Kuna tabia zinakera sana katika jamii zetu

Kuna tabia zinakera sana katika jamii zetu

Hivi kusalimia kuna gharama gani?

Shida sio gharama
shida ni kuwa 'stressed life' tunayoishi mtu wakati mwingine hata hujui umeshamsalimia au la
sasa mtu unakutana nae unaanzisha mazungumzo anakununia kisa asubuhi hukumsalimia
si utoto huo? tena mazungumzo ya kiofisi
 
Ni utamaduni. Hata ukienda Ulaya ukaanza kusalimia salimia watu watakushangaa kwa sababu sio utamaduni wao. Tatizo sisi utamaduni wetu wowote ambao ni tofauti na wa mzungu tunaudharau mwanzo mwisho! Wengi wa watu wanaodharau hizi tamaduni ndio hao wamekaa nje kidogo au wamesoma elimu ya mzungu. Hivi hamjiulizi mbona hao wazungu wenyewe wakija huku wanaiga tamaduni zetu na wanajitahidi kujifunza. Jitahidini muige na hilo la kujifunza na kuelewa tamaduni kutoka kwa wazungu basi.

Mimi pia namshangaa sana tu yule anayemshangaa mtanzania anayependa salamu. Of coz kuna baadhi ya tabia kama hizi za kuazima chilisosi inabidi ifike mahali zife kwa sababu maisha yanabadilika.

Tamaduni zibadilika
Uliza watu wa Mbeya na Sumbawanga na Iringa wanavyosalimiana
ni dakika 20 nzima kusalimiana tu..mtu atakuuliza hadi mbwa wa nyumbani kama mzima
na hapo mmekutana tu njiani...

Sasa sidhani wakija mjini wanaweza fanya hivyo....
tamadani zina evolve..na hili la kusalimiana lazima li evolve tu hakuna jinsi
 
Habarini?

Jamani ukweli kuna tabia za watu zina kera sana, sijui nikukosa ustarabu, sijui ni ushamba, sijui nini ila zinakwaza sana.

  • Tabia ya mtu anakuja nyumbani kwa mtu(mgeni) lakini ni mjuaji hadi kero, ukigeuka kidogo tayari kaparamia vitu hata visivyomuhusu kama: simu, pc, flash n.k

  • Tabia ya mgeni kila akija anapoondoka anaazima kitu na kuondoka nacho alafu harudishi ila akija anaazima kingine inanikera sana.

  • Tabia ya watu kuazima vitu kama fagio la ndani, ungo, CD, pasi,chillsource, n.k inakera sana.

  • Tabia ya mtu anaazima kitu unampa kwa moyo wote, baada ya siku unakuta kile kifaa chako kinaburuzwa na kuchezewa hovyo hovyo na watoto wake, yaani kimetupwa tupwa, inanikera sana.

  • Hii ndio inakera sana, mtu anaazima kitu cha mtu cha thamani tena anapewa kikiwa kizuri lakini mtu harudishi hadi udai na siku yakukirudisha unaweza lia baada ya kukiona, unakuta kimerudi kimeharibika na kuchakaa, alafu yeye anaona sawa tu, inakera sana.

We unakaa Tandale au gongolamboto!
 
Dah! Umenigusa jana nilicheka upande mwingne niuzka na aibu juu ilikuwa hivi,

aliingia mgeni rafiki wa mama sasa katoka na njaa yake kwao nasi tulishakula maana ilikuwa mida y saa 10 ivi sasa yule mgeni nikasikia ananiita kwa saut maana nilikuwa chumban na ni mbal kdogo na sebulen akasema
ME TOO naomba ugali nja inauma nikamwambia sawa maan ulibak nkaona nmpe huohuo
sasa wakat anamalizia kula akaingia SHEMEJI wa mama kuja kumsalimia mama amini usiamini hakusalimia watu wengne waliokuwepo akiwepo yule nilie mtengea chakula akaenda kumsalimu mama tu sasa yule aliekuwa anakula akasema tena
jaman ME TOO njo utoe vyombo vyako asante,

hahahah shemeji wa mama alirusha neno kali hapo hajakaa kwenye kiti.

