Kuna tabia zinakera sana katika jamii zetu

Kuna tabia zinakera sana katika jamii zetu

Uswahilini ndio wapi??


Kwa Dar mfano uswahilini ni sehemu nyingi ambazo hazijapangika, hazina city plan..
Njoo kwetu buguruni gana, vingunguti kwa mnyamani na maeneo mengi ambayo hayana plani rasmi, nyumba zimejemgwa kiholela, ukitembea mtaani si aghalabu kutokea chooni kwa mtu...sehemu ambazo utakuta watu wapo tu vibarazani tangu kukuche hadi kukuchwe ni kupiga stories tu..
Hiyo ndio definition yangu...
 
Nimesema hali halisi ya uswahilini lakini hizi tabia sio kwenye nyumba za upangaji tu, bunafsi nimekerwa sana na mtu ambaye ni rafiki yangu tu tena tunaishi mbali mbali, yaani mwendo waboda boda 3000, mpumbavu huyu kila akija kwangu anaazima vitu hata visivyo azimika, kwa kweli kanikwaza sana, maana aliisha haribu flash yangu ambayo nimehifadhi mambo yangu muhimu, tangu juzi kuna kitu changu nilimtaka anirudishie akawa ananikwepa leo nikamtuma mtu akanichukulie wallah!!!!!!! nilitamani kulia baada ya kuletewa, ndio maana nimesema ila nimeunga na hizo pamoja zinakera tu. mi watu mingine sijui ikoje.

Ni kwamba hayo maisha umeyaanzisha wewe au mmeshazoea kuyaishi...
Inakuwia vigumu kukata aina ya maisha mnayoishi...
Kama unaona huwezi uwe muwazi kwa huyo rafiki yako muazima vitu.
 
Unashangaa pasi na fagio?
Uswazi hadi kopo la chumvi mnaazimana......
Ukiwasha jiko la mkaa ujue utasaidia kuwasha moto majirani hata watano

Dah... Umenikumbusha maisha flani ya uswani almost 13yrs ago. Basi pale kulikuwa na wapangaji zaidi ya watano, atakaye washa jiko mapema ajue wote watano watakuja kutaka moto, ila formula nikwamba ukichukua moto lazima utarudisha mkaa unaolingana na moto. Hapo tylipawezea na kukata mzizi wa fitina. Mkaa wenyewe ulikuwa wa mafungu unanunua fungu moja litoshe kupika ugali na mboga afu majirani watano waje kuomba moto khaaaa!!!!
 
Ni kwamba hayo maisha umeyaanzisha wewe au mmeshazoea kuyaishi...
Inakuwia vigumu kukata aina ya maisha mnayoishi...
Kama unaona huwezi uwe muwazi kwa huyo rafiki yako muazima vitu.

Siwez kumnyima mtu kitu, roho inanisuta, sema tatizo ni mtu anakuwa sio mtunzaji, dawa yake siku nyingine namziria tu.
 
Kumbe ndio profile yako ulivyo Bi_shost? Nashukuru kukufahamu...maana nilikuwa napata shida sana kukufahamu but now everthing is out...

NB: Msiwe mnaanika wajihi wenu wazi wazi hivi..wengine ni wepesi wa kusoma btn the lines....you will be kwishney..!

Nani?????
 
Nyumba za kupanga hizo, wapangaji mko mia. Hata karamu atakuja azima
 
Watanzania tunaona haya sana ndiyo maana mtu anachukuwa advantage.

Ukiishi nje sana, hasa nchi za magharibi, mishipa ya haya hukatika automatically.

Sasa, nampa mtu za uso mpaka anaomba msamaha.

Kuna watu wengi hawaongei na mimi mitaani kwa kuwa nimekataa kuwanunulia kinywaji au chakula na kuwaambia usoni "Mimi siyo ATM card yako, nafanya kazi kama wewe".

Kuna wengine wamekasirika eti nipo mjini siku ya nne lakini sijaenda kwao kuwasalimia.

Wanaonichukia zaidi ni watu wa karibu niliowakatalia kuchukuwa mizigo nje kwa ndugu zao. Nasafiri light, and that's the way I like it. Wanabaki kuduwaa na maboxi yao ya machungwa na kahawa airport, mimi huyoooo.

Watolee aibu, utaishi kwa raha.
 
