Kuna tatizo kuoa mwanamke mwenye mtoto?

kwisha

JF-Expert Member
Sep 9, 2021
1,666
4,365
Hallo ndugu zangu

Kuna jambo ambalo linanitatiza kidogo naomba ushauri kutoka kwenu

Hivi kuna madhara gani ya kuoa mwanamke mwenye mtoto?

Sasa ni hivi kuna dada mmoja wa Kigoma ambaye tulipendana naye na tulivyo pendana akunificha aliniambia yeye ana mtoto
Nikamuliza situation ilikuwaje mpaka Akapata mtoto na kwanini baba mtoto hakumuoa?

Akaniambia kuwa uyo jamaa alimdanganya lakini alivyo mpa mimba yule jamaa alikimbia mimba ile na tena jamaa hakuwa mtanzania alikuwa mrundi na uko burundi ana mke na watoto Wa tatu

Sasa ki ukweli sikuamini maneno yake nilichunguza kwa majirani zake kuuliza walicho ni ambia ni ivo ivo tu

Sasa nikaona isiwe case nilienda kumtambulisha nyumbani kwetu cha ajabu wazazi wangu walivyo sikia kuwa ana mtoto kiukweli wamekataa kweli kweli nimejaribu kuwapa hali halisi ya ilivyo kuwa mpaka akapata mtoto uyo wamekula chini kweli
kibaya zaidi nimesha mpa mimba na kwao nina famika vizuri

Sasa familia wamenitenga kabisa yaani hawataki kusikia abari za uyo dada nimejaribu kuwaomba wao kama wazazi wangu basi wahende kujitambulisha kwao na mtoto na kuacha na weka Mali hawataki
Na mimi dada uyo na mpenda saana

Je ni kitumia wazee wengine ambao si Wa familia yangu kwenda kuniwekea Mali nitakuwa nime kosa?

Na ni madhara gani ambayo yanaweza kutokea pale familia wakikutenga?

Na nini ni fanye ili kumaliza tatizo hili ndugu zangu
Au ni sikie ushauri Wa wazazi na mimi ni achana naye?
 
Jambo
Kuoa mwanamke mwenye mtoto si vibaya as long as mnapendana na mmekubaliana nyinyi kama nyinyi wawili kwanza. Wazazi hawana mamraka ya kukupangia nani uoe au usioe (jambo la kizamani), we endelea na utaratibu wa utambulisho na kulipa mahali, wazee watajirudi wenyewe baadae
 
Wengi hufikiri kuoa mwanamke mwenye mtoto ni rahisi kivile sio kabisa.
1. Watoto baada ya 18 yrs bado kama baba utawajibika kuwaendeleza maana ni wa kufikia tena waweza kuwa babu wakufikia ukicheza.
2. Kuwalea hasa kunidhamu yaweza kuwa tabu kwani watoto wa namna hii huamini kila kitu wanaonewa hata kama unawapa malezi bora.
3. Mgawanyo wa mali ni lazima uwape sawa na wanao wa kuzaa. Pambana kuwekeza ujanani.
4. Watoto huwa na dharau wao kwa wao na ndugu wengine ndani ya familia na kuonekana wanabaguliwa au wanajibagua kwa hiyo jenga utaratibu wa kufamilia mapema.
5. Kuna muda mtajikuta wewe na baba wa huyo mtoto mnalea familia ya wife wako na pia kuingiliana mapenzi hasa watoto wakiitaji kumuona baba yao. Usipokuwa makini unagongewa live.
Ni baadhi ya sababu tu.
Sikushauri.Tafuta mwanamke ambaye hajazaa muanze maisha pamoja.
 
Jeffrey Bezos amelelewa na baba wa kambo mwisho wa siku baada ya kuwa tajiri, baba wa kambo ndo anakula mafao ya Amazon na baba yake halisi hana mpango nae. Jaribu bahati yako mzee huwezi jua mtoto atakuja kuwa nani baadae.. Pengine ndo huyo huyo atakaekuja kukuthamini.
 
