Wanaume mnaojitafuta anzisheni familia mkishajipata, mnaharibu maisha ya watu na kutengeneza single mothers wengi

Mbogo_beichee

Senior Member
Mar 31, 2021
175
484
Naomba niende kwenye point kabisa. Hii ni kwa wanaume/kaka/vijana kama mimi. Najua life ni ngumu na kwa kipindi hiki mwanaume kutafuta mpaka ukajipata sio kitu cha muda mfupi inachukua muda sana.

Basi hii isipelekee kuwatesa viumbe wa upande wa pili basi.

Utakuta mwanaume anasema ooh. Mimi kuoa mpaka nikijapata sasa kipato changu cha kulea familia hakijitoshelezi, ilo unalosema ni sawa sasa mbona unaendelea kugawa mimba kwa wadada zetu, ko hao watoto wanatakiwa kulelewa na nani aliejipata?

Wewe unasema ukijipata ndio utaoa ili uweze kulisha familia yako, wakati muda huo huo unaendelea kutengeneza familia nyingine (ili ilelewe na nani sasa).

Em kuweni WAUNGWANA BASI. Kama unataka Familia siku ukijipata basi subiri muda huo ndio utengeneze hizo familia, sio kutubuluzia wadada zetu tunaishia kuwa na SINGLE MOTHERS kibao.

Siku hizi kila ukitongoza Dem ana mtoto. Kuoa dem mwenye mtoto inaanza kuwa kawaida sasa hivi.

Demu kuwa na mtoto mmoja imeanza kuwa afadhali sasa hivi kuna madem wana watoto mpaka wa3 baba tofauti.

Hii inachosha jamani. kha.
 
Naomba niende kwenye point kabisa. Hii ni kwa wanaume/kaka/vijana kama mimi. Najua life ni ngumu na kwa kipindi hiki mwanaume kutafuta mpaka ukajipata sio kitu cha muda mfupi inachukua muda sana...
Sikuhizi vijana hawaoi wanachezea tu, sababu kuu wala sio kujipata bali sheria kandamizi za kugawana mali baada ya kujipata tena kwa kumkomoa mwanaume amgawie mke mvivu kisa tu amechangia uroda basi hudai mgao wa 50/50
 
Me nadhani suala la kubeba mimba libaki kuwa ni makubaliano ya pande zote mbili.

Haiwezekani u-date na Mwanaume hata hujui mwenendo wake Wala kufahamu Mipango yake eti umbebee mimba, itakuwa ni kujiingiza kwenye matatizo ya Usingo Mama tu

Ndiyo maana zipo njia za Uzazi wa Mpango kwaajili hiyo.

Wanawake watambue kwamba Mwanaume hakai na Mtoto, unaweza kukutana na Mwanaume DSM, kumbe Kigoma alipotoka ana Mke na Watoto
 
Me nadhani suala la kubeba mimba libaki kuwa ni makubaliano ya pande zote mbili.

Haiwezekani u-date na Mwanaume hata hujui mwenendo wake Wala kufahamu Mipango yake eti umbebee mimba, itakuwa ni kujiingiza kwenye matatizo ya Usingo Mama tu...
Ni kweli ila kwa upande wa mwanaume maisha yanabadilika na kwa upande wao pia wanaume hubadilika sana hasa anapojipata
 
Sikuhizi vijana hawaoi wanachezea tu, sababu kuu wala sio kujipata bali sheria kandamizi za kugawana mali baada ya kujipata tena kwa kumkomoa mwanaume amgawie mke mvivu kisa tu amechangia uroda basi hudai mgao wa 50/50
Kwa uzoefu nilionao mimi, wasichana wanategeshea mimba kwa kudhani kwmb nikishamzalia atanioa.

And that is the stupidiest thing to do, matokeo yake huwa inakula kwao!
 
Back
Top Bottom