Sheria 12 za karma na Ufafanuzi wake kwa kifupi

2 of Amerikaz most wanted

JF-Expert Member
Jan 13, 2023
1,328
3,692
THE TWELFTH(12) LAWS OF KARMA.
SHERIA 12 ZA KARMA.

👉Neno karma ni msamiati wa lugha ya kihindi(Hinduism vocabulary) ukimaanisha jumla ya matendo au mawazo ya mtu na matokeo hufuata kwa jinsi alivyotenda au kuwaza.

Awali tuliweza kusoma ule msingi mkuu wa sheria ya KARMA kuwa unavuna ulichokipanda (what goes around comes around) ,kimsingi sheria hii ni kubwa ambapo ndani yake inatawaliwa na sheria 12 za karma wengine huzicategorize kuwa ni sheria kumi, Hilo sio tatizo kwani kila sheria huitaji Ufafanuzi ili msomaji aweze kutenganisha Katika utendaji

Karma ndio hukumu pekee hapa duniani Peponi na motoni vyote ni matokeo ya karma hivyo usitegemee Nini kitatokea baada ya kifo ili Mungu akakuhukumu Kama wafia dini waaminivyo, ukweli ni Kwamba unahukumiwa ukiwa hapa hapa duniani, Kama mwili utakufa kabla hujalipa ubaya ulioutenda Kwa wengine basi karma itakurejesha Tena ili uje kulipa kile ulichokitenda japo Katika mwili Mwingine, hapa ndipo mtu utasikia akinung'unika kuwa anamikosi lakini hakuna mkosi hakuna bahati mbaya Bali Kuna kitu kimoja na nisheria moja nayo ni KARMA unavuna ulichokipanda.

Unaposikia familia Fulani ama mtu Fulani Huwa anabahati sana basi tambua sio bahati Yani kitu au vitu vinakuja tu Kama mchezo wa kubashiri/betting Bali ni matokeo ya matendo yao au matendo yake na mawazo mazuri Kwa mtu au jamii iliyomzunguka , Kama ni Watoto kupata mafanikio basi ni matokeo ya wazazi wao kutenda wema Kwa wengine hata wakifariki basi matendo yao mema yatalipwa kwa kizazi Chao nakadhalika nakadharika....

Sheria 12 za karma na Ufafanuzi wake japo kwa kifupi👇

👉Sheria ya1: Sheria Mama ya Asili ya Kisababisho na Athari (Cause and Effect).

Hii ni sheria ya asili yenye nguvu katika kuamua mafanikio ya kila aina katika maisha yetu ya kila siku. Kubwa ni kwamba tunachojifunza kupitia sheria hii ni kila matokeo tunayopata ni zao la matendo yetu kwenye maisha ya kila siku. Tunavuna kulingana na kile tunachopanda. Ikiwa unahitaji kupata furaha, amani, upendo, na urafiki, ni lazima mtu AWE mwenye furaha, amani, upendo, na rafiki wa kweli. Hivyo, chochote ambacho mtu atapanda kwenye Ulimwengu kama mbegu ni lazima kimrudie kama matunda kulingana na mbegu alizopanda.

👉Sheria ya 2: Uumbaji.
Chochote tunachohitaji kufanikisha katika maisha ni lazima tuwe tayari kushiriki kwa maana hakuna muujiza utakaofanikisha matokeo pasipo uhusika wetu. Sisi ni wamoja na Ulimwengu ndani na nje, chochote kinachotuzunguka katika Ulimwengu huu ni kwa ajili ya kutuimarisha ndani. Hakikisha unazungukwa na yale ambayo unahitaji yatokee katika maisha yako ili kufanikisha uumbaji wake.

👉Sheria ya 3: Unyenyekevu.
Chochote unachohitaji kubadilisha katika maisha yako ni lazima kwanza ukubaliane nacho. Ikiwa ni tabia ambayo unahitaji kuibadilisha ni lazima kwanza ukubali madhaifu ya kuwa na tabia hiyo. Ikiwa ni mtu unamuona kuwa adui kwa mafanikio unayohitaji ni lazima uwe tayari kukubaliana kuachana naye kwa ajili ya kufikia kiwango cha juu cha mafanikio. Zaidi ya yote ili ufanikiwe ni lazima uwe tayari kujinyenyekea na kujiona mdogo kuliko wengine.

👉Sheria ya 4: Ukuaji.
Popote uendapo, hapo ulipo; mara zote ikiwa unahitaji kukua kiroho ni sisi ambao tunapaswa kubadilika na wala sio watu, mahali au vitu vilivyopo sehemu husika. Kitu pekee ambacho tumepewa katika kubadilika ni mamlaka juu ya nafsi zetu. Tunapobadilisha nafsi yetu kulingana na mazingira na imani zilizopo ndani ya mioyo yetu, maisha yetu yanafuatia kubadilika pia ili kuendena na mazingira mapya. Hivyo, husipambane kubadilisha watu au mazingira na badala yake pambana kufanya yanayokuhusu na mwishowe utaeleweka.