Hallo ndugu zangu

kuna jambo ambalo linanitatiza kidogo naomba ushauri kutoka kwenu

Hivi kuna madhara gani ya kuoa mwanamke mwenye mtoto?
Hivi unadhani kupenda ni sawa na damu? Kupenda sawa na mafua. Kuna kipindi mafua huisha. Oa ambae hana mtoto. Kuhusu mimba yako, acha azae mbona ya kwanza alizaa? Cha zaidi kipi? Usisahau akikua atakuchapa tu
 
Hicho ndio kirusi kinitafunacho, bora wako ana mmoja, wangu ana wawili tena kila mmoja na baba yake walah usithubutu! Utaja shika suruali mkononi, wanasumbua sana tena sana linapokuja suala la baba wa mtoto kutaka kumjulia hali mwanae hapo kubali kugongewa, acha kabisa! Narudia kusema walah usithubutu
 
Hallo ndugu zangu

kuna jambo ambalo linanitatiza kidogo naomba ushauri kutoka kwenu

Hivi kuna madhara gani ya kuoa mwanamke mwenye mtoto?
Umuhimu wa kuwa na wazazi ni kukujulisha waliyokutana nayo njiani wakati wa safari yao ya maisha ,kukusaidia kukwepa mashimo ambayo utaweza kutumbukia kirahisi sababu ya kukosa experience na barabara unayopita,unakokwenda walishakwenda tayari ,wanaweza kukadiria kwa usahihi zaidi matokeo ya maamuzi Yako ya sasa
Kwa sasa uko under influence ya bwana abdallah,sikiliza wazee wako
 
Wazazi mungu wa pili wasikilize,yakikukuta ya aidha ugonjwa ama kifo ilihali una mtoto wa watu bila ridhaa ya wazazi utatafuta mlango wa kutokea hutouona.

Mtoto wa kufikia hata um care chochote kile siku mkikosana tu kidogo na mke,mkeo huyo atakurundika na matusi mbele ya watu kuwa wamnyanyasia mwanae wakati tu pengine juzi juzi umetoka kumtibu mwanae homa kali iliyovuruga bajeti kwa tsh. 500,000.

Utalea wewe baada ya umri fulani watamchukua wenye mtoto.

Kundi la marafiki wa aliyezalia nyumbani pia ni walioshindikana shindikana tu.
Utakuja ulie na jua la kuwaka,acha kabisa yamenitokea mie.
 
Acha kugombana na familia yako kisa Mwanamke wewe kijana...
Single mother haolewi anagongwa na kuachwa...
Sasa wewe unataka kuweka kambi eti unampenda...

Kijana ‘Kwisha’ angalia utakwisha...

Kwanza unawezaje date Mwanamke aliyezalishwa na mwanaume mwingine... Maungo huwa hayarudi kama mwanzo na kiakili tiyari anabond na yule jamaa...
 
Jambo
Kuoa mwanamke mwenye mtoto si vibaya as long as mnapendana na mmekubaliana nyinyi kama nyinyi wawili kwanza. Wazazi hawana mamraka ya kukupangia nani uoe au usioe (jambo la kizamani), we endelea na utaratibu wa utambulisho na kulipa mahali, wazee watajirudi wenyewe baadae
Siku ninawajulisha ndugu zangu kuwa namwoa dada x ambaye amezaa, mamangu aliapa viapo vyote na kulia kikamilifu. Walioniunga mkono ni wadogo zangu wawili wa kiume tu.

Ila leo katika familia nzima, msaada wa haraka na wa dhati ambao mama huutegemea ll the time huwa ni huyu mke wangu. Sijui huwa anajisikiaje wakati alimkataa.

Ninamshukuru Mungu kwa kunipa huyu mwanamke. Ninampenda na ananipenda.
 
Back
Top Bottom