Kuna siku karma itaongea kwa chuki na fitina anazofanyiwa kijana huyu!

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
3,865
5,683
Habarini!
Poleni kwa mtikisiko huu wa korona na Mwenyezi Mungu atuepushe, amina! tuendelee kuchukua hatua stahiki tafadhali!

leo ni siku ya 3 kama sikosei nyimbo ya alikiba inatrend namba 01 views ni kama 1.4M. kuna mambo kidogo yananishangaza:

1. Kwanini views za huyu lazima mara zigande au zishushwe? tangu alipovunja rekodi 2017 na 'seduce me' ni kama kuna mtu 'asiyejulikana' anamfuatilia kwa karibu sana......alipojaribu kutoa mvumo wa radi 2018 kuna mambo kama hayo yalitokea.....zikisogea basi husogea taratibu sana. nina uhakika, siku tatu kitu kutrend namba moja kwa upande ule stori ingekuwa kubwa sana na views zingesogea kwa kasi mno. kuna nini?!!!!

2. Akitoa nyimbo watu humfuata sana na kujaribu kumponda kwa kila namna tofauti na wengine. alipotoa seduce me na wengine nao wakaachia muda huo huo ili kujaribu kuipoteza. alipotoa mvumo wa radi mtu fulani alisikika akisema, 'tunamkaushia ili ibume'.....baadae views zikaanza kuganda. ametoa dodo juzi, kuna mtu sijui meneja au prodyuza analeta vijembe na mafumbo eti 'kipindi hiki cha corona watu wanahitaji za kucheza na hatutaki maqaswida' sijajua ye inamuathiri vp na kwanini afuatilie. ukiacha hilo, kuna mtu alikuwa anatambulishwa siku hiyohiyo alipokuwa anazindua nyimbo yake. sijawahi kusikia alikiba akisema chochote kuhusu wao wanapotoa kazi zao au hata bila kutoa kazi zao zaidi ya kujaribu kujibu tu pale anapotajwa. humu leo umefunguliwa uzi ukisema, 'huyu ndo!' zimemwagwa sifa zake humo kedekede. thread ililetwa km jaribio la kutaka kupoteza habari za dodo!

3. Kuna ajabu gani ya kumtumia mobeto?!! eti nyimbo imepata umaarufu sababu ya mobeto. nikikumbuka mwaka jana alikiba alipofanya ziara kule tabora na umati ambao ulikuwa unampokea na kumsimamisha humo njiani, nabaki najiuliza hivi na hamisa mobeto nae ni hivyo hivyo? haya tufanye mobeto ni maarufu kuliko kiba, sasa kuna ubaya gani wa kumtumia mtu maarufu ili nawe upate umaarufu? kwani muziki si biashara jamani?!!! sasa mnataka amtumie joanah wa jf ili nyimbo yake iambulie 1k mwaka mzima?!!!

4. Kwanini watu wahangaike na mtu asiyejua kuimba/aliyeishiwa/aliyechuja kama inavyosemwa? ninapata hisia kuwa kuna mtu ana roho mbaya kwelikweli licha ya mafanikio lukuki aliyonayo. hapendi kabisa kuwaona wengine nao wakijipatia ugali wao. inawezekana yale malalamiko ya penseli yana maana kubwa sana!. hii ni hatari sana!

Many are the plans in a man's mind, but it's the God's purpose that prevails! tutajikuta tunaendelea kushangaa tu jamaa hapotei kama matamanio yetu yanavyotaka!
 
Hayo maswali unayojiuliza kuwa huyo kijana wako watu wanafanya na kusema basi tambua hata kuna vijana wengine nao wanafanyiwa hivyo hivyo. Naona mnatafuta huruma za watu pambaneni na hilo suala la views mbona limeshatolewa maelezo sana au ndio mnachagua cha kuelewa.
 
huyu jamaa amekuwa mtu wa ajabu sana wakati huu,na hii ndio sababu inamfanya yule kijana na leble yake wabaki wanahaha why!!!!!

tukiwaambia huyu mtu ana royal fans watu hawakubali,ila maisha yake ya kawaida yanaeleza mengi ambayo upande ule hautaki kuyasikia.

binafsi huwa napata wakati mgumu sana kumwelewa huyo dogo,hela umepata,umaarufu umepata,mafanikuo umepata,fanbase kubwa unayo,kwanini roho za kimasikini kwa ndugu yako njia moja????mpaka huwa najiuliza au anaelekezwa!!!!sio msimamo wake??

