Kuna tabia zinakera sana katika jamii zetu

Kuna tabia zinakera sana katika jamii zetu

Apologise lady

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2013
Posts
5,980
Reaction score
3,115
Habarini?

Jamani ukweli kuna tabia za watu zina kera sana, sijui nikukosa ustarabu, sijui ni ushamba, sijui nini ila zinakwaza sana.

  • Tabia ya mtu anakuja nyumbani kwa mtu(mgeni) lakini ni mjuaji hadi kero, ukigeuka kidogo tayari kaparamia vitu hata visivyomuhusu kama: simu, pc, flash n.k

  • Tabia ya mgeni kila akija anapoondoka anaazima kitu na kuondoka nacho alafu harudishi ila akija anaazima kingine inanikera sana.

  • Tabia ya watu kuazima vitu kama fagio la ndani, ungo, CD, pasi,chillsource, n.k inakera sana.

  • Tabia ya mtu anaazima kitu unampa kwa moyo wote, baada ya siku unakuta kile kifaa chako kinaburuzwa na kuchezewa hovyo hovyo na watoto wake, yaani kimetupwa tupwa, inanikera sana.

  • Hii ndio inakera sana, mtu anaazima kitu cha mtu cha thamani tena anapewa kikiwa kizuri lakini mtu harudishi hadi udai na siku yakukirudisha unaweza lia baada ya kukiona, unakuta kimerudi kimeharibika na kuchakaa, alafu yeye anaona sawa tu, inakera sana.
 
Wenye tabia hizo wengi wao hawana uwezo na wana tabia za "Maskini jeuri".
 
Hiyo namba 1 nakumbuka 2006 nilienda kumtembelea jamaa yangu nikakuta ugomvi akimpiga MTU (shemeji yake si kihalali) kisa jamaa (shemeji) alikuja home halafu hawajuani ila akamkuta rafiki yangu (ambaye ndo kwao) akiwa sebuleni akicheki movie ila jamaa akachukua remote akabadili channeli bila ruhusu huku akionekana kama ndo kwao kabisa
 
No 3 ukiishi uswazi ukijifanya huazimishi watu vitu vyako basi hata msiba wanaweza kukususia

au ukawa wezi wanakuibia wewe tu

kuna mitaa uswahilini hadi wali wanaiba....linaibiwa sufuria la wali na jiko lake la mkaa...

Dawa ya yote hayo tafuta hela uhame tu mitaa hiyo.....
 
Kapange nyumba zisizo na utiriri wa wapangaji, uwe peke yako au wawili.
 
80% ya mada yako ni kuchukia kuazimana vitu!!!

Lazma unakaa uswazi sana. Bado mnaazimana chilisosi, chumvi, pasi, ungo, ... dah!!!
 
Khaa!! Ukiona hizo tabia huziwezi ni simple tu. Hama huko unakoishi. Nenda kaishi kule ambako hata jirani yako humjui jina
 
Kwa kweli kuna baadhi ya mambo kwenye jamii zetu ambayo ni ya kipumbavu mno.

Unakuta watu wanakumaindi kwenye mambo ambayo hayawahusu kabisa.

Mbaya zaidi, upumbavu wao unakuwa umekithiri kiasi cha hata kutotambua ni mambo yepi yasiyowahusu.

Unakuta mtu anamaindi kisa tu mimi naishi Mbezi au Kenya.

Yeye mambo yangu yanamhusu nini?

Halafu sasa mtu mwenyewe hata hakujui na wewe humjui lakini ana fundo kwenye koromeo kisa maisha ya mtu mwingine.

Sasa kwa mfano hayo mambo ya kuazimisha watu vitu [unaweza pia ukaongeza mambo ya michango kuhusu jambo lolote lile], hivi kwani ni lazima kumuazimisha mtu kitu chako?

Yaani ni kama vile watu hawaelewi kabisa kuwa mambo mengine ni ya hiari na si lazima.

Sijui ni lini tu jamii yetu hii itaanza kuthamini watu kujali mambo yao wenyewe na kuacha kujihusisha na maisha ya wengine.

Moja kati ya mambo ambayo kwa kweli nayachukia kwa nguvu zangu zote ni hayo ya kumaindi maisha ya wengine.
 
Kwa kweli kuna baadhi ya mambo kwenye jamii zetu ambayo ni ya kipumbavu mno.

Unakuta watu wanakumaindi kwenye mambo ambayo hayawahusu kabisa.

Mbaya zaidi, upumbavu wao unakuwa umekithiri kiasi cha hata kutotambia ni mambo yepi yasiyowahusu.

Unakuta mtu anamaindi kisa tu mimi naishi Mbezi au Kenya.

Halafu sasa mtu mwenyewe hata hakujui na wewe humjui lakini ana fundo kwenye koromeo kisa maisha ya mtu mwingine.

Sasa kwa mfano hayo mambo ya kuazimisha watu vitu [unaweza pia ukaongeza mambo ya michango kuhusu jambo lolote lile], hivi kwani ni lazima kumuazimisha mtu kitu chako?

Yaani ni kama vile watu hawaelewi kabisa kuwa mambo mengine ni ya hiari na si lazima.

Sijui ni lini tu jamii yetu hii itaanza kuthamini watu kujali mambo yao wenyewe na kuacha kujihusisha na maisha ya wengine.

Moja kati ya mambo ambayo kwa kweli nayachukia kwa nguvu zangu zote ni hayo ya kumaindi maisha ya wengine.

