Kuna tatizo kubwa sana IKULU

Kuna tatizo kubwa sana IKULU

Uoga tu unawasumbua watu...

"Change Management"ndio swala la msingi.

Kila kitu anachofanya JPM lazima atakuwa amefanya consultation lakini kwa kuwa maamuzi aliyofanya yanaathiri "maslahi" ndio maana mnatoka povu.

Mwanzo wa jambo lolote haukosi changamoto. ...

Hapa agenda ni kuhamia dodoma hizo ngonjera nyingine zisubiri baadae
 
Nani atakaepitisha gharama za kuhamisha makao makuu ya wizara na idara za serikali kwenda Dodoma na ni lini?
 
Hivi kwannn nchi nzima tusiandamane kwa yanayoendelea?

Nina uhakika kitendo cha kuhamia Dodoma kitasababisha umaskini nchini sababu matataizo ya msingi jhayatatatuliwa bado focus itakua kuhama tu.

Jamani huyu mtu afungiwe speed governor; huyu baba anatupeleka pabaya pabaya mno jamani umaskini utaisha lini?
Safari ya dodoma iko pale pale!
 
Kuna mtu aliwahi niambia alisema mkuu hashauriki
Makamba alifikisha ujumbe kinamna pale dodoma "watu wanasema rais hashauriki,hapana rais ana sahaurika sana ila hataki vi memo" kwa tafsiri nyepesi ana mwambia baba jesc.a uwe unakubali kushauriwa....
 
That is building castles in the air, viwanda bila umeme wapi na wapi. Umeme wa nyumbani tu ni shida na ghali tunaoteshwa ndoto za mchana kwamba tunajenga Tanzania ya viwanda! Huu ni wendawazimu. Tunataka kujenga viwanda visivyokuwa na mali ghafi, mfano viwanda vya nguo, pamba iko wapi au wakulima wamewezeshwa vipi kulima pamba?

IKULU KUNA TATIZO KUBWA, YAANI KAMA NDEGE KUBWA ANGANI ILIYOISHIWA MAFUTA, therefore let us brace for crush landing.

Tatizo sio umeme hata, ni swala la 'political will'. Kama huna, mipango yote itabaki kwenye makabrasha.
 
Uoga tu unawasumbua watu...

"Change Management"ndio swala la msingi.

Kila kitu anachofanya JPM lazima atakuwa amefanya consultation lakini kwa kuwa maamuzi aliyofanya yanaathiri "maslahi" ndio maana mnatoka povu.

Mwanzo wa jambo lolote haukosi changamoto. ...

Hapa agenda ni kuhamia dodoma hizo ngonjera nyingine zisubiri baadae

Ni mwaka unakaribia kuisha tangu aingie madarakani. Mbona hatuoni matunda ya hayo madabiliko aliyoyafanya?
 
Kuna tatizo kubwa sana Ikulu.

Ndio Ikulu nzima na watu wote wanaomzunguka rais katika shughuli za kila siku.

Ina maana hawatambui "Urais" ni taasisi kubwa na nyeti kuliko zote nchi nzima?

Ina maana hawatambui kuwa anachoongea au kutenda rais ndo sauti na matendo ya Tanzania nzima?

Inakuwaje wanamuacha rais atoe hutuba ngumu na zilizojaa utata kila siku? Hana washauri wa kumuambia anakosea?

Mfano, anasema akihamia dodoma atauza majengo yote ya serikali Dar es Salaam, kwa hii kauli unadhani anafikisha ujumbe gani kwa jamii ya watanzania na wasio watanzania wanofuatilia siasa za tanzania? Niambie serikali yeyote duniani inayouza majengo yake hasa kwa sehemu 'potential' kama dar es salaam? Na huko Dodoma atajenga au atakodi pia? Nyumba za serikali ziliuzwa, kipi kilipatikana baada ya hayo mauzo? Unahamia Dodoma kwa bajeti gani uliyoitenga? Hao watakaohamia wataenda kukaa wapi? Serikali ina majengo ya kupokea hizo Wizara? Wanajua idadi ya hao watakaohamia Dodoma?

