Kuna tatizo kuoa mwanamke mwenye mtoto?

Hallo ndugu zangu

Kuna jambo ambalo linanitatiza kidogo naomba ushauri kutoka kwenu

Hivi kuna madhara gani ya kuoa mwanamke mwenye mtoto?

Sasa ni hivi kuna dada mmoja wa Kigoma ambaye tulipendana naye na tulivyo pendana akunificha aliniambia yeye ana mtoto
Nikamuliza situation ilikuwaje mpaka Akapata mtoto na kwanini baba mtoto hakumuoa?

Akaniambia kuwa uyo jamaa alimdanganya lakini alivyo mpa mimba yule jamaa alikimbia mimba ile na tena jamaa hakuwa mtanzania alikuwa mrundi na uko burundi ana mke na watoto Wa tatu

Sasa ki ukweli sikuamini maneno yake nilichunguza kwa majirani zake kuuliza walicho ni ambia ni ivo ivo tu

Sasa nikaona isiwe case nilienda kumtambulisha nyumbani kwetu cha ajabu wazazi wangu walivyo sikia kuwa ana mtoto kiukweli wamekataa kweli kweli nimejaribu kuwapa hali halisi ya ilivyo kuwa mpaka akapata mtoto uyo wamekula chini kweli
kibaya zaidi nimesha mpa mimba na kwao nina famika vizuri

Sasa familia wamenitenga kabisa yaani hawataki kusikia abari za uyo dada nimejaribu kuwaomba wao kama wazazi wangu basi wahende kujitambulisha kwao na mtoto na kuacha na weka Mali hawataki
Na mimi dada uyo na mpenda saana

Je ni kitumia wazee wengine ambao si Wa familia yangu kwenda kuniwekea Mali nitakuwa nime kosa?

Na ni madhara gani ambayo yanaweza kutokea pale familia wakikutenga?

Na nini ni fanye ili kumaliza tatizo hili ndugu zangu
Au ni sikie ushauri Wa wazazi na mimi ni achana naye?
Ukweli ni kwamba kuna changamoto utakutana nazo huko mbeleni kutokana na kuoa mke mwenye mtoto wenda hata huyo mrundi baada ya miaka kadhaa akaja kumuona mtoto na lazima mzaz mwenzie atatoa ushirikia maana burundi sio mbali na kama aliweza kumtia mimba hapa atashindwaje kuja kumuona mtoto, na katika kumuona mtoto wanaweza kukumbushiana maana kiporo hakihitaji moto mwingi. hapo ndio utakumbuka kwanini wazazi walikugomea. Ushauri wangu ni raha sana kuanza maisha na ambaye hajazalishwa yaani (0-0) kuliko (1-0)
 
Mkuu nishawahi kupitia wakati kama uwo ila mzee wangu,alinikalisha nakuniambia ‘mwanangu mwanamke mzuri huwa haachwi ukiona pesa njiani watu wanakwepa jua ni pesa ya kafara “ nilimuelewa nakumtii badae nikuja pata tena mwanamke bikra mkuu. Kwaiyo tumia kichwa cha juu wewe ni mwanaume, usiendeshwe na hisia.
 
Hicho ndio kirusi kinitafunacho, bora wako ana mmoja, wangu ana wawili tena kila mmoja na baba yake walah usithubutu! Utaja shika suruali mkononi, wanasumbua sana tena sana linapokuja suala la baba wa mtoto kutaka kumjulia hali mwanae hapo kubali kugongewa, acha kabisa! Narudia kusema walah usithubutu
Acha kumfundisha mtu ujinga mkuu yaani aishi kwa KUSUBIRI BAHATI?
Maskini sku zote huwaza hv
 
Watu wanatoa ushauri mzuri humu hadi raha, jf ni zaidi ya kijiwe.

Nami nakazia hapohapo, single mother haolewi atakusumbua mpaka utakoma. Hapo huyo ni mke wa jamaa we unamshikia tu akija atakugongea waziwazi au kwa kujificha.
Dah nime kata tamaa kabisa
Kila nikimcheki demu Uyu . dah na jinsi ushauri Munao nipa na muonea uruma

Maana nipo naye apa ajui nini kinacho ni fanye niwe mnyonge ana fikiri ni majukumu tu kumbe mwenzio nimepigwa na comment za jm mpaka na muona kama nyuki mbele ya macho yangu tu

Na fanya ni kimuona alivyo alafu ni mkimbie si atajitowa duniani Uyu kweli
Mmmmmmm ni makubwa
Mm nakazia usioe mwanamke mwenye mtoto utajuta mm yalinikuta tena huruma hiyo usiiweke kabisa ndio iliniponza ktk kutaka kuoa usiweke huruma mbele au kutumia hisia inatakiwa utumie akili hao wazazi wako wako sahihi mm najuta mpka kesho single mama hawafai
 
Back
Top Bottom