social engineer
Member
- Jul 3, 2015
- 23
- 6
kuishi na watu kazi, watu kama hao wnakera japo inahitaji akili nyingi kuwakwepa.
Nijitathmini nini Sasa? Ni lazima kusalimia? tunapenda kukuza Mambo ambayo wala sio muhimu
80% ya mada yako ni kuchukia kuazimana vitu!!!
Lazma unakaa uswazi sana. Bado mnaazimana chilisosi, chumvi, pasi, ungo, ... dah!!!
Kibongo bongo wengi tu huwawekea wenzao vifundo kwenye makoromeo hahaaaa yao bila sababu either, kwa kumhisi vibaya, kumuona ana ringa bila sababu, na ukimzidi mtu kitu nalo ni kosa.
Hilo la kusalimia ndo sijui wanaona ni nini kuna mtu alikua anauliza kitu baada ya kutoa msaada wakaanza kumshambulia mbona husalimii, sijui nini? Hivi hapa mjini utasalimia wangapi.
Na tabia ya jamii kutaka uishi wao wapendavyo na kupangia wengine life style. Kuna vtu vingi Jamii ibadilike sasa.
Bongo, tatizo uelewa wa wengi ni mdogo sana (niko tarari kusahihishwa ktk hili)!
Hii si ktk kuazimana vitu tu..., bongo ukimzidi watu kielimu, kimaisha n.k., tayari kwao huo ni uhasama/uadui!
Wale maadui watatu (Ujinga, Maradhi na Umasikini) bado umewakaa wengi kiasi cha kwamba ukitoka tu kimaisha inakuwa kama umejenga uadui kuanzia kwa ndugu, jamaa, marafiki n.k.
Tubadilikeni jamani, hizi roho za kwanini hazitufikishi popote zaidi ya kututia vijiba vya roho!
Hahahah ilinikuta hii
Nilikuwa nafanya ofisi fulani...asubuhi moja na hataka haraka zangu za kuwahi ile napanda ngazi tu nyuma wamama watu wazima wakaanza kunisema na kuniteta.... nikaamua heri nichelewa, nikaweka ustaarabu kwenye pochi nakuwarudia....nikawapa za uso za kutosha.
Toka siku hiyo ilibidi wawe wanatabasamu wanaponiona hata kama nipo mbali...hadi nilipoondoka
lol...nimecheka hiyo ya "nikumbushe"kila nikitembelea home nakutana na watu wao wananikumbuka mimi nimewasahau basi nawaulizaga straight "hebu nikumbushe" wanakasirika sana kumbe ninakua nimewasahau kweli.
teh teh teh...bwenga weeeee!.,we unajitosheleza?
umeandika kitu nilichotaka kusema,No 3 ukiishi uswazi ukijifanya huazimishi watu vitu vyako basi hata msiba wanaweza kukususia
au ukawa wezi wanakuibia wewe tu
kuna mitaa uswahilini hadi wali wanaiba....linaibiwa sufuria la wali na jiko lake la mkaa...
Dawa ya yote hayo tafuta hela uhame tu mitaa hiyo.....
kaka yangu Mtingijoli,nimekuelewa na naheshimu msimamo wako ni kweli jamii yetu ina tabia za ajabu moja wapo ni hili suala la salamu,ila nashindwa kuafikiana na ww kwa upande wa kazini...Tukumbuke kazini ni mahali nyeti na muhimu sana ili ufanikiwe kikazi ni vyema ukawa na ushirikiano mzuri na wafanyakazi wenzio,hata wale ambao hauko nao department moja..suala muhimu hapa ni kuthamin kazi uliyonayo na kujenga uhusiano mzuri na wafanyakazi wenzio salamu inahusika hapa I think it's a matter of attitude.
Ushaona jinsi watu waishio ughaibuni wanavyoandamwa humu?
Utadhani maisha ya hao waishio ughaibuni yanawahusu watu wanaowaandama.
unaweza sema kwa hekima sio kutusi watu ambao huwajui.sijajitosheleza lakini siazimi kitu kwa mtu na wala nafasi hiyo hakuna kwani hata jirani yangu simjui anafananaje.
teh teh teh teh...hujui kama kuna watu wanaazima vitu karne hii ya 21 maana hata jirani yako hujui anafananaje!...
Mbona wewe unadanganya watu ambao huwajui?!!
Uswahilini ndio wapi??
Babu we, usijifanye wa kishua wakati sredi imekugusa hadi imekukwangua.
Rudishaaaaaaaa.
Siwez kumnyima mtu kitu, roho inanisuta, sema tatizo ni mtu anakuwa sio mtunzaji, dawa yake siku nyingine namziria tu.