Yani kila siku mapya yaanzishwa kutoka hewani na yanahitajika kutekelezwa.

Swali linakuja: Kwa bajeti ipi?

Hao washauri wanatakiwa wamwambie mambo hayaendi hivyo, serikali sio familia. Kila kitu kinatakiwa kipangwe na kutekelezwa kutokana na mpango elekezi. Jambo jipya litakalojitokeza litekelezwe bajeti inayofuatia.

Zoezi la kuhamia Dodoma linahitaji fedha nyingi sana na linatakiwa kutekelezwa kwa awamu. Ila hili la kusema hadi Septemba wawe wameshahama sio sawa kabisa. Hata hao watumishi mnawatesa na familia zao.

Pia, inavyoonekana hata hotuba zinatolewa kwa jazba au hazifanyiwi tafiti. Nimesoma sehemu anasema 'Wizara ya takwimu'. Hapa alikuwa ana maanisha nini?

Kurugenzi ya ikulu imetoa taarifa kituko haijawahi kutokea. Maswali yanakuja, inamaana wametoa kwa utashi wao kwa shinikizo?

Binafsi, nadhani Rais yupo pale kulipa kisasi na kuwakomoa watu fulani. Mtaani hali ni ngumu, biashara zinadorora. Ina maana wao hawaoni? Au wanaishi mbingu gani?

Mawaziri wanajua wanachofanya? Wana sera gani kumkomboa mwananchi wa kawaida?

Kuna tatizo Ikulu.
kwa kaui kama hizi,nina hakika kuna INVESTORS,wameshabaki STRANDED,yaani uchumi unaendelea kusimama UNLESS kuna hidden agenda.
 
Jibu hoja ya maana kwa hoja iliyoenda shule. Usijaze nyuzi za watu kwa hoja za kipuuzi.

Na wewe usilete mada na malalamiko ya kipuuzi, raisi keshasema kabla ya 2020 atakuwa amekamilisha mipango ya kuhama. Haya mambo ni complex sana, na usichukulie kauli zote haswa za wanasiasa serious. Chill, ifikapo 2020 hakuna kitu kimefanyika ndio uanze dodosa hilo tatizo kubwa lilipo ikulu, sasa hivi ni upashkuna tu unaleta, so far ikulu ina perform good.
 
Kuna tatizo kubwa sana Ikulu.

Ndio Ikulu nzima na watu wote wanaomzunguka rais katika shughuli za kila siku.

Ina maana hawatambui "Urais" ni taasisi kubwa na nyeti kuliko zote nchi nzima?

Ina maana hawatambui kuwa anachoongea au kutenda rais ndo sauti na matendo ya Tanzania nzima?

Inakuwaje wanamuacha rais atoe hutuba ngumu na zilizojaa utata kila siku? Hana washauri wa kumuambia anakosea?

Mfano, anasema akihamia dodoma atauza majengo yote ya serikali Dar es Salaam, kwa hii kauli unadhani anafikisha ujumbe gani kwa jamii ya watanzania na wasio watanzania wanofuatilia siasa za tanzania? Niambie serikali yeyote duniani inayouza majengo yake hasa kwa sehemu 'potential' kama dar es salaam? Na huko Dodoma atajenga au atakodi pia? Nyumba za serikali ziliuzwa, kipi kilipatikana baada ya hayo mauzo? Unahamia Dodoma kwa bajeti gani uliyoitenga? Hao watakaohamia wataenda kukaa wapi? Serikali ina majengo ya kupokea hizo Wizara? Wanajua idadi ya hao watakaohamia Dodoma?

Yani kila siku mapya yaanzishwa kutoka hewani na yanahitajika kutekelezwa.

Swali linakuja: Kwa bajeti ipi?

