Kuna siri gani walimu kutokuzeeka mapema?

patricl

JF-Expert Member
Oct 2, 2015
431
250
Habari,
Miaka nenda rudi walimu huonekana vile vile tangu nilipomuacha akifundisha.mfano miez ya juz hapa nilikwenda marangu kilimanjaro kuzika bibi yangu ambae alikuwa na miaka 112, baada ya msiba tukiwa tumekaa mahali alipita babu wa umri kidogo asie na fimbo ya kutembelea nilvyomkadiria kwa haraka nilhisi ana 95....la haula! Nilisikia sauti ya baba yangu mzazi akiitikia salamu kutoka kwa yule mzee na walisalimiana kwa dakika nne hivi.

Basi alivyopiga hatua nilimuuliza maswali huyu ni nani? Alinijibu huyu ni mwalimu wangu shule ya msingi, ila alistaafu mwaka 1978 kipindi hicho nilkwisha hitimu shule muda.

(Kumbe nilvodhani miaka yake ni 95 si kwel ni anazaidi ya 107 na kuzidi) kumbuka hana hata fimbo ya kutembelea

By the way IPO mifano mingi tu ya walimu wanaotufundisha, unakuta MTU umemaliza shule ya msingi, sekondar, chuo, ukaanzisha familia, na ndan ya familia ukabarikiwa na kuongeza kizaz kingine lakn mwalim yupo vilevile

Wakuu walimu wanasiri gani ya kutokuzeeka mapema?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom