Kuna tabia zinakera sana katika jamii zetu

Kuna tabia zinakera sana katika jamii zetu

Hahahahaaaaaaaaaaaaaa hahahahahaaaaaaaaaaaa daaaah nimecheka kwa kweli...!

Ok,anyway uswahilini ni kule ambapo kuna vijumba vilivyo bananabanana na havikujengwa katika utaalamu, viwanja havijapimwa mtu anajijengeajengea tu bila utaratibu vichochoro ndo usiseme...,Kumejaa majungu fitina na Umbea..
Ukiamka asubuhi unakuta watu wamekakaa tu hawajishughulishi kazi kukalia majungu, umbea na fitina.

Mfano mzuri manzese,mbagala kwa bibi nyau, temeke uswahilini,vingunguti, Buguruni ndanindani n.k

Wanatapishaga vyoo kukinyesha! Kuna sukari za kununua kwa vijiko na majani ya chai hivyohivyo. Kila mtaa kuna watoto wanacheza kifua wazi wanatirirsha kamasi na wote wana vitambi balaa...... mkaribishe Heaven on Earth uswahilini ajionee mambo 🙂

Njia za huko asilimia kubwa unakatiza korido za watu na zingine zinaisha ghafla. Utajuta kama umepotea njia na uliwapita watu bila salamu sasa unarudi kuomba uelekezwe. Watu wenyewe ukute ni full wazaramo!
 
Last edited by a moderator:
Kama hutaki kuazimisha kitu weka Gate..
Utabakia kulalama kipuzipuzii..
 
maofisini kunakera sana, hasa wamama wanapenda sana shikamoo...usiposalimia utadiskasiwa mpaka basi. hivi utakaa kunote yupi umemsalimia yupi hujamsalimia on a daily basis? hivi huwezi kuwa kwa wkt huo labda mtu hujamuona au mawazo yako mbali? inaudhi sana

You are right on point Princess:wink2:...
 
no 3 ukiishi uswazi ukijifanya huazimishi watu vitu vyako basi hata msiba wanaweza kukususia

au ukawa wezi wanakuibia wewe tu

kuna mitaa uswahilini hadi wali wanaiba....linaibiwa sufuria la wali na jiko lake la mkaa...


Dawa ya yote hayo tafuta hela uhame tu mitaa hiyo.....
the boss....
Kumbe kuna watu hadi chill souce wanaazima!!! Looh
 
No 3 ukiishi uswazi ukijifanya huazimishi watu vitu vyako basi hata msiba wanaweza kukususia

au ukawa wezi wanakuibia wewe tu

kuna mitaa uswahilini hadi wali wanaiba....linaibiwa sufuria la wali na jiko lake la mkaa...


Dawa ya yote hayo tafuta hela uhame tu mitaa hiyo.....
hahahaha TB umenikumbusha mambo mengi sana yaani nimecheka sana dah! Ila ukiishi uswahili inabidi uende nao sawa vivyo hivyo ukiishi ushuani. Inatakiwa uishi kulingana na mazingira husika.
 
Kwa kweli kuna baadhi ya mambo kwenye jamii zetu ambayo ni ya kipumbavu mno.

Unakuta watu wanakumaindi kwenye mambo ambayo hayawahusu kabisa.

Mbaya zaidi, upumbavu wao unakuwa umekithiri kiasi cha hata kutotambua ni mambo yepi yasiyowahusu.

Unakuta mtu anamaindi kisa tu mimi naishi Mbezi au Kenya.

Yeye mambo yangu yanamhusu nini?

Halafu sasa mtu mwenyewe hata hakujui na wewe humjui lakini ana fundo kwenye koromeo kisa maisha ya mtu mwingine.

Sasa kwa mfano hayo mambo ya kuazimisha watu vitu [unaweza pia ukaongeza mambo ya michango kuhusu jambo lolote lile], hivi kwani ni lazima kumuazimisha mtu kitu chako?

Yaani ni kama vile watu hawaelewi kabisa kuwa mambo mengine ni ya hiari na si lazima.

Sijui ni lini tu jamii yetu hii itaanza kuthamini watu kujali mambo yao wenyewe na kuacha kujihusisha na maisha ya wengine.

Moja kati ya mambo ambayo kwa kweli nayachukia kwa nguvu zangu zote ni hayo ya kumaindi maisha ya wengine.
Inabidi ujifunze kuna kitu kinaitwa utamaduni. Usidhani tamaduni fulani tu ndio sahihi. Kila jamii ina utaratibu wake.
 



Mimi huwa inanishangaza mtu yuko mjini kwenye jiji halafu tabia kama anaishi kwenye a small village kuna mtu alikuwa old neighbor miaka tukapoteana na hatukuwahi kuwa hata close..ni kujuana tu kijuu juu siku moja nimekutana nae kanisalimia,nikamwambia 'nimekusahau' nikumbushe.....cha ajabu akakasirika ye aliona kumwambia 'nimemsahau' kama nimemtukana... nikaona kweli waswahili tuna tabu

Hii kweli hata mimi inanikera niliwahi kukutana na school mate wangu wa primary tumemaliza miaka mingi miaka kumi imeshapita nimemsahau namuomba anikumbushe eti kakasirika, au kwny simu mtu sina mazoea naye kivile nilikuwa na #yake siku nyingi nikaifuta baada ya kuona sina mawasiliano naye siku hiyo ananipigia naona namba ngeni namuuliza eti kakasirika. Yani waswahili tuna tabu kwa kweli
 
Hahaa nimecheka kwa sauti uliposema 'ana fundo kwenye koromeo'

Kiukweli tuna tabia za ki primitive sana
au mtu anakuchukia kisa humsalimii
as kumsalimia kila mtu ni lazima.....

Mwingine atakuchukia akiamini 'unatakiwa kumsaidia'
hata kama hujui exactly shida zake since hajawahi kukwambia..
au kakwambia huoni ulazima wa kufanya hivyo ...
the list is endless...
Hizi tofuati za tamaduni tu. Tatizo sasa hivi kwenye jamii zetu tuna mkorogo wa tamaduni kwenye jamii. Ukiwa Ulaya/Amerika watu hawapati tabu kwa kuwa kwa sehemu kubwa wanakubaliana katika tamaduni sasa sisi kuna wengine usipomsalimia ni shida na kuna wengine ni poa na kuna wengine hawataki salamu. Kwa hiyo unaweza kuta A kamsoma B vibaya na kudhani hapendi salamu, A anamkaushia B ambaye kimsingi angependa salamu. Kinachotokea B anaanza kumchukia A lakini hawezi kumwambia kwa kuwa anahofia anaweza hata kutukanwa. Kinachobaki kuviziana viziana tu.
 
Nimesema hali halisi ya uswahilini lakini hizi tabia sio kwenye nyumba za upangaji tu, bunafsi nimekerwa sana na mtu ambaye ni rafiki yangu tu tena tunaishi mbali mbali, yaani mwendo waboda boda 3000, mpumbavu huyu kila akija kwangu anaazima vitu hata visivyo azimika, kwa kweli kanikwaza sana, maana aliisha haribu flash yangu ambayo nimehifadhi mambo yangu muhimu, tangu juzi kuna kitu changu nilimtaka anirudishie akawa ananikwepa leo nikamtuma mtu akanichukulie wallah!!!!!!! nilitamani kulia baada ya kuletewa, ndio maana nimesema ila nimeunga na hizo pamoja zinakera tu. mi watu mingine sijui ikoje.
Sasa kama anakukera kwa nini unaendelea kumuazima?!! Kwani lazima?
 
Nyie mnashangaa hayo kufanyika mtaani ambapo wengi wao hawako civilized, mi nilikuwa nashangaa sana miaka hiyo nikiwa bado chuoni, mtu (anayejiita msomi) ana mind issue ya kutokusalimiwa, mara fulani anaringa hasalimii, mi nikawa najiuliza hivi kama msomi analilia salamu vipi wale mama zangu wa uswahili? Siasa za ujamaa zimetuharibu sana waTanzania!
We naye na usomi wako umekariri vibaya sana. Unadhani huku uswahili akina mama wote wanalilia salamu. Kwanza wako bize kuchoma maandazi.
 
We naye na usomi wako umekariri vibaya sana. Unadhani huku uswahili akina mama wote wanalilia salamu. Kwanza wako bize kuchoma maandazi.

Kipimo kipi kinakuonesha nimekariri? Ni wapi nimekwambia wakina mama wote wanalilia salamu? Hujui kusoma au huwezi kuelewa? Haya jipe muda usome tena afu uelewe, Ukishindwa kunywa na maji kabisa, I was just curious to know , what is your problem then?
 
Watanzania wanapenda sana salamu

Sijui salamu ni chakula, usipomsalimia atakufa njaa...au salamu inawaongezea hela mfukoni? ???
Ni utamaduni. Hata ukienda Ulaya ukaanza kusalimia salimia watu watakushangaa kwa sababu sio utamaduni wao. Tatizo sisi utamaduni wetu wowote ambao ni tofauti na wa mzungu tunaudharau mwanzo mwisho! Wengi wa watu wanaodharau hizi tamaduni ndio hao wamekaa nje kidogo au wamesoma elimu ya mzungu. Hivi hamjiulizi mbona hao wazungu wenyewe wakija huku wanaiga tamaduni zetu na wanajitahidi kujifunza. Jitahidini muige na hilo la kujifunza na kuelewa tamaduni kutoka kwa wazungu basi.

Mimi pia namshangaa sana tu yule anayemshangaa mtanzania anayependa salamu. Of coz kuna baadhi ya tabia kama hizi za kuazima chilisosi inabidi ifike mahali zife kwa sababu maisha yanabadilika.
 
Hivi kusalimia kuna gharama gani?
 
Hii kweli hata mimi inanikera niliwahi kukutana na school mate wangu wa primary tumemaliza miaka mingi miaka kumi imeshapita nimemsahau namuomba anikumbushe eti kakasirika, au kwny simu mtu sina mazoea naye kivile nilikuwa na #yake siku nyingi nikaifuta baada ya kuona sina mawasiliano naye siku hiyo ananipigia naona namba ngeni namuuliza eti kakasirika. Yani waswahili tuna tabu kwa kweli


Hao wa kwenye simu ndo wanakera hadi basi
mwingine kabadili no...namba huijui anakufuata watsap
unamuuliza we nani...eti basi bana....
mimi huwa nawakjibu tu 'wasalimie'
 
Back
Top Bottom