La MaGique
Member
- Jan 12, 2016
- 66
- 54
Kiwaki huyo mtu alikwambia sishiriki wap ndg
Kuna wale walijipa takribani wiki 2 za kuhama hao ndo sikuwaelewa.Hivi Magufuli alisema watahamia Dodoma kesho? Amesema ndani ya miaka minne! Naomba muandamane hata Leo.
Sipingani na Wewe, ila naomba niongezee uelewa; vipi Kenya??? Mbona ikulu iko Nairobi na Mombasa ni mji mwingine tu...ingawa uko kando ya bahari lakini bado siyo mji mkuu Wa Kenya, ila pia siyo kwamba nakubaliana au kupingana na mpango Wa serikali Wa kuhamia Dodoma la!!!!Wizara zitahama lakin ikulu kuhamia Dodoma *HAIWEZEKANI*
Changamoto kubwa nayoiona ni suala la ulinz na usalama,Landlocked countries znataman sana uwepo wa bahari ktk nchi zao, lkn sisi tunataka tupuuze hilo.Dodoma itabaki ikulu ndogo tu lkn main campus ni magogoni
Ni kweli hashauriki kabisaKuna mtu aliwahi niambia alisema mkuu hashauriki
Kuna tatizo kubwa sana Ikulu.
Ndio Ikulu nzima na watu wote wanaomzunguka rais katika shughuli za kila siku.
Ina maana hawatambui "Urais" ni taasisi kubwa na nyeti kuliko zote nchi nzima?
Ina maana hawatambui kuwa anachoongea au kutenda rais ndo sauti na matendo ya Tanzania nzima?
Inakuwaje wanamuacha rais atoe hutuba ngumu na zilizojaa utata kila siku? Hana washauri wa kumuambia anakosea?
Mfano, anasema akihamia dodoma atauza majengo yote ya serikali Dar es Salaam, kwa hii kauli unadhani anafikisha ujumbe gani kwa jamii ya watanzania na wasio watanzania wanofuatilia siasa za tanzania? Niambie serikali yeyote duniani inayouza majengo yake hasa kwa sehemu 'potential' kama dar es salaam? Na huko Dodoma atajenga au atakodi pia? Nyumba za serikali ziliuzwa, kipi kilipatikana baada ya hayo mauzo? Unahamia Dodoma kwa bajeti gani uliyoitenga? Hao watakaohamia wataenda kukaa wapi? Serikali ina majengo ya kupokea hizo Wizara? Wanajua idadi ya hao watakaohamia Dodoma?
Yani kila siku mapya yaanzishwa kutoka hewani na yanahitajika kutekelezwa.
Swali linakuja: Kwa bajeti ipi?
Hao washauri wanatakiwa wamwambie mambo hayaendi hivyo, serikali sio familia. Kila kitu kinatakiwa kipangwe na kutekelezwa kutokana na mpango elekezi. Jambo jipya litakalojitokeza litekelezwe bajeti inayofuatia.
Zoezi la kuhamia Dodoma linahitaji fedha nyingi sana na linatakiwa kutekelezwa kwa awamu. Ila hili la kusema hadi Septemba wawe wameshahama sio sawa kabisa. Hata hao watumishi mnawatesa na familia zao.
Pia, inavyoonekana hata hotuba zinatolewa kwa jazba au hazifanyiwi tafiti. Nimesoma sehemu anasema 'Wizara ya takwimu'. Hapa alikuwa ana maanisha nini?
Kurugenzi ya ikulu imetoa taarifa kituko haijawahi kutokea. Maswali yanakuja, inamaana wametoa kwa utashi wao kwa shinikizo?
Binafsi, nadhani Rais yupo pale kulipa kisasi na kuwakomoa watu fulani. Mtaani hali ni ngumu, biashara zinadorora. Ina maana wao hawaoni? Au wanaishi mbingu gani?
Mawaziri wanajua wanachofanya? Wana sera gani kumkomboa mwananchi wa kawaida?
Kuna tatizo Ikulu.
Mkuu. Sema haki ya mungu!wizara zitahama na taasisi zake zote dodoma asietaka kuhama aache kazi
Hivi mara yako ya mwisho kuchangia humu kwa kutoa comment ya maana ilikuwa ni lini??Wewe twambie kwanza unafanya biashara gani? Ulitegemea Magufuli atakulete hela? Umeambiwa Dodoma wana hamia kesho?
Wewe unaonekana umekubali kuishi kama mtumwa ndani ya nchi yako na unakubali chochote unacho amriwa kufanya.Ningekuwa rais, anawake wenye akili muflisi kama wewe ningewahamishi Mogadishu, Somalia. Wote!