Hao washauri wanatakiwa wamwambie mambo hayaendi hivyo, serikali sio familia. Kila kitu kinatakiwa kipangwe na kutekelezwa kutokana na mpango elekezi. Jambo jipya litakalojitokeza litekelezwe bajeti inayofuatia.

Zoezi la kuhamia Dodoma linahitaji fedha nyingi sana na linatakiwa kutekelezwa kwa awamu. Ila hili la kusema hadi Septemba wawe wameshahama sio sawa kabisa. Hata hao watumishi mnawatesa na familia zao.

Pia, inavyoonekana hata hotuba zinatolewa kwa jazba au hazifanyiwi tafiti. Nimesoma sehemu anasema 'Wizara ya takwimu'. Hapa alikuwa ana maanisha nini?

Kurugenzi ya ikulu imetoa taarifa kituko haijawahi kutokea. Maswali yanakuja, inamaana wametoa kwa utashi wao kwa shinikizo?

Binafsi, nadhani Rais yupo pale kulipa kisasi na kuwakomoa watu fulani. Mtaani hali ni ngumu, biashara zinadorora. Ina maana wao hawaoni? Au wanaishi mbingu gani?

Mawaziri wanajua wanachofanya? Wana sera gani kumkomboa mwananchi wa kawaida?

Kuna tatizo Ikulu.
Suala la Katiba halikuwa na bajeti
pesa zilitoka wapi?
Kwa nini wapinzani wasinge pinga ?
 
Nasubiri mikutano ya leo kuna jipya gani atasema ,maana aamekuwa mtu wa kusema tu hakuna vitendo
 
Ni mwaka unakaribia kuisha tangu aingie madarakani. Mbona hatuoni matunda ya hayo madabiliko aliyoyafanya?

Maskini wenye watoto wanaona mabadiliko, sasa wanawapeleka watoto wao shule bure, Hilo ni moja tu
 
acha upuuzi wewe wafanyakazi wote wa serikali lazima wahamie dodoma
Kuhamia Dodoma siyo tatizo ila suala la kulazimisha wizara ihame bila maandalizi yoyote ndiyo tatizo kama anavyotaka kulazimisha Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi aliyesema wahamie next week ! !!!!
 
Mh. Rais alisema atahakikisha ndani ya miaka minne na miezi minne iliyobaki serikali itakua imehamia dodoma. Aliyesema atahamia dodoma mwezi septemba ni mh waziri mkuu. Kuna kipengele hapo juu umemnkuu kimakosa mh rais, nilikua narekebisha
Kila waziri naye amekurupuka kuwa haiwezakani waziri Mkuu akatutangulia wanatakiwa wawahi wao kwanza!
Picha hii inaonesha hakuna plans!
Hapakuwa na haja ya waziri Mkuu kusema yeye ataenda September au mwingine akajibizana na wenzake!
Huu mpango unapaswa kuwa na taratibu, nani aende kwanza, kwa bajeti ipi na umuhimu upi! Bila orders hatutofanikiwa!
Hili taifa litadidimia kwa ufukara, watu wanaamua masuala ya kitaifa kama jinsi mtu anavyoamua kubadili shuka chumbani kwake!
 
hii serikali ya ccm ni ya ajabu ktk kuhamia dodoma tukiacha insu za majengo kama ofisi kuna vitu viwili ambavyo vinahitaji rasilimali fedha za kutosha na muda
1.kuna insu ya makazi ya wafanyakazi ktk wizara zote kasoro hiyo ya tamisemi,pia magufuli itabidi avunje baadhi ya sheria za wafanyakazi pale anapohamishwa ni lazima alipwe hizo fedha zote zitatoka wapi
2.kubwa zaidi installation ya mifimo ya utendaji wa kazi ktk wizara zote mfano mifumo ya fedha wizara ya fedha,kufanya installation ya mifumo ni kitu kinacho hitaji pesa nyingi
 
Mimi sishtuki sana na hili la kuhamia dodoma kwa pupa na wala silitilii sana umuhimu coz nina imani ndani ya hizi ziara anazofanya wiki hii, ataibuka na kipaumbele (mpango) kipya na upepo na washabiki wake wote watahamia kushangilia mpango mpya....dodoma tutatia kapuni. Hivi la viwanda limeishia wapi vileeee?? 🙁
 
Kuna tatizo kubwa sana Ikulu.