Hahaa nimecheka kwa sauti uliposema 'ana fundo kwenye koromeo'

Kiukweli tuna tabia za ki primitive sana
au mtu anakuchukia kisa humsalimii
as kumsalimia kila mtu ni lazima.....

Mwingine atakuchukia akiamini 'unatakiwa kumsaidia'
hata kama hujui exactly shida zake since hajawahi kukwambia..
au kakwambia huoni ulazima wa kufanya hivyo ...
the list is endless...
 
Hahaa nimecheka kwa sauti uliposema 'ana fundo kwenye koromeo'

Hahahaa....

Kiukweli tuna tabia za ki primitive sana
au mtu anakuchukia kisa humsalimii
as kumsalimia kila mtu ni lazima.....

Hiyo ya salamu utapachikwa kila aina ya sifa...utaambiwa 'unajiona/ unajisikia', 'unaringa', 'unajifanya mzungu' na kila aina ya ushuzi na upuuzi.

Mwingine atakuchukia akiamini 'unatakiwa kumsaidia'
hata kama hujui exactly shida zake since hajawahi kukwambia..
au kakwambia huoni ulazima wa kufanya hivyo ...
the list is endless...

Hiyo ya msaada ndo kama janga la kitaifa. Watu wanakuwa na matarajio ya ajabu ajabu tu.

Unakuta hata jitu li stranger na lenyewe linakuwa linatarajia kupewa msaada na watu hata lisiowajua.

Kama vile kutoa msaada ni jambo la lazima na si hiari.

So ridiculous.
 
Haya maisha ya uswazi ni magumu kila kitu kuazimana mi maisha hayo siyawezi na ctakaa niyaishi kuazimana ni source ya umaskini kabisa mwishowe ukidai ni ugomvi
 
Siku nyingine akiomba usimpatie. Huu ndio mzizi wa fitina.

Wapi mnaazimana pasi,fagio,chilli source?! Hostel?!

80% ya mada yako ni kuchukia kuazimana vitu!!!

Lazma unakaa uswazi sana. Bado mnaazimana chilisosi, chumvi, pasi, ungo, ... dah!!!

Kapange nyumba zisizo na utiriri wa wapangaji, uwe peke yako au wawili.

Khaa!! Ukiona hizo tabia huziwezi ni simple tu. Hama huko unakoishi. Nenda kaishi kule ambako hata jirani yako humjui jina

Nimesema hali halisi ya uswahilini lakini hizi tabia sio kwenye nyumba za upangaji tu, bunafsi nimekerwa sana na mtu ambaye ni rafiki yangu tu tena tunaishi mbali mbali, yaani mwendo waboda boda 3000, mpumbavu huyu kila akija kwangu anaazima vitu hata visivyo azimika, kwa kweli kanikwaza sana, maana aliisha haribu flash yangu ambayo nimehifadhi mambo yangu muhimu, tangu juzi kuna kitu changu nilimtaka anirudishie akawa ananikwepa leo nikamtuma mtu akanichukulie wallah!!!!!!! nilitamani kulia baada ya kuletewa, ndio maana nimesema ila nimeunga na hizo pamoja zinakera tu. mi watu mingine sijui ikoje.
 
Hahahaa....

Hiyo ya salamu utapachikwa kila aina ya sifa...utaambiwa 'unajiona/ unajisikia', 'unaringa', 'unajifanya mzungu' na kila aina ya ushuzi na upuuzi.

Hiyo ya msaada ndo kama janga la kitaifa. Watu wanakuwa na matarajio ya ajabu ajabu tu.

Unakuta hata jitu li stranger na lenyewe linakuwa linatarajia kupewa msaada na watu hata lisiowajua.

Kama vile kutoa msaada ni jambo la lazima na si hiari.

So ridiculous.

Mimi huwa inanishangaza mtu yuko mjini kwenye jiji halafu tabia kama anaishi kwenye a small village kuna mtu alikuwa old neighbor miaka tukapoteana na hatukuwahi kuwa hata close..ni kujuana tu kijuu juu siku moja nimekutana nae kanisalimia,nikamwambia 'nimekusahau' nikumbushe.....cha ajabu akakasirika ye aliona kumwambia 'nimemsahau' kama nimemtukana... nikaona kweli waswahili tuna tabu
 
Hahaa nimecheka kwa sauti uliposema 'ana fundo kwenye koromeo'

Kiukweli tuna tabia za ki primitive sana
au mtu anakuchukia kisa humsalimii
as kumsalimia kila mtu ni lazima.....

Mwingine atakuchukia akiamini 'unatakiwa kumsaidia'
hata kama hujui exactly shida zake since hajawahi kukwambia..
au kakwambia huoni ulazima wa kufanya hivyo ...
the list is endless...

Kibongo bongo wengi tu huwawekea wenzao vifundo kwenye makoromeo hahaaaa yao bila sababu either, kwa kumhisi vibaya, kumuona ana ringa bila sababu, na ukimzidi mtu kitu nalo ni kosa.
Hilo la kusalimia ndo sijui wanaona ni nini kuna mtu alikua anauliza kitu baada ya kutoa msaada wakaanza kumshambulia mbona husalimii, sijui nini? Hivi hapa mjini utasalimia wangapi.
Na tabia ya jamii kutaka uishi wao wapendavyo na kupangia wengine life style. Kuna vtu vingi Jamii ibadilike sasa.
 
Hahahaa mkuu hapo namba 3. Mtu anaazima hadi chillsource!!!!!! huyo kweli hafai.
 
Back
Top Bottom