Eti,
'ulipokuwa unakula vyombo vilikuwa vyako sasaivi sio vyako'
duh hi kaul noma kila mtu alpigwa bumbuwaz

yaan jiwe moja limeuwa ndege buku.duuh hyo kaul noma
 
ss wshehe salam yetu ni unique asee utapenda tuu.kukisiana mikono noma cna
 
Tamaduni zibadilika
Uliza watu wa Mbeya na Sumbawanga na Iringa wanavyosalimiana
ni dakika 20 nzima kusalimiana tu..mtu atakuuliza hadi mbwa wa nyumbani kama mzima
na hapo mmekutana tu njiani...

Sasa sidhani wakija mjini wanaweza fanya hivyo....
tamadani zina evolve..na hili la kusalimiana lazima li evolve tu hakuna jinsi
Hiyo ni kweli na ndio maana tuna huo mkorogo maana kuna wale waliobadilika ambao wanadhani kila mtu anatakiwa awe ameshabadilika kuna wale walio kati na kati ambao ukimsalimia au usipomsalimia ni sawa tu maana wanajua kuna mkorogo na kuna wale ambao hawajabadilika. Shida huwa kubwa wakikutana wale waliobadilika na wale ambao bado. Kwa sehemu kubwa wale walio kati na kati ndio wanayamudu mazingira vizuri kwa sababu wana uwezo wa kumsoma mtu haraka na kuelewa yuko katika hatua ipi ya mabadiliko.
 
Shida sio gharama
shida ni kuwa 'stressed life' tunayoishi mtu wakati mwingine hata hujui umeshamsalimia au la
sasa mtu unakutana nae unaanzisha mazungumzo anakununia kisa asubuhi hukumsalimia
si utoto huo? tena mazungumzo ya kiofisi
Okay, kupitiwa/kusahahu inatokea.

Kuna wengine sio kupitiwa kuna kuwa na kadharau fulani hivi au kujisikia. Huwezi pitiwa kila siku. Nadhani hiyo ndio inayokera watu. Lakini kama walivyosema wengine inategemea na utamaduni pia. Kwetu tumekuzwa kusalimiana (hasa mdogo kumsalimu mkubwa wako kiumri), kwa hivyo usiposalimia watu hawakuelewi sana. Kule kijijini kwangu unaweza kupigwa "fine" kama husalimii "wazee"!

Binafsi nauona ni utaratibu mzuri tu katika kudumisha mawasiliano baina ya wanajamii....
 
Kapange nyumba zisizo na utiriri wa wapangaji, uwe peke yako au wawili.

Hakuna cha utitiri au nini ni tabia tuu ya mtu tuu kuazima kipaji! nyumba za uswazi ndio zao unazima je kwa jirani fagio? never! Kuna jirani alikuja anataka kupasha chakula kwa microwave! jibu ibebe kapashie kwenu mie naogopa umeme! aibu kwani alithubutu kuibebe! nilimnyima tuu kiakili
 
unaweza sema kwa hekima sio kutusi watu ambao huwajui.sijajitosheleza lakini siazimi kitu kwa mtu na wala nafasi hiyo hakuna kwani hata jirani yangu simjui anafananaje.

Kwa kweli wewe unafanana huko na mimi kwanza sikai uswazi mie. Nakaa kwa middle class! then hata kama sina kitu lakini sina shida maana shida zangu nazimudu mwenyewe kabisa! sina chumvi nala hivyo hivyo! na hata jirani yangu simjui vizuri!

Na salam nitakusalimia pale ulipo karibu yangu siwezi kukubishia hodi ati kukusalimia! lakini niko vizuri sana kwa jamii nashiriki vizuri tuu
 
Tamaduni zibadilika
Uliza watu wa Mbeya na Sumbawanga na Iringa wanavyosalimiana
ni dakika 20 nzima kusalimiana tu..mtu atakuuliza hadi mbwa wa nyumbani kama mzima
na hapo mmekutana tu njiani...