Ndio Ikulu nzima na watu wote wanaomzunguka rais katika shughuli za kila siku.

Ina maana hawatambui "Urais" ni taasisi kubwa na nyeti kuliko zote nchi nzima?

Ina maana hawatambui kuwa anachoongea au kutenda rais ndo sauti na matendo ya Tanzania nzima?

Inakuwaje wanamuacha rais atoe hutuba ngumu na zilizojaa utata kila siku? Hana washauri wa kumuambia anakosea?

Mfano, anasema akihamia dodoma atauza majengo yote ya serikali Dar es Salaam, kwa hii kauli unadhani anafikisha ujumbe gani kwa jamii ya watanzania na wasio watanzania wanofuatilia siasa za tanzania? Niambie serikali yeyote duniani inayouza majengo yake hasa kwa sehemu 'potential' kama dar es salaam? Na huko Dodoma atajenga au atakodi pia? Nyumba za serikali ziliuzwa, kipi kilipatikana baada ya hayo mauzo? Unahamia Dodoma kwa bajeti gani uliyoitenga? Hao watakaohamia wataenda kukaa wapi? Serikali ina majengo ya kupokea hizo Wizara? Wanajua idadi ya hao watakaohamia Dodoma?

Yani kila siku mapya yaanzishwa kutoka hewani na yanahitajika kutekelezwa.

Swali linakuja: Kwa bajeti ipi?

Hao washauri wanatakiwa wamwambie mambo hayaendi hivyo, serikali sio familia. Kila kitu kinatakiwa kipangwe na kutekelezwa kutokana na mpango elekezi. Jambo jipya litakalojitokeza litekelezwe bajeti inayofuatia.

Zoezi la kuhamia Dodoma linahitaji fedha nyingi sana na linatakiwa kutekelezwa kwa awamu. Ila hili la kusema hadi Septemba wawe wameshahama sio sawa kabisa. Hata hao watumishi mnawatesa na familia zao.

Pia, inavyoonekana hata hotuba zinatolewa kwa jazba au hazifanyiwi tafiti. Nimesoma sehemu anasema 'Wizara ya takwimu'. Hapa alikuwa ana maanisha nini?

Kurugenzi ya ikulu imetoa taarifa kituko haijawahi kutokea. Maswali yanakuja, inamaana wametoa kwa utashi wao kwa shinikizo?

Binafsi, nadhani Rais yupo pale kulipa kisasi na kuwakomoa watu fulani. Mtaani hali ni ngumu, biashara zinadorora. Ina maana wao hawaoni? Au wanaishi mbingu gani?

Mawaziri wanajua wanachofanya? Wana sera gani kumkomboa mwananchi wa kawaida?

Kuna tatizo Ikulu.
Hayo majengo ya Serikali yaliyoko Dsm ukiondoa ikulu serikali ikishahamia Dodoma yatakuwa na kazi gani tena?
Kiongozi wa juu wa serikali atakaye baki Dsm ni mkuu wa mkoa na ana ofisi yake.
Au unadhani ipo tena siku serikali itarudi Dsm baada ya kuwa imeshahamia Dodoma?
Naunga mkono serikali kuyauza na hizo pesa zijenge mengine huko inakohamia.
 
Kuhusu kuhamia Dodoma Nadhani si tatizo kwani yeye kasema atahamia ndani ya Miaka 4 na si Wizara zote zitahamia huko kwa haraka sana, pesa za kuhamia huko anayo tayari anajua alipoipata, kibaya ambacho anakifanya ni kuminya Uhuru wa vyama vya siasa ( Udikteta ) kuwazua wapinzani wasifanye mikutano na siasa ni unyanyasaji mkubwa .
 
Back
Top Bottom