au kisa jamaa hatumii nguvu kula

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo maswali unayojiuliza kuwa huyo kijana wako watu wanafanya na kusema basi tambua hata kuna vijana wengine nao wanafanyiwa hivyo hivyo. Naona mnatafuta huruma za watu pambaneni na hilo suala la views mbona limeshatolewa maelezo sana au ndio mnachagua cha kuelewa.
tupambane na swala la views 1.4mln ndani ya siku 3,trending no 1.

hujui maana ya kupambana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tupambane na swala la views 1.4mln ndani ya siku 3,trending no 1.

hujui maana ya kupambana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani umepata shida kuelewa hata kiswahili chepesi kilichoandikwa hapo. Rejea tena usome vizuri,kumekuwa na malalamiko la views kuleta shida na maelezo yapo lakini watu wanachagua cha kuelewa kama vile kuna mtu kashika remote control ya youtube.

Mwisho mimi na wewe suala la trendig halina faida labda kama wewe ni meneja wa kijana huyo.
 
Nadhani umepata shida kuelewa hata kiswahili chepesi kilichoandikwa hapo. Rejea tena usome vizuri,kumekuwa na malalamiko la views kuleta shida na maelezo yapo lakini watu wanachagua cha kuelewa kama vile kuna mtu kashika remote control ya youtube.

Mwisho mimi na wewe suala la trendig halina faida labda kama wewe ni meneja wa kijana huyo.

ni kwanini akili timamu zitumike kwenye kutizama maswala ya mtu fulani na mwingine hapana!!!!

ukifungua mziki wa taarabu sauti ya juu kwa jirani kuna msiba,utaonekana mchawi tu.ila wanaofanya hivi sababu wanajua wanao followers vilaza,kwao hawatumii akili hata za kulia chakula.

mwisho halipo lenye faida hata moja kwako na kwangu,kama kila kitu kitabaki kilivyo.





Sent using Jamii Forums mobile app
 
ni kwanini akili timamu zitumike kwenye kutizama maswala ya mtu fulani na mwingine hapana!!!!

ukifungua mziki wa taarabu sauti ya juu kwa jirani kuna msiba,utaonekana mchawi tu.ila wanaofanya hivi sababu wanajua wanao followers vilaza,kwao hawatumii akili hata za kulia chakula.

mwisho halipo lenye faida hata moja kwako na kwangu,kama kila kitu kitabaki kilivyo.





Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio maana nikakwambia kiswahili chepesi lakini umeshindwa kuelewa embu soma tena hapa “......Hayo maswali unayojiuliza kuwa huyo kijana wako watu wanafanya na kusema basi tambua hata kuna vijana wengine nao wanafanyiwa hivyo hivyo.
 
Umenikumbusha movie ya Joker kuna soundtrack moja hivi inaitwa "That's Life"

Ila I think inabidi tutambue mziki ni Kazi. Mashabiki tunaonaga mziki kama Game fulani La kwenye simu Au reality Show flani hivi. Yani its like Kuna some sort of possession we have on these artists.

Kiba alivyotoa Dodo Kuna mtu Alisema Hiyo nyimbo ni Mbaya na hajaipenda kabla ht hajaiskiliza. Sasa imagine mzee Kiba siku anapita Humu jukwaani anaona that comment.

Kiba angekuwa anaishi mambele kwa maneno na figisu anazofanyiwa angekuwa kundi Moja na kina Whitney Houston au Sulli.

Thank God yuko Bongo hatuna Mental Health Crisis.
 
kibongo bongo hakuna msanii aliefanyiwa na anaefanyiwa figisu kama diamond na kila siku anawaprove wrong haters, inshort karma inawalamba sawa sawa...

pia kiba na team yake hutueleza kwao views wala trending si lolote kwao bt zikipungua wanamwaga mapovu mapipa laki 7

hua najiuliza kama kweli hazitaki views kwa nini zikipungua anapovuka vile, pia kama hazitaki kwa nini anaz iupload nyimbo zake daily, si aache zipgwe kwa radio tu ziheat mtaan basi

nimeamin kiba na team yake ni vinyonga daily wanatubadilishia maneno yakila rangi kama waimba taarabu. OVA
 
Back
Top Bottom