👉Sheria ya 5: Wajibu.
Ikiwa kuna kitu kibaya katika maisha yako, tambua kuwa hayo ni matokeo ya nje ambayo ni mwitikio wa kutoka ndani mwako. Hivyo, jambo lolote baya linaloonekana kwenye limeanzia ndani mwako (mfumo wako wa fikra). Tunaakisi yale yanayotuzunguka na yanayotuzunguka yanaakisi kutoka kwetu – huo ndiyo ukweli kuhusu Ulimwengu. Anza kubadilika mwenyewe kwa ajili ya kubadilisha Ulimwengu unaokuzunguka. Hivyo, lazima mtu atambue wajibu wake katika kufikia kile ambacho nahitaji katika maisha yake.

👉Sheria ya 6: Uunganisho (connection).
Vitu vidogo au vinavyoonekana kuwa vya maana sana lazima vifanyike kwa sababu kila kitu katika Ulimwengu kimeunganishwa. Kila ni muhimu kwa ajili ya hatua inayofuata, na kadhalika na kadhalika. Mtu lazima afanye kazi ya awali ili kukamilisha kazi iliyopo mbele yake. Hivyo, kila hatua ni muhimu katika ukamilisho wa matokeo unayotaka kulingana na kazi husika. Pia, ni lazima kutambua kuwa kuna muunganiko kati ya yaliyopita, yaliyopo na yajayo. Kila unalofanya sasa lina mchango chanya au hasi katika maisha yako ya baadae.

👉Sheria ya 7: Kujikita kwenye jambo moja.
Mtu hawezi kufikiria vitu viwili kwa wakati mmoja. Ikiwa mtazamo wetu uko kwenye Maadili ya Kiroho, haiwezekani kwetu kwa wakati huo huo kuwa na mawazo ya chini kama uchoyo au hasira. Hauwezi kuwa wa moto na wakati huo huo ukawa wa uvuguvugu. Kumbe, kupitia sheria hii tunatakiwa kutuliza akili yetu kwenye jambo moja linalofanyika kwa wakati husika. Epuka kuwa na fikra zilizogawanyika.

👉Sheria ya 8: Utoaji na Ukarimu.
Ikiwa mtu anaamini kitu kuwa ni kweli, basi wakati mwingine katika maisha yake atahitajika kudhihirisha ukweli huo. Hapa ndipo mazoea yanachukua mkondo wake kwa maana yapo ambayo SIYO kweli lakini kulingana na mazoea tumeaminishwa kuwa ni KWELI.

👉Sheria ya 9: Hapa na Sasa (Here & Now).
Mtu hawezi kuwa “hapa” na “sasa” ikiwa anaangalia nyuma yaliyopita au ana wasiwasi juu ya siku zijazo. Mawazo ya zamani, mitindo ya zamani, tabia za zamani, na ndoto za zamani na hofu kwa maisha yajayo hutuzuia kuwa wapya kulingana na maisha ya wakati uliopo. Tunaishi katika yaliyopita wakati hatuna nafasi ya kuyabadilisha ya kurekebisha.

👉Sheria ya 10: Badilisha.
Historia inajirudia ikiwa hatujajifunza masomo ambayo yanatakiwa kubadilishwa katika njia ya sasa. Kuna mengi ambayo tunatakiwa kujifunza kutokana na matukio ya historia ili kuepusha matukio hayo katika maisha ya sasa na wakati ujao.

👉Sheria ya 11: Uvumilivu na Thawabu.
Zawadi zote zinahitaji taabu ya awali. Tuzo za thamani ya kudumu zinahitaji uvumilivy na bidii ya muda wote. Furaha ya kweli hutokana na kufanya kile ambacho mtu anapaswa kufanya kwa kutambua kuwa tuzo itakuja kwa wakati wake.

👉Sheria ya 12: Umuhimu & Ushawishi.
Mtu anapata kutoka kwenye kitu chochote kulingana na thamani anayoweka katika kitu hiko. Thamani ya kweli ya kitu ni matokeo ya moja kwa moja ya nguvu na dhamira ambayo mhusika amweka katika kitu hiko. Kila mchango binafsi ni mchango wa wote na mchango wenye upendo huleta fura ya maisha na kuhamasisha wengine.

Mwisho niseme kuwa Kwenye elimu ya Kiroho hasa African spirituality hatuiti dhambi Bali ni uvunjifu na ukiukwaji wa sheria 12 za karma ama kwa ujumla tuseme ni kwenda Kinyume na kanuni, taratibu na sheria za ulimwengu na lazima uhukumiwe kwani karma haikosei(karma is real) ,waandishi wa biblia wakaicopy/wakainakili hivi, tusome👇

📘mathayo7:1-2
1,msihukumu ,msije mkahukumiwa ninyi 2,kwakuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayo hukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa..

Nini Kifanyike kukwepa sheria hii Kali?
👉JIBU lake ni tuishi Kwa UPENDO❤️

Imetayarishwa na :Naligia Mninoi...✍️
_20230531_213140.JPG
FB_IMG_16855573374761332.jpg
 
View attachment 2641876View attachment 2641878
kula K-VANT
 
Back
Top Bottom