Kwahiyo unataka kutuaminisha sisi great thinkers kuwa maandamano ndo chanzo cha maendeleo kwenye hizo nchi?Wewe unaonekana umekubali kuishi kama mtumwa ndani ya nchi yako na unakubali chochote unacho amriwa kufanya.
Usichokubaliana nae hapo ni kipi?
Nitajie nchi yoyote duniani endelevu yanye democratic government isiyo ruhusu maandamano?
Na hizi ndio akili za watanzania ambazo serikali ya ccm inapenda kuziongoza.Wewe ndiye mwenye matatizo, fanya yaliyokuleta duniani tu ambayo hayakuhusu yaache na uwaachie wenyewe, kwani usipoandamana nini kitatokea? na ukiandamana nini kitatokea? piga hesabu zako, huo muda wa kuandamana ungefanya kazi ungejiingizia sh. ngapi au ungepunguza majukumu kwa kiasi gani?
sasa jidanganyeni.
Kuna tatizo kubwa sana Ikulu.
Ndio Ikulu nzima na watu wote wanaomzunguka rais katika shughuli za kila siku.
Ina maana hawatambui "Urais" ni taasisi kubwa na nyeti kuliko zote nchi nzima?
Ina maana hawatambui kuwa anachoongea au kutenda rais ndo sauti na matendo ya Tanzania nzima?
Inakuwaje wanamuacha rais atoe hutuba ngumu na zilizojaa utata kila siku? Hana washauri wa kumuambia anakosea?
Mfano, anasema akihamia dodoma atauza majengo yote ya serikali Dar es Salaam, kwa hii kauli unadhani anafikisha ujumbe gani kwa jamii ya watanzania na wasio watanzania wanofuatilia siasa za tanzania? Niambie serikali yeyote duniani inayouza majengo yake hasa kwa sehemu 'potential' kama dar es salaam? Na huko Dodoma atajenga au atakodi pia? Nyumba za serikali ziliuzwa, kipi kilipatikana baada ya hayo mauzo? Unahamia Dodoma kwa bajeti gani uliyoitenga? Hao watakaohamia wataenda kukaa wapi? Serikali ina majengo ya kupokea hizo Wizara? Wanajua idadi ya hao watakaohamia Dodoma?
Yani kila siku mapya yaanzishwa kutoka hewani na yanahitajika kutekelezwa.
Swali linakuja: Kwa bajeti ipi?
Hao washauri wanatakiwa wamwambie mambo hayaendi hivyo, serikali sio familia. Kila kitu kinatakiwa kipangwe na kutekelezwa kutokana na mpango elekezi. Jambo jipya litakalojitokeza litekelezwe bajeti inayofuatia.
Zoezi la kuhamia Dodoma linahitaji fedha nyingi sana na linatakiwa kutekelezwa kwa awamu. Ila hili la kusema hadi Septemba wawe wameshahama sio sawa kabisa. Hata hao watumishi mnawatesa na familia zao.
Pia, inavyoonekana hata hotuba zinatolewa kwa jazba au hazifanyiwi tafiti. Nimesoma sehemu anasema 'Wizara ya takwimu'. Hapa alikuwa ana maanisha nini?
Kurugenzi ya ikulu imetoa taarifa kituko haijawahi kutokea. Maswali yanakuja, inamaana wametoa kwa utashi wao kwa shinikizo?
Binafsi, nadhani Rais yupo pale kulipa kisasi na kuwakomoa watu fulani. Mtaani hali ni ngumu, biashara zinadorora. Ina maana wao hawaoni? Au wanaishi mbingu gani?
Mawaziri wanajua wanachofanya? Wana sera gani kumkomboa mwananchi wa kawaida?
Kuna tatizo Ikulu.
Wewe tangu umezaliwa hadi leo una miaka 29-33 wazazi wako hawajaona matunda yoyote kutoka kwako...ije iwe Magufuli kuona matunda ya Serikali yake ndani ya miezi 8?...be serious bwana mdogo...Ni mwaka unakaribia kuisha tangu aingie madarakani. Mbona hatuoni matunda ya hayo madabiliko aliyoyafanya?
Hamjambo Milembe? Hoja za msingi wewe unajiuliza kama mimba uliyopata Milembe ni ya panya au ngedere.Wewe twambie kwanza unafanya biashara gani? Ulitegemea Magufuli atakulete hela? Umeambiwa Dodoma wana hamia kesho?