Sasa sidhani wakija mjini wanaweza fanya hivyo....
tamadani zina evolve..na hili la kusalimiana lazima li evolve tu hakuna jinsi
Watu wanasalimiana hadi kuku, nguruwe wote wanawajulia hali
 
Kwa kweli wewe unafanana huko na mimi kwanza sikai uswazi mie. Nakaa kwa middle class! then hata kama sina kitu lakini sina shida maana shida zangu nazimudu mwenyewe kabisa! sina chumvi nala hivyo hivyo! na hata jirani yangu simjui vizuri!

Na salam nitakusalimia pale ulipo karibu yangu siwezi kukubishia hodi ati kukusalimia! lakini niko vizuri sana kwa jamii nashiriki vizuri tuu

nakuelewa kabisa
 
We mtoto wewe.........!!

Kunani??????

Unakosea sana, unashindwa kumnyima mtu kitu?

Ndo nasikia kwako leo

Uchoyo ni kipaji ndugu, unamnyima mtu ili iweje??????? tatizo ni utunzaji ila kama mtu mtunzaji na ana shida nimnyime ili nifaidike nini???????????

Sasa kama anakukera kwa nini unaendelea kumuazima?!! Kwani lazima?

Tatizo sio kuazima tatizo ni utunzaji mbaya wa vitu anavyochukua.

We unakaa Tandale au gongolamboto!
Hahahahahaha!!!!!! nilikuwa nakaa kwa mtogole sasa hivi nimehamia kwa mfuga mbwa, upo hapo?????????????
 
Sasa si ndio uache kumuazima? Au unaona poa kuendelea kukereka na utunzaji wake mbovu??!!! Hivi tunaelewana kweli hapa?

Nimekuelewa mkuu, tayari nishampa last warning ivo naamin kwa sasa nitakuwa adui yake.
 
Okay, kupitiwa/kusahahu inatokea.

Kuna wengine sio kupitiwa kuna kuwa na kadharau fulani hivi au kujisikia. Huwezi pitiwa kila siku. Nadhani hiyo ndio inayokera watu. Lakini kama walivyosema wengine inategemea na utamaduni pia. Kwetu tumekuzwa kusalimiana (hasa mdogo kumsalimu mkubwa wako kiumri), kwa hivyo usiposalimia watu hawakuelewi sana. Kule kijijini kwangu unaweza kupigwa "fine" kama husalimii "wazee"!

Binafsi nauona ni utaratibu mzuri tu katika kudumisha mawasiliano baina ya wanajamii....
Kama kuna kitu baadhi ya watanzania tunakidharau lakini ni kizuri na bora mno ni muingiliano wa kijamii tulionao. Kimsingi pamoja na ukweli kwamba kuna baadhi ya tabia kama hizi za kuazima na kutotunza vitu si nzuri kabisa. Lakini uwepo wa hizi tabia chache mbovu usifanye watu wasahau uzuri wa muingiliano uliopo kwa jamii kama ya Tanzania. Labda suala la msingi ni kuwa na mipaka na kuendana na mazingira. Nasema hivi kwa sababu tamaduni za magharibi za kila mtu na lwake zina athari hasi nyingi sana. Watu wanaugua misongo ya mawazo ya ajabu ajabu kwa sababu hawana hata mtu wa kumsalimia. Fikiria mtu anakaa labda hata miezi sita hata mtu wa kuongea naye kama jirani tu unategemea nini?

Inasemekana sana pamoja na maendeleo ya kiuchumi na teknolojia kwa nchi kama U.S tabia za kujiua zimekuwa zikiongezeka mwaka hadi mwaka. Pamoja na ukweli kuwa maisha ya kijamii waliyonayo wamarekani sio sababu pekee lakini inawezekana inachangia kwa kiasi kikubwa kwa sababu wengi wanaojiua hufikia hatua hiyo kwa kuona hakuna tena faida ya kuendelea kuishi. Hivyo basi cha msingi ni kuchukua vile vilivyo njema kutoka nchi zilizoendelea ila pia tukumbuke kuenzi tamaduni zetu nzuri.
 
Back
Top Bottom