JAMHURI YA KIDIZI ... we aint no bana republic yet.
 
Nyani Ngabu, Membe hawezi kwenda upinzani. Membe alikuwa anajijenga kuelekea 2025. Sema tatizo la jiwe hajiamini lkn ukweli hakuna mtu akiwemo membe ambaye angempinga mwaka huu 2020. Membe atarejea ccm km ccm itabaki maana nna wasiwasi ccm ikamfia mkononi jiwe. Watu anaofanya nao kazi jiwe wote hawaaminiki. Kwenye safu yake yote watu pekee watiifu kwake ni H.polepole,benson bana na gerson msigwa wengine wote ni nidhamu ya woga tu na hawa ndo wanakuja kumuumbua jiwe,
Utakuwa humjui Lepolepo...mtiifu huyu?
 
ila Jiwe ni mwanasiasa mjanja kuliko hata JK. Hakuna sasa hivi sijui cha mtoto wa Mjini wala nini. Ni kawaida wakati uchaguzi unakaribia waliotangulia walikuwa wanalegeza kidogo nyongeza za mshahara vitu kushuka Jiwe wala hata hajali kashatucontained. Sasahivi wajanja tutamuacha atawale tu atakavyopenda bora mkono uende kinywani
Mkono utaupeleka kinywani ukiwa umeshika nini? Au kulambisha vidole tu?
 
Hatimaye siku ya siku imetimia.

CCM wamemtimua Bernard Membe.

Sababu ambayo inazungumziwa na wajuvi wa mambo ya kisiasa na siasa za Tanzania ni kwamba katimuliwa ili ashindwe kugombea uteuzi wa kuwa mgombea nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi hapo baadaye mwaka huu kwenye Uchaguzi Mkuu.

Kama angegombea uteuzi huo, basi kitendo hicho kingeandika sura mpya katika siasa za CCM kwani sikumbuki kabisa kama imewahi kutokea huko nyuma Rais kutoka CCM kupata ushindani toka ndani ya chama chake wakati wa kugombea muhula wa pili.

Kitendo hiki cha leo kimenikumbusha yaliyotokea miaka michache iliyopita katika CHADEMA.

CHADEMA waliwafukuza Zitto Kabwe, Kitila Mkumbo, na Samson Mwigamba kwa kile kilichodaiwa kuwa walikuwa wanasuka njama za kumuondoa Mwenyekiti wao, Bw. Freeman Mbowe.

Sasa kama hivyo ndivyo ilivyokuwa, kimsingi, kuna tofauti gani na walichokifanya CCM leo?

Sioni kilicho tofauti. Nyie mnaona?

NB: Naweza nikakosea, lakini sidhani kama Membe atadumu sana kuwa nje ya CCM. Ni suala la muda tu.

I see them kissing and making up at some point....

Ipo tofauti kubwa sana,mmoja ana haki za kufukuza na mwingine hana haki.
 
Umetumia Whataboutism

1. Kwani ni kosa nikitumia whataboutery?

2. Mimi sijatuhumiwa kwa jambo lolote lile. Nawazungumzia watu wengine kabisa ambao sina hata uhusiano nao. Hivyo, sijakwepa lawama wala tuhuma zozote zile dhidi yangu kwa kuonyesha madhambi ya wengine.
 
1. Kwani ni kosa nikitumia whataboutery?

2. Mimi sijatuhumiwa kwa jambo lolote lile. Nawazungumzia watu wengine kabisa ambao sina hata uhusiano nao. Hivyo, sijakwepa lawama wala tuhuma zozote zile dhidi yangu kwa kuonyesha madhambi ya wengine.
Haina noma mzee baba
 
Back
Top Bottom