Kuna siri gani walimu kutokuzeeka mapema?

Habari,
Miaka nenda rudi walimu huonekana vile vile tangu nilipomuacha akifundisha.mfano miez ya juz hapa nilikwenda marangu kilimanjaro kuzika bibi yangu ambae alikuwa na miaka 112, baada ya msiba tukiwa tumekaa mahali alipita babu wa umri kidogo asie na fimbo ya kutembelea nilvyomkadiria kwa haraka nilhisi ana 95....la haula! Nilisikia sauti ya baba yangu mzazi akiitikia salamu kutoka kwa yule mzee na walisalimiana kwa dakika nne hivi.

Basi alivyopiga hatua nilimuuliza maswali huyu ni nani? Alinijibu huyu ni mwalimu wangu shule ya msingi, ila alistaafu mwaka 1978 kipindi hicho nilkwisha hitimu shule muda.

(Kumbe nilvodhani miaka yake ni 95 si kwel ni anazaidi ya 107 na kuzidi) kumbuka hana hata fimbo ya kutembelea

By the way IPO mifano mingi tu ya walimu wanaotufundisha, unakuta MTU umemaliza shule ya msingi, sekondar, chuo, ukaanzisha familia, na ndan ya familia ukabarikiwa na kuongeza kizaz kingine lakn mwalim yupo vilevile

Wakuu walimu wanasiri gani ya kutokuzeeka mapema?
Kuna research nyingi tu zimefanyika na wamegundua kuwa kukaa sehemu moja kwa muda mrefu ni hatari.... na mabaya zaidi wansema hata kama unafanya mazoezi! Wanashauri mtu awe anatembea tembea. Na ukiangalia mwalim kazi yake kila saa anatembea au kusimama.
Sitting too long can kill you, even if you exercise, study says - CNN
 
nimeyapenda sana haya mawazo yako. kwa kweli wanapokea baraka nyingi.

Lakini kikubwa ni kwamba hawana stress na kazi zao. wameridhika na maisha yao. kutokana na ugumu wa maisha hawali hata vyakula hivi vya kistarehe vinavyoleta madhara ya kisukari na pressure. wao ni ugali wao na maharage na mboga za majani, ndizi za kuchemshwa na kunywa maziwa klwa walimu kama wa kilimanjaro. Jioni wapo nyumbani na wake/waume zao. hakuna muda wa kukaa katika viti virefu vya baa. kazi zao ni hizo hizo kila mwaka, hakuna kuumiza sana akili. Wengine huku mjini fujo kibao, kila saa unawaza namna ya kupiga pesa, halafu hazishiki. Ni fujo kwa mbele maisha yote, vyakula mitaani ambavyo vimepikwa na mafuta yaliyogeuka kuwa kama oil chafu, wali, ugali vyote vimefunikwa na nailoni muda wote ili visipoe, ni sumu ya kimekali kwa kwenda mbele. Hapo hukatizi, lazima uzeeke kabla ya umri.
waalimu hoyeee
 
Hiz mada zinaanzaga katikati ya mwezi na mwisho wa mwezi!!! Wajuvi mmenielewa eee
 
Yupo Mwalimu mmoja alinifundishsa tangu awali, hivi sasa nina miaka 37 lakini teacher yupo fresh sana. Kwa kweli hata mimi inanishangaza. Pia huyu teacher ni mwanamke ana watoto 8 ila hajaolewa .
duuuuhhh watoto 8 bila ndoa...teacher alikuwa sio mchoyo aiseee
 
Back
Top Bottom