Isanga family
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 22,863
- 47,513
Nchi inaongozwa utadhani Serikali za mitaa au kijiji...
Please refrain your words, you ain't one of those great thinkers, not even close to it. If you really were, you hadn't asked that dumb question.Kwahiyo unataka kutuaminisha sisi great thinkers kuwa maandamano ndo chanzo cha maendeleo kwenye hizo nchi?
Wizara zitahama lakin ikulu kuhamia Dodoma *HAIWEZEKANI*
Changamoto kubwa nayoiona ni suala la ulinz na usalama,Landlocked countries znataman sana uwepo wa bahari ktk nchi zao, lkn sisi tunataka tupuuze hilo.Dodoma itabaki ikulu ndogo tu lkn main campus ni magogoni
Wewe tangu umezaliwa hadi leo una miaka 29-33 wazazi wako hawajaona matunda yoyote kutoka kwako...ije iwe Magufuli kuona matunda ya Serikali yake ndani ya miezi 8?...be serious bwana mdogo...
Kwa jinsi katiba inavosiginywa mpk dk hii waziri husika alitakiwa awe ameshajiuzulu.
Alaf wapi busara za kina mzee Mwinyi, Mzee Mkapa etc? Kuweza mpa ushauri huyu bwana anapotupeleka siko!
Kwa hili raisi kachemka, kwa hiyo kila penye majengo ya serikali yapigwe mnada sasaNikahoji nikasema kwani wizara haiwezi kufanya kazi bila kuwa karibu na Ikulu?
Haiwezekani serikali kuuza majengo ya umma sehemu muhimu kama Dar. Haiwezekan na inaonekana hata washauri wake wanaogopa kumshauri sasa hivi maana atawatumbua
Hili la kuuza haya majengo kiukweli siliungo hata kidole kabla ya mkono aseeeVipi kuhusu kuuza majengo yote ya Serikali ya Dsm
Wizara zitahama lakin ikulu kuhamia Dodoma *HAIWEZEKANI*
Changamoto kubwa nayoiona ni suala la ulinz na usalama,Landlocked countries znataman sana uwepo wa bahari ktk nchi zao, lkn sisi tunataka tupuuze hilo.Dodoma itabaki ikulu ndogo tu lkn main campus ni magogoni
Kama hujui bora ukapitia mawazo ya watu huenda yakakusaidiLabda niulize swali dogo tu. Serikali ikitoka dar hiyo potential itatoka wapi? It will only be a useless, big shopping mall lisilo na maana.
Kama hujui bora ukapitia mawazo ya watu huenda yakakusaidi
Hujui umuhimu wa dar mpaka leo??
Dar ni mji wa kibiashara na rena hili la luhama utaongezewa hadhi na kuwa mji wa kihistoria umelitunza taifa kwa miaka zaidi ta 50, na baadae serikali ikahamia dodoma ikiwa salama salimin
Sasa hili la kuuza haya majengo likitimia itakua aibu siku tukikuta ikulu yetu imegeuka hoteli inayomilikiwa na mchina kisa ilipigwa mnada
Hapa ntakataa mpaka kufa
Kuna tatizo kubwa sana Ikulu.
Ndio Ikulu nzima na watu wote wanaomzunguka rais katika shughuli za kila siku.
Ina maana hawatambui "Urais" ni taasisi kubwa na nyeti kuliko zote nchi nzima?
Ina maana hawatambui kuwa anachoongea au kutenda rais ndo sauti na matendo ya Tanzania nzima?
Inakuwaje wanamuacha rais atoe hutuba ngumu na zilizojaa utata kila siku? Hana washauri wa kumuambia anakosea?
Mfano, anasema akihamia dodoma atauza majengo yote ya serikali Dar es Salaam, kwa hii kauli unadhani anafikisha ujumbe gani kwa jamii ya watanzania na wasio watanzania wanofuatilia siasa za tanzania? Niambie serikali yeyote duniani inayouza majengo yake hasa kwa sehemu 'potential' kama dar es salaam? Na huko Dodoma atajenga au atakodi pia? Nyumba za serikali ziliuzwa, kipi kilipatikana baada ya hayo mauzo? Unahamia Dodoma kwa bajeti gani uliyoitenga? Hao watakaohamia wataenda kukaa wapi? Serikali ina majengo ya kupokea hizo Wizara? Wanajua idadi ya hao watakaohamia Dodoma?
Yani kila siku mapya yaanzishwa kutoka hewani na yanahitajika kutekelezwa.
Swali linakuja: Kwa bajeti ipi?
Hao washauri wanatakiwa wamwambie mambo hayaendi hivyo, serikali sio familia. Kila kitu kinatakiwa kipangwe na kutekelezwa kutokana na mpango elekezi. Jambo jipya litakalojitokeza litekelezwe bajeti inayofuatia.
Zoezi la kuhamia Dodoma linahitaji fedha nyingi sana na linatakiwa kutekelezwa kwa awamu. Ila hili la kusema hadi Septemba wawe wameshahama sio sawa kabisa. Hata hao watumishi mnawatesa na familia zao.
Pia, inavyoonekana hata hotuba zinatolewa kwa jazba au hazifanyiwi tafiti. Nimesoma sehemu anasema 'Wizara ya takwimu'. Hapa alikuwa ana maanisha nini?
Kurugenzi ya ikulu imetoa taarifa kituko haijawahi kutokea. Maswali yanakuja, inamaana wametoa kwa utashi wao kwa shinikizo?
Binafsi, nadhani Rais yupo pale kulipa kisasi na kuwakomoa watu fulani. Mtaani hali ni ngumu, biashara zinadorora. Ina maana wao hawaoni? Au wanaishi mbingu gani?
Mawaziri wanajua wanachofanya? Wana sera gani kumkomboa mwananchi wa kawaida?
Kuna tatizo Ikulu.
Wewe ni kutetea kila kitu, humsaidii.Wewe twambie kwanza unafanya biashara gani? Ulitegemea Magufuli atakulete hela? Umeambiwa Dodoma wana hamia kesho?