Dah! Umenigusa jana nilicheka upande mwingne niuzka na aibu juu ilikuwa hivi,

aliingia mgeni rafiki wa mama sasa katoka na njaa yake kwao nasi tulishakula maana ilikuwa mida y saa 10 ivi sasa yule mgeni nikasikia ananiita kwa saut maana nilikuwa chumban na ni mbal kdogo na sebulen akasema
ME TOO naomba ugali nja inauma nikamwambia sawa maan ulibak nkaona nmpe huohuo
sasa wakat anamalizia kula akaingia SHEMEJI wa mama kuja kumsalimia mama amini usiamini hakusalimia watu wengne waliokuwepo akiwepo yule nilie mtengea chakula akaenda kumsalimu mama tu sasa yule aliekuwa anakula akasema tena
jaman ME TOO njo utoe vyombo vyako asante,

hahahah shemeji wa mama alirusha neno kali hapo hajakaa kwenye kiti.

Eti,
'ulipokuwa unakula vyombo vilikuwa vyako sasaivi sio vyako'
duh hi kaul noma kila mtu alpigwa bumbuwaz
 
Kwa kweli kuna baadhi ya mambo kwenye jamii zetu ambayo ni ya kipumbavu mno.

Unakuta watu wanakumaindi kwenye mambo ambayo hayawahusu kabisa.

Mbaya zaidi, upumbavu wao unakuwa umekithiri kiasi cha hata kutotambua ni mambo yepi yasiyowahusu.

Unakuta mtu anamaindi kisa tu mimi naishi Mbezi au Kenya.

Yeye mambo yangu yanamhusu nini?

Halafu sasa mtu mwenyewe hata hakujui na wewe humjui lakini ana fundo kwenye koromeo kisa maisha ya mtu mwingine.

Sasa kwa mfano hayo mambo ya kuazimisha watu vitu [unaweza pia ukaongeza mambo ya michango kuhusu jambo lolote lile], hivi kwani ni lazima kumuazimisha mtu kitu chako?

Yaani ni kama vile watu hawaelewi kabisa kuwa mambo mengine ni ya hiari na si lazima.

Sijui ni lini tu jamii yetu hii itaanza kuthamini watu kujali mambo yao wenyewe na kuacha kujihusisha na maisha ya wengine.

Moja kati ya mambo ambayo kwa kweli nayachukia kwa nguvu zangu zote ni hayo ya kumaindi maisha ya wengine.

kweli tupu
 
Habarini?

Jamani ukweli kuna tabia za watu zina kera sana, sijui nikukosa ustarabu, sijui ni ushamba, sijui nini ila zinakwaza sana.

  1. Tabia ya mtu anakuja nyumbani kwa mtu(mgeni) lakini ni mjuaji hadi kero, ukigeuka kidogo tayari kaparamia vitu hata visivyomuhusu kama: simu, pc, flash n.k
  2. Tabia ya mgeni kila akija anapoondoka anaazima kitu na kuondoka nacho alafu harudishi ila akija anaazima kingine inanikera sana.
  3. Tabia ya watu kuazima vitu kama fagio la ndani, ungo, CD, pasi,chillsource, n.k inakera sana.
  4. Tabia ya mtu anaazima kitu unampa kwa moyo wote, baada ya siku unakuta kile kifaa chako kinaburuzwa na kuchezewa hovyo hovyo na watoto wake, yaani kimetupwa tupwa, inanikera sana
  5. Hii ndio inakera sana, mtu anaazima kitu cha mtu cha thamani tena anapewa kikiwa kizuri lakini mtu harudishi hadi udai na siku yakukirudisha unaweza lia baada ya kukiona, unakuta kimerudi kimeharibika na kuchakaa, alafu yeye anaona sawa tu, inakera sana.

Sema tu tabia ya mtu kuazima vitu bas.
Ila ukitaka kuishi ivyo hakikisha na wewe ni Self Sustaining koz Siku ukipata shida ya kuazima kitu itakula kwako.
 
Sema tu tabia ya mtu kuazima vitu bas.
Ila ukitaka kuishi ivyo hakikisha na wewe ni Self Sustaining koz Siku ukipata shida ya kuazima kitu itakula kwako.

Kaka mim sina tatizo na mtu kuazima ila kuna vitu vingine si vyakuazima, pia mtu akiazima kitu cha mtu basi atunze vizuri, mim napenda mtu athamin kitu nilichomwazima. Binafsi naishi na mwenye nyumba tu tena tunaheshimiana sana ila hata ukiacha kandambili mlangon ukiingia ukatoka tayari wamevaa hawapooo!!! Haya mambo ni ustarabu wa mtu tu, haina cha wapangaji wengi wala nin.
 
maofisini kunakera sana, hasa wamama wanapenda sana shikamoo...usiposalimia utadiskasiwa mpaka basi. hivi utakaa kunote yupi umemsalimia yupi hujamsalimia on a daily basis? hivi huwezi kuwa kwa wkt huo labda mtu hujamuona au mawazo yako mbali? inaudhi sana
 
Back
Top Bottom