Kuna tatizo kuoa mwanamke mwenye mtoto?

Jambo
Kuoa mwanamke mwenye mtoto si vibaya as long as mnapendana na mmekubaliana nyinyi kama nyinyi wawili kwanza. Wazazi hawana mamraka ya kukupangia nani uoe au usioe (jambo la kizamani), we endelea na utaratibu wa utambulisho na kulipa mahali, wazee watajirudi wenyewe baadae
Yakimkuta yakumkuta pia umshauri hivohivo.
 
Siku ninawajulisha ndugu zangu kuwa namwoa dada x ambaye amezaa, mamangu aliapa viapo vyote na kulia kikamilifu. Walioniunga mkono ni wadogo zangu wawili wa kiume tu.

Ila leo katika familia nzima, msaada wa haraka na wa dhati ambao mama huutegemea ll the time huwa ni huyu mke wangu. Sijui huwa anajisikiaje wakati alimkataa.

Ninamshukuru Mungu kwa kunipa huyu mwanamke. Ninampenda na ananipenda.
So sweet
 
Siku ninawajulisha ndugu zangu kuwa namwoa dada x ambaye amezaa, mamangu aliapa viapo vyote na kulia kikamilifu. Walioniunga mkono ni wadogo zangu wawili wa kiume tu.

Ila leo katika familia nzima, msaada wa haraka na wa dhati ambao mama huutegemea ll the time huwa ni huyu mke wangu. Sijui huwa anajisikiaje wakati alimkataa.

Ninamshukuru Mungu kwa kunipa huyu mwanamke. Ninampenda na ananipenda.
Ukute mpaka sasa mna miaka chini ya 10
 
Ikiwa bado yuko hai baba wa mtoto basi nawe subiri kulea mwanao si kuoa utajutia kosa unalo taka kufanya. Ila moyo wako ndio serikali yako, chagua kuhangaika au kuishi kwa amani.
 
Wengi hufikiri kuoa mwanamke mwenye mtoto ni rahisi kivile sio kabisa.
1. Watoto baada ya 18 yrs bado kama baba utawajibika kuwaendeleza maana ni wa kufikia tena waweza kuwa babu wakufikia ukicheza.
2. Kuwalea hasa kunidhamu yaweza kuwa tabu kwani watoto wa namna hii huamini kila kitu wanaonewa hata kama unawapa malezi bora.
3. Mgawanyo wa mali ni lazima uwape sawa na wanao wa kuzaa. Pambana kuwekeza ujanani.
4. Watoto huwa na dharau wao kwa wao na ndugu wengine ndani ya familia na kuonekana wanabaguliwa au wanajibagua kwa hiyo jenga utaratibu wa kufamilia mapema.
5. Kuna muda mtajikuta wewe na baba wa huyo mtoto mnalea familia ya wife wako na pia kuingiliana mapenzi hasa watoto wakiitaji kumuona baba yao. Usipokuwa makini unagongewa live.
Ni baadhi ya sababu tu.
Sikushauri.Tafuta mwanamke ambaye hajazaa muanze maisha pamoja.
This make sense aise, asome hapa alafu atajua kama anazika au anasafirisha
 
Hakuna madhara yoyote, ni ushamba na ujinga tu wa baadhi ya watu kufikiri mwanamke mwenye mtoto hapaswi kuolewa.
Kama umempa mimba oa wala usiulize, utamwachaje singi maza na watoto wawili!!! Utakuwa umemwongezea mlima wa kupanda bora asingekuwa na mimba yako.
 
Kwa kifupi sio kila single mother sio wife material!

Wengine wapo vizuri tu na wana tabia njema ila kuna aina yetu ya wanaume tunapenda kuzalisha na kulala mbele haijalishi wewe ni wife material ama la!

Huwa hatupendi kubanana muda wote na mwanamke mmoja kama roho! Kwahiyo oweni tu single baby mama wetu hakuna tatizo tutakuwa tu tunasaidiana polepole.
 
Kwa maoni yangu,Anayeoa ni wewe siyo wazazi wako! Maadamu umefanya utafiti na kujiridhisha kuwa alipewa mimba lakini hakuolewa huyo hana shida! Kuhusu kwenda kulipa mahari unaweza kuchukua hata Rafiki yako akaenda kutoa mahari.

Unachopaswa kuzingatia,maadamu ana mtoto ambaye hukumzaa wewe,usije kumchukia mtoto au kutomjali! FAHAMU KABISA UCHUNGU WA MWANA ANAUJUA MAMA! Hata kama Mkeo anakupenda kiasi gani HUWEZI KUMTENGA NA MWANA ALIYEMZAA!
 
Hallo ndugu zangu

Kuna jambo ambalo linanitatiza kidogo naomba ushauri kutoka kwenu


Au ni sikie ushauri Wa wazazi na mimi ni achana naye?
Nawe hamia burundi, yani mwanamke anabeba mimba kabla hata kwenu hujamtambulisha.....hapo kuna shida
 
Na utajisikiaje ndoa yake ikajawa na upendo wa hali ya juu, baraka na mafanikio kama ndoa ya mkuu Lihakanga?
Love is all about intensive feelings of caring over your partner mengine yanafuatia nyuma kijana.
Ashindwe kua na love kwa aliyemzalisha aje kua na love kwako?
 
Back
Top Bottom